Lupamba's grandson
JF-Expert Member
- Jan 9, 2015
- 1,232
- 1,196
Wazazi na walezi,
Tembelea watoto wako wanaosoma vyuo!
Hasa hawa walioenda ngazi ya cheti baada ya kumaliza kidato cha nne, wengine wameoa na kuolewa!
Binti haingii darasani, anafua na kupika kwa kijana waliyekutana naye chuoni.
Kuna ambao pesa ya ada hajalipa anahudumia "mke"! Unaweza fikiri yupo masomoni kumbe analea mke na mtoto.
Kuna ambao wamefukuzwa vyuo au kuacha masomo kwasababu mbalimbali, mzazi usipofuatilia hautajua.
Wengi wanaoenda vyuo vya kati au vyuo vikuu baada ya kidato cha nne wana umri mdogo sana, hawajafundishwa namna ya kutumia "uhuru" wa chuo, huko hakuna mwalimu wa darasa au mwalimu wa nidhamu. Haulizwi kwanini hajaingia darasani, au hajafanya mtihani, ni matokeo ya mwisho yatakayoamua.
Sasa mzazi usipoyajua haya unaweza kushangazwa na hayo matokeo ya mwisho, na inaweza kuwa tayari umeshachelewa.
Siku hizi wahitimu wengi wa kidato cha nne hawataki kwenda kidato cha tano, wanataka kwenda vyuo, ukiacha sababu ya kutaka kupata ujuzi na ajira kwa haraka, wengi wanataka kuwa huru. Wanasema vyuoni hakuna mambo ya kuvaa sare wala kupangiwa vitu vya kufanya, na kingine wanafurahia pesa ya matumizi anayopewa chuo ni kubwa kuliko akienda sekondari.
Sasa huu uhuru na pesa ya matumizi ukivichanganya na usipokuwa na akili njema, kuna kitu kinaitwa "majuto ni mjukuu"!
MZAZI TIMIZA WAJIBU WAKO!
Mwl.Doris Mboma!