Wazazi tusomeshe watoto waje kujiajiri kwa taaluma walizosomea au kuajiriwa, biashara kwa hapa Tanzania zataka moyo

Wazazi tusomeshe watoto waje kujiajiri kwa taaluma walizosomea au kuajiriwa, biashara kwa hapa Tanzania zataka moyo

Tanzania kuna makazi zaidi ya 12mil
Wafanyakazi Tanzania ni chini ya 1mil
 
Biashala inahitaji kujitoa kingine usione watu wanafanikiwa kwenye biashala kuna vitu vingi Sana ikiwemo kujinyima nakumbuka Mimi nilikuwa nashindia mkate na maji lakini Leo hii nishavuka kutoka kuwa na genge la nyanya mpka kumiliki Mali ambazo inabaki kuwa Siri yangu lakini yote kwa yote biashala ina Siri unaweza kujinyima na usifanikiwe.
 
Upo sahihi mkuu,unakuta unafanya kazi una tasks kibao hata muda wa lunch we una skip lunch,jion wenzio wanatoka saa 11 we unatoka saa 1 jion….kupata kazi ni kazi ila kumantain nafasi yako ni kazi sana
Kabisa mzee kuna kazi zinakubana.
 
Elon musk analala ofisin 😀
Huyu hasaki utajiri yeye ana passion ya kuacha alama Dunia. Vision yake tu inamtoa mtu kama isac newton ambayr anasahau jina lake mwenyewe.

Mm na wewe tukiwa na biashara ilitoajiri vijana kati ya 10-25 na bajeti ya uendeshaji kwa mwaka ikagota 3B tayar tunaishi maisha ya ndoto zetu. Regardless tuna passion au hatuna katika kile tunafanya. Wew unawez kulala ofisin sababu ya kufunga hesabu au kureview muenendo wa ofisi yako Tu. Kwa vision na level hii huwez kuniambia Kuna nasaba ya ufanano wa sabab kati yako na elon musk
 
Biashara sio kwa ajili ya wazembe na waoga ndo maana wapo wachache. Unavyosema kwamba watu waajiriwe tambua kwamba kampuni binafsi zilikuwa ni mawazo ya majasiri walioweka uvivu na uoga pembeni hadi wakafanikiwa. Hao waajiriwa unaona wanakula bata wengi wao ni mafisadi na wabadhirifu sana. Ni ngumu kuishi high life kwa mishahara ya kibongo.
 
Back
Top Bottom