Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Wadada waongo Kama huyu ,hawaolewi ng'o ,ni juzi ulisema habari za umri vidume vinajichenga alafu Sasa hivi unakuja na huu uongo tena ? Namshukuru Mungu sikuja PM maana nisingekuoa ningekuchezea kabisa
Hata ungenipata wap mahidiha unafkr tupo jf kutafuta wanaume .....akili zako kichwan hazina akili
 
Ndoa naitaka ila sio haraka hivyo! Kidogo nifikishe 25
Umebakiza miaka mingapi ufike 25? Mi ni mwanaume na miaka 27 sasa hakuna anaeniuliza kuhusu kuoa hata wazazi wangu wamepiga kimya wanaona niko sawa tu ila binafsi naona nimechelewa kuoa na ninahitaji kuoa wakati huu ili nipate muda wa kulea watoto nikiwa na nguvu changamoto ni kwamba sioni wa kumuoa naogopa kupata mwanamke pasua kichwa ambae nitashindwana nae alafu familia itawanyike binafsi naomba Mungu niwe na familia yenye utulivu ila huyo mwanamke sijakutana nae.

Je vipi we mwanamke unauhakika ukifika 25 unaweza kupata mume sahihi? Na hata ukimpata atakua tayari kukuoa ?
 
Hapana.

Nilitaka Ubainishe Mada ya Kujadiliana na Mimi maana umetaka Mjadala kwa namna Ilivyohitaji Maelezo yangu. Sasa kila mjadala lazima Mada iwekwe wazi. Kama kubainisha Hoja Kuu ni tatizo tunaweza kuendelea hivyo hivyo haina shida.
Umedai sijasema uhalisia, nikakuuliza uhalisia ni upi. Ukaniuliza hoja yangu ni ipi.
Sasa ulijuaje sijasema uhalisia wakati hujajua hoja yangu ni ipi.

Unapinga jibu, unaulizwa kama hili sio jibu basi tupatie jawabu sahihi ili tujifunze. Unaanza kuuliza hivi swali lilikuwa ni nini.

Hoja kuu nimebainisha, unadai hujaiona ila hapa umeipinga⬇️⬇️
Unaongea vitu kinadharia mno mkuu.

Mtu asiyejua Lolote kuhusu Familia anaweza kukuona wewe ni shujaa wa Hoja.
Hizo unazodai ni nadharia ndio uhalisia nilioona. Sasa nipe uhalisia wako mkuu, maana wangu umeita nadharia.
 
Kuna binti nadhani mtakuwa mnalingana nae kamaliza degree miaka 4 iliyopita, alitaka sana kuolewa na milionea ili atukomeshe macuzooo ni wiki iliyopita tu kanipigia anatafuta mume walau mwenye elimu na kazi ya kuzugia,🤣🤣 anataka mbinu za kumnasa mwanaume wa kumpa heshima ya ndoa nyie dunia iko speed, yuko very desperate kwa sasa anahaha hadi huruma nyodo zote zimemuisha

Kama hauko tayari kuolewa baki hivyo hivyo ila huko mbeleni usije sumbua watu km huyo cuzo wangu
Men get better with time, Women lose value with time.

No matter how beautiful a girl she is, on the throne of time her value decreases.

Tatizo wakiwa kwenye peak za uzuri wao huwaambii kitu.

Halafu wanakuja kushtuka Dakika za jioniiiiii....

Wanakuja JF kutafuta mume kikubwa awe anapumua tu..😄
 
Umebakiza miaka mingapi ufike 25? Mi ni mwanaume na miaka 27 sasa hakuna anaeniuliza kuhusu kuoa hata wazazi wangu wamepiga kimya wanaona niko sawa tu ila binafsi naona nimechelewa kuoa na ninahitaji kuoa wakati huu ili nipate muda wa kulea watoto nikiwa na nguvu changamoto ni kwamba sioni wa kumuoa naogopa kupata mwanamke pasua kichwa ambae nitashindwana nae alafu familia itawanyike binafsi naomba Mungu niwe na familia yenye utulivu ila huyo mwanamke sijakutana nae.

Je vipi we mwanamke unauhakika ukifika 25 unaweza kupata mume sahihi? Na hata ukimpata atakua tayari kukuoa ?
Umeongea ukweli
 
Habari!
Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'
Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja
Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
Ajabu ninayoiona hapa ni vile wewe unatafsiri msukumo huo unasababishwa na kukosa kazi! .... Lini mtagundua ukweli kuwa wanaume tunapenda sana magari? tukikosa gari iliyo zero kilimoter basi angalau tupate low mileage kidogo!

Basi na wazazi wako pia wanaogopa na wewe usiangukie kwenye high mileage category ... trust your parents, they have more than enough experience. Ujinga uliopo kwa vijana wengi ni kuamini kuwa kizazi kilichopita ni washamba na wajinga, ila kumbuka wale unaowaona hivo na wao pia walikuwa vijana enzi zao and probably na wao walifanya kosa kama lako (sio lazima katika jambo hili), ila leo wamegundua kuwa ukweli kamwe haubadiliki kwa kubadilika kizazi ... amini kuwa wazee wana experience kubwa na wana busara kubwa zaidi yako.

Usitafute wa kukuoa, jipambe sifa za kuolewa ukiwa bado umri unaruhusu.
 
Sasa maisha hayaendi hivyo! Kwamba niolewe sasa wakati sipo tayari kwa kuhofia nikifikisha 25 naweza kukosa mtu sahihi! Sio kweli
Uko sawa kabisa na maamuzi yako usioe au kuolewa kwa presha ya watu wengine ukajikuta upo kwa mtu asie sahihi lakini pia usiseme kuwa hauko tayari kwa sasa Binafsi nimekuja kugundua Kuoa au kuolewa ni jambo gumu sana ambalo huwezi kusema kuwa nimepanga ikifika muda flani nitalifanya japo watu ambao hawajafika wakati wa kuoa au kuolewa huwa wanafikiri ni jambo rahisi ila ni kitu kigumu sana hasa zama hizi ndo maana unaona wanaume tunaogopa kuoa.

Kwako mwanamke wewe una wakati mgumu zaidi ukijichanganya ukafanya kosa 1 linakua doa kwenye jamii ndo maana nikakutahadharisha kama haupo tayari basi chunga usije ukapeleka aibu nyumbani
 
Habari!
Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'
Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja
Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.

Kwani vp?
 
Back
Top Bottom