Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Sio wazee wa zamani, hata sisi tulivyokuwa 20s wazazi walikuwa na uchungu na sisi hivi hivi, na madogo tulikuwa hatuwasikiizi.
Sawa nimekusikiliza! Kesho naolewa
 
Hata sio mabinti peke yao. Vijana ambao tunatafuta bado nao waliokurupuka kuoa wanaonja joto la jiwe. Mtu kisa kamaliza chuo wazazi hao mbiombio wanataka aoe au kuolewa. Kuna washkaji zangu Waislamu wao wazazi wanaandaa mazingira kijana akimaliza ataoa na atamtunza mke kwa hiki kibiashara. Sunna haiji na maneno matupu.

Sasa wazazi wengine wanawaza kuchangiwa kurudishiwa michango yao ya harusi na kutuzwa, aftermath utajua wewe. Binti ni gratuate anaolewa na mume kaajiriwa Posta kwenye ofisi binafsi zile zinakaba unatumia muda mwingi kazini, take home 600,000 alafu wanaishi Mbezi ndanindani huko maana ndio nyumba nzuri zina gharama nafuu.

Ukitazama spending ya wote kwenye familia kwa mwezi ni 550,000 na hapo kuna miujiza mtoto haumwi. Akiumwa tu hizo nauli za Mbezi kwenda hospitali mke na mtoto hawapandi daladala ni bajaj. Hapo ukweni hawajafiwa na hawajapata harusi.

Vicious cycle of poverty.
Unaongea vitu kinadharia mno mkuu.

Mtu asiyejua Lolote kuhusu Familia anaweza kukuona wewe ni shujaa wa Hoja.
 
Back
Top Bottom