Mm nadhani wazazi hawana uwezo wa kubadilisha lolote hasa walio mbali na vyuo, mfano mtu uko singida na mtoto wako anasomea chuo Dar hata ufanyeje huna uwezo wa kumdhibiti.
Mwenye uwezo wa kukomesha huu upuuzi ni serikali kwa kufuta huu upuuzi unao itwa uhuru ulio pitiliza vyuoni ,kwa sababu wenye busara walisha sema ya kuwa demokrasia ipo kwa ajili ya watu wenye akili na si kwa ajili ya wapumbavu.
Taasisi ya elimu ya juu ni taasisi nyeti sana ndani ya nchi ambayo inaandaa watu watakao amuwa msitakabili wa nchi lakini cha kushangaza serikali ni kama imefumba macho utadhani haioni kinacho endelea alafu kesho tukipata viongozi na watumishi wa hovyo tuanze kulalamika.
Tatizo waafrika tuna razimisha kuishi wa kufuata demokrasia ya kamagharibi hali ya kuwa sisi ni watu wawili tofauti kabisa, kuanzia upeo wa kiakili na mfumo wetu wa maisha
Mfano binti wa kijerumani mwenye umri wa 16 tiyari anakuwa amesha jiwekea malengo ya anahitaji kuwa nani na atafanya nn pale atapo maliza masomo, wakati binti wa kiafrika mwenye miaka 25 anacho waza ni kumiliki iPhone ili awalingishie mashoga zake na jinsi ya kuwapanga mabwana zake 10 anao tembea nao wasijuane, sasa watu wa namna hii huwezi ukawaongoza kwa mtindo mmoja ni lazima ufeli tu.
Huu upuuzi unao itwa uhuru vyuoni ukienda nchi nyingi za Asia na mashariki ya kati haupo na ndio maana wanazalisha wasomi wa maana wenye msaada kwa mataifa yao wakati huku Africa wanao jiita wasomi wamegeuka mizigo ndani ya matifa yao.