Wazazi msipowafuatilia watoto wenu chuo mtajutia mwishoni

Wazazi msipowafuatilia watoto wenu chuo mtajutia mwishoni

Miaka 18 ni mtu mzima wacha wajifunze maisha, kadri wanavyofanya makosa katika umri mdogo ndivyo wanavyopata experience ya maisha. Kila mtu anaweza kuharibikiwa ajirishi umri wake.
Kama ni mtu mzima basi ajitafutie na ada ajilipie huko chuoni sio mm nishinde juani na niuze vitu vyangu vya thamani kama ardhi na mifugo ili aende akasome alafu yy anaenda kufanya upuuzi kisa eti anesha vuka miaka 18 alafu na bado akisha feli anakuja kunidai urthi.
 
Serikali pia iangalie. Siku hizi kuna mtoto wa miaka 11 anamaliza la saba. Mtoto huyu akifisha miaka 15 kamaliza form four tayari kapangwa chuo. Huu ndio muda wa balehe.

Je mtoto wa miaka 15 anaweza kujisimamia? Bado ni mchanga mno. Atleast akipita form six atafika huko yupo 18. Tuangalie wakati wa kupanga watoto.
 
1.waliowengi hela ya matumizi haiwatoshi

2.kufuata mkimbo kua flani anafanya hivi nami nawafuata tuwe sawa.

3.utoto. ..hapa ndio unahitajika usimamizi wa kijana kwa hali ya juu.

4.malezi wanayokulia siku hizi kijana anajilinda mwenyewe wazazi wapo busy kutafuta hela. ..vijana wakazi ndio wamegeuzwa wazazi
 
Kama ni mtu mzima basi ajitafutie na ada ajilipie huko chuoni sio mm nishinde juani na niuze vitu vyangu vya thamani kama ardhi na mifugo ili aende akasome alafu yy anaenda kufanya upuuzi kisa eti anesha vuka miaka 18 alafu na bado akisha feli anakuja kunidai urthi.
Hao wakubwa wa bachelor wanajilipia? ada
 
Huko chuoni wengi wanaishi kama mke na mume wakimaliza pale hawaoani tena.

Sasa binti anaenda kutafuta mwanaume mwingine ili apate kuolewa.

Huyu akiolewa unafikiri hiyo ndoa itakua ya heri? Kutakua na utulivu na uaminifu kwa hiyo ndoa kweli, hiyo ndoa itakua na maadili mema kweli?

Hapo lazima malalamiko ya ndoa kuwa mengi hamna namna sababu hawa wameshaharibika kuanzia huko mashuleni na vyuoni.
 
Hao wakubwa wa bachelor wanajilipia? ada
Hata kama ungekuwa na miaka 40 ilimaradi unanitegemea huna Uhuru kwangu mtu mwenye maamuzi na maisha yake ni yule anaye jitegemea.
 
Ukoloni huo
Demokrasia ipo kwa ajili ya watu wenye akili na si kwa ajili ya wapumbavu.

Bila ukoloni waafrika mpaka sasa tungekuwa tunaishi maisha ya ajabu sana haka kaangalau tulio nako kameletwa na ukoloni.
 
Uliyosema ni kweli kabisa hasa hivi vyuo vikuu vinavyotoa kuanzia certificate, diploma hadi degree. Unakuta mtoto wa kike umri miaka 18 anasoma certificate analipiwa ada na wazazi hapo hapo kuna kijana anasoma bachelor degree na anapata boom
 
Uko sahihi mkuu, nina mfano wa hili jambo.......watoto wa zama hizi wana mawenge sana, wanakurupukia hatua za kimaisha kabla ya muda. Muda ambao wanatakiwa kuwajibika kwenye masomo yao hapo hapo wanataka wawe wabobezi wa vilevi, mambo ya mapenzi na anasa nyinginezo........yaani ni kizazi kinachoelekea kwenye uangamivu kwa spidi zilezile za mtandao 3G, 4G, 5G......​
 
Back
Top Bottom