Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Kuna shule anasoma mtoto wa jirani wanaenda had j2, afu ni private.
Najisemeaga Pesa zinatolewa ilo watoto wateseke, lol [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hivi wazazi wamekuwaje zama hizi.. Cha kusomesha watu Weekend ni nini hasa?
Tena madarasa ya mitihani ni mwaka mzima utaratibu ni uleule..
 
Kuna school, ilitaka 50elfu kwa likizo ya mwezi wa sita. Nikagoma watoto nikashinda nao home wiki zote nne nikawa nasikilizia waniulize mtoto wenyewe darasa la tatu ati mwezi wa sita asifunge aamkie shule na kurudi mchana. Huu upuuzi ulikubaliwa na walimu na wazazi mimi sikuhudhuria kikao hicho wife akaja na maazimio nikasema hiiiii!. Shida ni kuwa wazazi wengi hawajenda shule na kukosa kwao elimu wanataka watoto wao wasikose pia. Hiibinapelekea kudanganywa na waalimu kwa kupewa mipango hewa kama hii na wao wana ogopa kuhoji ili ujinga wao usidhihirike na uwoga pia umo.
 
Kuna shule anasoma mtoto wa jirani wanaenda had j2, afu ni private.
Najisemeaga Pesa zinatolewa ilo watoto wateseke, lol [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa shule za msingi kiukweli utaratibu ubadilishwe ikiwezekana waingie saa mbili watoke saa 9 masaa 6 ni mengi kwa siku kama yatatumika vizuri hawa bado wanakuwa kuwachosha sana inakuwa si vizuri aisee sasa weekend wanapata lini?
 
Si kwa shule zote mkuu mfano hizi international school m.f Tanganyika, st contstatine , braeburn na nyenginezo kama hizo wale watoto kwanza wazazi wapo vizuri halafu hata elimu ipo vizuri pia ila upo sahihi kwa kiwango kikubwa.
 
Si kwa shule zote mkuu mfano hizi international school m.f Tanganyika, st contstatine , braeburn na nyenginezo kama hizo wale watoto kwanza wazazi wapo vizuri halafu hata elimu ipo vizuri pia ila upo sahihi kwa kiwango kikubwa.
Hizo shule ulizoandika hazitoi elimu ya hapa Tanzania tofauti na shule zengine ambazo ndizo zinazungumziwa katika huu uzi.
 
Wazazi ndo mmeamua hivyo sasa kama hutaki mwanao awahi acha kumlipia school bus umpeleke hio saa mbili inayoitaka au wote mkatae huo mda wa watoto kuchukuliwa saa kumi .....
 
Duh.. mkuu, hii inatisha..wazazi wengine wanasemaje?
Kwenye magroup ya madarasa pia wanatia pin admins tu ndiyo wacomment.. mi nna imani wazazi wengi hawaridhishwi na hiyo hali..
 
Hiyo ratiba unaona ni sawa kwa mtoto wako?
 
Usomaji usio na tija wala manufaa kwa taifa we mtoto aamke saa 10 usiku arudi saa 12 mpaka saa 1 usiku naapo bado ana home workers zinamtolea macho rikizo yenyewe hana anacho kisoma shule akija kuki aplay mtaani hakifanyi kazi apo ndipo mkoloni alituweza ifikie mahala wazazi tuamke kutoka usingizini🥶
 
Wazazi wanata kuwa free, watoto ni mzigo kwao
 
Wazazi wanachangia hili. Siku wakiamua linaisha.
Wataamuaje wakati wazazi wenyewe ni watumwa? Wanachofanya ni kutengeneza watoto watumwa. Hicho kitu wanapambana watoto wakifuate shule kipo hata kwenye simu zao.
Ifike muda serikali yetu ijitambue. Lakini nachelea kuamini kuwa hamna serikali tuliyonayo au itakayokuja yenye kujitambua kwenye hili
 
Sasa wakuu haya mambo mnayosema hapa si tayari serikali wkt wa msoga ilishatakaga kuingilia kati na kuyakomesha mkawajia juu kuwa yapo private skuls ambako serikali haihusiki na wengine mkaenda mbali zaidi kudai serikali ifanye ivo kwa shule zake tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…