kulea mtoto wa kike, hasa akivunja ungo/pale awali anapobalehe, ni kazi ngumu sana. na ni hatari, ukizembea utavuna mabua, aidha ataambukizwa ngoma umpoteze kabisa au atapata mimba, au mabonjwa mengine ya zinaa au atashindikana hata shule hata soma. binafsi niliamua, na niliwaeleza mabinti zangu kwamba, kuchapwa mtachapwa tena sana na sihitaji mnipende kama mna tabia mbaya, mtakuja kunishukuru mkiwa watu wazima baada ya kugundua nilichokuwa nakifanya kwenu. sio kwamba siwapendi, ninakaa nao, ninacheza nao, na ninawaeleza ukweli madhara ya ngono za utotoni, umuhimu wa shule kwao na wakikosea nahakikisha wamejua kuwa wamekosea na wamejutia. imefika wakati wanalindana wao kwa wao, mmoja akifanya ujinga mwezake anakuja kumsemelea kwangu. Mungu anatakiwa kuhusika.