Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Ila hii nchi inamambo mengi sana aisee, kila siku tunaharibu kizazi chetu tena kwa mikono yetu. Vijana wengi wanafanya mambo ya ajabu na tunatazama tu bila kusemea wala kukemea huku tukisubiri yatokee madhara tuanze kulaumu vyombo vya usalama na mamlaka zingine.
Ijumaa nilitoka kazini mapema nikajisemea nipite mjini mara moja nikaulizie bei ya bidhaa zangu za nyumbani, tukiwa kwenye gari ghafla lilipita basi moja lilikiwa na mziki mmoja mkubwa sana, na mbaya zaidi watoto wa kike ambao walikuwa ni wadogo wenye umri kati ya miaka 18 hivi walikuwa wakicheza nusu uchi tena kwenye madirisha ya gari hiyo. Niliumia sana kuona kila siku tunarudi nyuma kimaadili ilihali asili ya mtanzania ni nidhamu na maadili.
Jana usiku nilikutana na poster mtandaoni ikitangaza kuwa kuna House Party huko Arusha, na kwenye poster hiyo ilidai kuwa kiingilio ni bure na kutakuwa na kila kitu kwa maana huduma zote. Pombe za kila aina, chakula, sigara na bangi. Pia walieleza kuwa kutakuwa na swimming pool (Bwawa la kuogelea) ambao watu wataweza kuogelea wakiwa uchi.
Leo nimekutana na hii asubuhi hii, wajuzi wa haya mambo ya bata ebu mnieleweshe hii free sex nikwamba unajilia yeyote tu ndani humo au inakuaje?? Mbona haya ni mapya kwenye masikio yangu? Je usalama wa afya za watu upoje? Maswali ni mengi sana.
Kwa hakika Mheshimiwa Dorothy Gwajima una kazi kubwa sana Mama yangu, pole sana. Wazazi, walezi na watanzania tumsaidie huyu mama sio kila tukio likitokea tumpelekee, ilihali tunakuwa tunakutana na viashiria vya hatari mapema.
Balehe inavuruga sana vichwa vya vijana wengi, na sisi kama jamii tuna kila sababu ya kuwaelekeza vijana wetu katika namna bora yenye maadili. Kwa mtindo huu kufika 2030 maambukizi ya virusi vya UKIMWI yatakuwa juu kwa sababu ambazo tunaweza kuziepuka.
Sina nia yoyote mbaya ya kuharibu biashara za watu, kumbi za starehe wala sehemu za kufanyia shughuli, ila tumsaidie huyu mama. Kazi yake inakuwa nzito haswa tunapokuwa tunapuuzia haya mambo, HOUSE PARTY ina watoto U18 na unaona kabsa kuna kiashiria cha hatari, tusaidiane watanzania.