Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Mama yako hajakosea baby sis, kikubwa atambue kuwa mke ana majukumu yake na akuandae kuwa mke bora, na walau uwe na kipato hata kama ni kidogo.

Kwa comments section; mkiendelea kuhamasishana kuoa, hamasishaneni na kuziishi hizo ndoa.

Kuna watu hawatakiwi kuwa mume/mke wa mtu yoyote duniani, ni aheri mkafahamu fungu lenu mapema kuliko kupeleka matatizo kwa watu.
 
Destine ya mtoto wa kike awe na kazi au hana kazi ni kupata mme! Stability ya binti ni mme! Utake/usitake hata kama wewe baba uko vizuri lakini ukiona binti yako yupo yupo tu ni shida! Tatizo ni kupata mme sahihi vinginevyo akiangukia kwa wavuta bangi ni shida zaidi!
Unaakili kumbe nilidhani ni waleee umeongea point na huyu dada kaongea point kazi kwanza ndoa inafuatab
 
Hata sio mabinti peke yao. Vijana ambao tunatafuta bado nao waliokurupuka kuoa wanaonja joto la jiwe. Mtu kisa kamaliza chuo wazazi hao mbiombio wanataka aoe au kuolewa. Kuna washkaji zangu Waislamu wao wazazi wanaandaa mazingira kijana akimaliza ataoa na atamtunza mke kwa hiki kibiashara. Sunna haiji na maneno matupu.

Sasa wazazi wengine wanawaza kuchangiwa kurudishiwa michango yao ya harusi na kutuzwa, aftermath utajua wewe. Binti ni gratuate anaolewa na mume kaajiriwa Posta kwenye ofisi binafsi zile zinakaba unatumia muda mwingi kazini, take home 600,000 alafu wanaishi Mbezi ndanindani huko maana ndio nyumba nzuri zina gharama nafuu.

Ukitazama spending ya wote kwenye familia kwa mwezi ni 550,000 na hapo kuna miujiza mtoto haumwi. Akiumwa tu hizo nauli za Mbezi kwenda hospitali mke na mtoto hawapandi daladala ni bajaj. Hapo ukweni hawajafiwa na hawajapata harusi.

Vicious cycle of poverty.
Una hoja ila Standard zako unaziweka juu sana, the way ume portray hio kazi ya mshawa 600,000 TZS kama kamshahara kadogo wakati ndio dream salary kwa Ground ya sasa. Yes gharama za maisha zipo juu ila tunaangalia uharisia kuna mtu ni Mlinzi anapokea 200,000 TZS Ana maisha kama hayo.

After all maisha ya sasa hakuna kitu kinaitwa kujipanga kabisa, yaani hakuna point ya hapa nimejipanga unabeti. Unaweza fifa 40 vilevile huna mbele wala nyuma.
 
Hata sio mabinti peke yao. Vijana ambao tunatafuta bado nao waliokurupuka kuoa wanaonja joto la jiwe. Mtu kisa kamaliza chuo wazazi hao mbiombio wanataka aoe au kuolewa. Kuna washkaji zangu Waislamu wao wazazi wanaandaa mazingira kijana akimaliza ataoa na atamtunza mke kwa hiki kibiashara. Sunna haiji na maneno matupu.

Sasa wazazi wengine wanawaza kuchangiwa kurudishiwa michango yao ya harusi na kutuzwa, aftermath utajua wewe. Binti ni gratuate anaolewa na mume kaajiriwa Posta kwenye ofisi binafsi zile zinakaba unatumia muda mwingi kazini, take home 600,000 alafu wanaishi Mbezi ndanindani huko maana ndio nyumba nzuri zina gharama nafuu.

Ukitazama spending ya wote kwenye familia kwa mwezi ni 550,000 na hapo kuna miujiza mtoto haumwi. Akiumwa tu hizo nauli za Mbezi kwenda hospitali mke na mtoto hawapandi daladala ni bajaj. Hapo ukweni hawajafiwa na hawajapata harusi.

Vicious cycle of poverty.
Vicious cycle of poverty
 
Habari!

Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'

Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja. Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
😅😅
 
Back
Top Bottom