Wazazi wa kiume malezi mnayowapa vijana wenu wa kike mtavuna mnachokitafuta

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Nimeona wababa wengi wa kisasa hasa hawa wenye vipato vya kubadilisha mboga aka middle-class wanawadekeza sana vijana wao wa kike (mabinti).

Sasa nachowaambia endeleeni ivoivo majibu mtayapata bdae.

Inajulikana, kiasili kijana wa kike anaenda sawa na baba kwa sababu ni ngumu au kuna uzito fulani kwa baba kumuadhibu kijana wake wa kike. Hii inasababisha kijana anakuwa upande wa baba zaidi, maana anajua kwa mama kwa moto.

Sasa mara nyingi wababa wanaingia kwenye huu mtego kwa kuwapa malezi ya "kimayaimayai" mabinti zao.

Sasa nipo hapa kuwahakikishia wababa, mnatengeneza mabomu ya bdae kwa malezi haya namna hii.

Kumbuka hapo unamtengeneza mke wa mtu wa hapo bdae.

Unamtengeneza mazahausi wa hapo bdae.

Unamtengeneza mama mkwe wa mtu wa hapo bdae.

Unamtengeneza wifi wa mtu wa hapo bdae.

Binti sio wa kudekezwa, tena kwa mimi unatakiwa kumkazia binti zaidi pengine kuliko hata dogo wa kiume maana kwa jamii zetu hizi ni hatari sana kuwa na mwanamke nyoronyoro.

Kama binti kaharibu apewe adhabu kama ambavyo ungempa kijana wako wa kiume na ikiwezekana msogeze zaidi awe kwa mamake wawekane sawa wenyewe huko.
 
Taa mfano wa hayo malezi ya mayai mayai Mara nyingi mambo ya msingi mtoto wa kike anafundishwa na mama, usafi,mapishi,mavazi haijawahi kutokea mama anampa ripoti baba Kama mwanao anamwendendo fulani mbaya halafu baba amchekee lazima alambwe fimbo,
Hii dhana imeea Sana Kama watoto wa kishua ni mayai mayai Mimi nasema si kweli malezi yanategemea na mzazi Tena angalau wakishua ni geti Kali kuliko wa uswahili wanazurura kutwa Kama kuku wa kienyej risk kabao.
 
Nimeona wababa wengi wa kisasa hasa hawa wenye vipato vya kubadilisha mboga aka middle-class wanawadekeza sana vijana wao wa kike (mabinti).

Sasa nachowaambia endeleeni ivoivo majibu mtayapata bdae.

Inajulikana, kiasili kijana wa kike anaenda sawa na baba kwa sababu ni ngumu au kuna uzito fulani kwa baba kumuadhibu kijana wake wa kike. Hii inasababisha kijana anakuwa upande wa baba zaidi, maana anajua kwa mama kwa moto.

Sasa mara nyingi wababa wanaingia kwenye huu mtego kwa kuwapa malezi ya "kimayaimayai" mabinti zao.

Sasa nipo hapa kuwahakikishia wababa, mnatengeneza mabomu ya bdae kwa malezi haya namna hii.

Kumbuka hapo unamtengeneza mke wa mtu wa hapo bdae.

Unamtengeneza mazahausi wa hapo bdae.

Unamtengeneza mama mkwe wa mtu wa hapo bdae.

Unamtengeneza wifi wa mtu wa hapo bdae.

Binti sio wa kudekezwa, tena kwa mimi unatakiwa kumkazia binti zaidi pengine kuliko hata dogo wa kiume maana kwa jamii zetu hizi ni hatari sana kuwa na mwanamke nyoronyoro.

Kama binti kaharibu apewe adhabu kama ambavyo ungempa kijana wako wa kiume na ikiwezekana msogeze zaidi awe kwa mamake wawekane sawa wenyewe huko.
Aah wapi, wewe hupendi wanawake in general tu! Daddy’s girl sio jambo baya at all, infact ushasema mama yake atamnyoosha sasa na wewe ukikaza si inakua jehanamu hio!For instance ( it’s always a bad look when baba anachapa mtoto wa kike ewww) unamuandalia mazingira ya kuonewa na men later in life na yeye ataona sawa tu….
 
Kuwa "daddy's girl" ni sawa lakini kuwa "momma's boy" mnasema sio sawa, mnavuta upande wenu tu.

Mzazi hatakiwi kuogopwa, awe mama au baba, ila ni lazima akemee upuuzi akiuona.

Hii kukariri kwamba mtoto wa kiume ni wa mama, wa kike ni wa baba, sio vizuri.
 
Nakubaliana na hoja kwenye suala la usawa wa malezi. Leeni watoto wa kike na kiume kwa upendo ili wakikua wajue upendo unafananaje waweze kumudu kuuonyesha pia. Malezi siyo nidhamu peke yake, ni pamoja na kumkuza mtoto kihisia na kiakili.

Mbali na hayo majukumu ya kifamilia, hao watoto wa kike watakuja kuwa wafanyakazi, wafanya biashara, viongozi n.k. Ni muhimu wakuzwe na kuandaliwa kwenye hayo pia.
 
Well said
 
Back
Top Bottom