Wazazi vaeni viatu vya wazazi wenzenu, inaumiza sana

Wazazi vaeni viatu vya wazazi wenzenu, inaumiza sana

Magidu

Member
Joined
Oct 18, 2022
Posts
52
Reaction score
86
Nawasalimu nyote,

Jana ni siku ambayo sitaisahau kutokana na story yakusikitisha niliyosimuliwa na binti wa miaka18. Binti huyu ni mwanafunzi wa mwaka wakwanza katika moja kati ya vyuo vikuu maarufu hapa nchini. Aliripoti chuoni Mwezi October Mwaka jana akionekana mtoto mtulivu na mwenye heshima zake.

Kama mjuavyo, vyuoni kuna mchanganyiko wa wanafunzi waliotoka sekondari moja kwa moja na wale ambao wametoka makazini waliokuja kwa lengo lakujiendeleza(In-service).

Sasa kumbe haka kabinti kalikutana na mwanaume mtu mzima(in-service) ambaye alikarubuni wakapanga chumba na kuishi pamoja kama mtu na mwenza wake.Kwa maelezo yabinti nikwamba huyu mwanaume ana zaidi ya miaka48.

Baada ya likizo fupi ya kumaliza semester ya kwanza, wapenzi hawa walitawanyika kila mmoja akienda nyumbani, binti alirudi kwa wazazi huku mwanaume akienda kwa mke nawatoto wake.

Shida imeanza baada ya likizo ambapo binti alitangulia kurudi huku jamaa akiahidi kurudi siku za mbeleni kidogo. Muda umeenda jamaa harudi huku binti akiishi maisha yashida kwani alikuwa anamtegemea yule mwanaume kwa kila kitu ikiwemo kodi ya chumba.

Jana nimemkuta mahali analia anadai baada yakuona anaumwa mara kwa mara ilibidi aende hospital ambapo amekutwa na magonjwa ya ngono ikiwemo VVU/UKIMWI.

Taarifa zauhakika kutoka kwa wanaomfahamu huyo mzee nikwamba ni mgonjwa wa miaka mingi na kutokana na sababu zakifamilia amesitisha masomo hatarudi tena chuoni.

Kilichoniuma binafsi nikwamba naamini mzee kama huyu hakosi binti wa umri kama huyo aliyemharibia kesho yake kwa makusudi. Alishindwaje kuvaa viatu vya mzazi mwenzake ambaye alitumaini kuwa elimu anayompa binti yake itaenda kumfaidisha siku zijazo? Ni vipi angejisikia endapo binti yake angefanyiwa unyama kama huo na mzee mwenzake?

Mwisho; Watoto wa kike mkienda vyuoni kumbukeni yale maneno mnaoambiwa na wazazi/walezi wenu.
 
Nawasalimu nyote,
Jana ni siku ambayo sitaisahau kutokana na story yakusikitisha niliyosimuliwa na binti wa miaka18. Binti huyu ni mwanafunzi wa mwaka wakwanza katika moja kati ya vyuo vikuu maarufu hapa nchini. Aliripoti chuoni Mwezi October
Washauri hao mabinti wapunguze tamaa
 
Kabla ya kutaka kuonewa na huruma na mtu baki jionee huruma wewe mwenyewe,binti wa miaka 18 na mzee wa miaka 50 inaingia akilini?
Wakukuonea huruma ni mama yako na si mwingine,jukumu la kujitunza lipo mikononi mwako either abstain ama be careful

Pole binti kwa kupenda vya bure

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Pole
 
watu wanasema wanafunzi hawajielewi.....hawajui mabinti wanapitia shida gani hasa za kiuchumi.

kama unatumia Linda afya yake akimaliza shule aendelee na maisha yake.
Hapa kwenye uchumi ndio tatizo,kuna mahitaji mengi anayohitaji,kuna vyuo binafsi,kama vya Afya,vinaagiza Rim(karatasi za mitihani)karibia tatu,kila moja 20000,wanaagiza gloves box 3 au zaidi,kila moja karibia 35000,Taulo karibia tatu,na bado yeye mwenywe ana matumizi ya ziada,sabuni,dawa ya msuaki,ped,nk,atapata wapi vyote hivyo,na wazazi ni maskini.
Ndio akikutana na mtu wa kumdanganya,kumsaidia,ana muamini.
Vyote hivyo vinatakiwa kila mwaka.
 
Huu ni mtihani sasa na unyama wa hali ya juu sana ww mtoto km huyo unamuambikiza kabisa ili iweje ila hivi vitoto vinatamaa sana 18 years bado kabisa akili haijakomaa.

Mimi nilizuia mtoto wa Sister asiende mbali kusoma chuo asome hapahapa Dar ana 19 years hata kama anakaa hostel week end anarudi una msihi mtoto kuhusu maisha na maradhi yazinaa atleast kuna unafuu. Huyo jamaa alaaniwe
 
Back
Top Bottom