Wazazi wa kisasa ni changamoto kubwa sana kwenye malezi

Wazazi wa kisasa ni changamoto kubwa sana kwenye malezi

Joined
Feb 23, 2021
Posts
19
Reaction score
33
Nimekuja kibiashara hapa mjini kahama nikaona si mbaya nifikie kwa jamaa yangu ambaye tunatoka sehemu mmoja anaishi na familia yake hapa hatimaye nimefika amenipokea vizuri nashkuru ukweli yuko vizuri hongera zake mambo si haba kapanga apartiment nzima anausafiri istoshe ni mwajiriwa wa kampuni mojawapo hapa mjini
mke kamfungulia biashara ya Min Supermarket kwa hiyo si Mama wa kushinda nyumbani na wamebarikiwa Mtoto mmoja wa kiume.

Sasa hapo ndo kwenye shida hapa nyumbani wana Dada wa kazi wanaishi naye huyu Mtoto sasa nitabu kwakweli siku nimefika tu alikuapo Mama mtoto litoto acha lin'gan'ganie kiti nilicho pewa nikalilie. Eti kiti changu toka toka nakulialia hovyo kiufupi toto limeishi kudekezwa sana yani balaa tupu mpaka kanipa kiti kingine nikalie et yani huyu Mtoto shem hebu njoo ukae hapa.

Nilishwangazwa sana kiukweli nilijiskia hasira sana, humo ndani sasa wawepo wasiwepo ni mwendo wa kuangalia midoli nakatuni kwenye TV ole wako utoe litakavyo bweka na Wazazi wanaenjoy tu asubui mpaka jioni tunaangalia katuni tu kiufupi toto lina lelewa kama yai.

Nimechukizwa sana na hii hali mara nyingine sitamani tena kufikia hapa nilitaka kuwashauli nikajiongeza tu hapa hamna la maana Wazazi wenyewe wamekaa kisasa sana.
wanaishi kama wazungu.

Kwenu wana Jamvi
 
Duh Pele sana mkuu si ungekafinya mbavu kasinge Rudi tena
 
Haya ni makosa tunayoyafanya wazazi,mwisho wa siku mtoto akiendelea na malezi haya,itamghalimu ukubwani,maana akiwa na wenzake atataka afanye anavyotaka,sasa akikumbana na upinzani kwa wengine ataona kama anaonewa ndo maana wahenga walisema; Samaki mkunje angali mbichi, akishanyauka hakunjiki!
 
Haya ni makosa tunayoyafanya wazazi,mwisho wa siku mtoto akiendelea na malezi haya,itamghalimu ukubwani,maana akiwa na wenzake atataka afanye anavyotaka,sasa akikumbana na upinzani kwa wengine ataona kama anaonewa ndo maana wahenga walisema;Samaki mkunje angali mbichi,akisha nyauka Hakunjiki!
Hakika
 
Mkuu mimi nipo kwa mjomba wangu hapa Chattle wiki ya tatu hii naangalia Nickelodeon na Cartoon network natamani nipate hata dakika 10 niangalie ITV labda ntakuta Tundu lissu anahutubia lakini JUNIOR kashikilia remote
Mama....wewe juniaaaa hebu mpe baba mdogo rimoti aangalie taarifa ya habari.
Junior.....chitakii chitakii rimoti ya kwanguuu.
Baba....Bwahahaha...junior bwana akishaanza vituko vyake humwambii kitu.
 
Mama....wewe juniaaaa hebu mpe baba mdogo rimoti aangalie taarifa ya habari.
Junior.....chitakii chitakii rimoti ya kwanguuu.
Baba....Bwahahaha...junior bwana akishaanza vituko vyake humwambii kitu.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duniani kuna mambo na changamoto nyingi ambazo huwezi kuzitatua.

Hivyo simple solution ni kuachana nazo alafu unamind your business.
Au Itakuwa hakuna tofauti na wale wakaa barazani.

No offense just a bitter truth.
 
Back
Top Bottom