Wazazi wa siku hizi wamewafanya watoto kuwa watumwa wa elimu

Wazazi wa siku hizi wamewafanya watoto kuwa watumwa wa elimu

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Elimu ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu lakini hutakiwi kuwa mtumwa elimu kwa sababu kuna maisha nje ya elimu.

Wazazi wa siku hizi sijui ni ujinga au ni ulimbukeni yaani unaamka 12:00 asubuhi kwenda kwenye mishe zako unakutana na rundo la watoto wa miaka 5,4,3 wakiwa wanasuburi daladala wengine kwenye bodaboda eti wanawahi shule asubuhi penyewe kunakuwa na baridi kali.

Hivi nyinyi wazazi mmeshindwa kuzishinikiza uongozi wa hizo shule zenu wakabadilisha muda wa kilipoti shule angalau ikawa 2:30 kwa hivi vitoto vidogo vya kindagat?

Yaani mzazi una akili timamu una muamusha mtoto wako wa miaka 3,4,5 uliye mzaa kwa uchungu usiku wa baridi kali eti unampeleka shule kweli? Kwanza mtoto wa miaka miaka 3 unampeleka shuleni akasome nini zaidi ya kuchocha ubongo wake tu?

Leo nimeamka mapema sana kwenda kwenye mishe nimekutana na kisa kimoja ndo kimenifanya niandike mada hii.

Nimekutana na watoto 3 nadhani ni watoto wa familia Moja kwa sababu walikuwa wanafanana walikuwa na binti nadhani ni binti wa kazi alikuwa anawasindikiza shuleni, mmoja alikuwa mkubwa kidogo kwa kumkadilia ana wasitani wa miaka 7 wa pili kwa kumkadilia ni miaka 5 sasa haka ka 3 ndo nimekaonea huruma kweli kalikuwa kadogo sana nadhani hata miaka 3 kalikuwa hakajakamilisha vizuri kalikuwa ka kike.

Sasa wenzake wakawa anatembea haraka wana kaacha nyuma kale kadogo kakawa kanalia, sasa nikamuuliza yule binti aliye kuwa nao kuwa kwanini usimbebe huyo mtoto huoni kwa kwamba ni mdogo hawezi kutembea kama wenzake? Akanijibu kuwa kama wazazi wake walijua ni Mtoto kwanini walimpeleka shule acha apambane aisee nilijisikia vibaya na kumuonea huruma yule mtoto.

Kuna wale wazazi wengine hawawapi nafasi watoto wao kufanya mambo mengine nje ya kusoma, unakuta mtoto anatoka shule, anamaliza kula anaenda tuition akirudi tuition bado usiku ana rundo la homework, mambo yanaendelea hivyo mpaka wakifunga shule ,wakisha funga shule ana mlipia tuition yaani mtoto hana muda wa kupumzika na kufanya na kujifunza mambo mengine nje ya kusoma.

Yaani mzazi anamjengea mtoto fikra kichwani kuwa hakuna maisha mengine nje ya kusoma hapa duniani alafu huyo mtoto akisha hitimu hiyo elimu aliyo muaminisha ndo kila kitu, akikosa ajira anaanza kumfukuza mtoto nyumbani eti aende apambane akatafute maisha,hivi aende atafute maisha yapi ambayo ww huhawahi kumfundisha?

Utamuambiaje mtoto ambaye ulimuaminisha kuwa kusoma ndo kila kitu eti ashike jembe akalime?
Utamuambije mtoto akawe, boda boda, asukume tolori, asaidie fundi, atembeze matunda,apike chips hali yakuwa umemkuza katika fikra za kuamini kuwa hizo ni kazi za wasio na elimu?

Mzazi hakikisha unamlea mtoto katika maisha ambayo una uhakika na uwezo wa kumpatia hata pale atakapo mkubwa , sio mtoto unalea kama sungura alafu unataka akikuwa aishi kama simba au chui.
 
Hii ndio inaonyesha tatizo kubwa zaidi linalotukabili...elimu ilitakiwa iwe sehemu ya maisha visiwe vitu viwili tofauti...elimu ilitakiwa itukomboe na itumike katika maisha yetu ya kila siku ....hii iliyopo sasa hivi inatakiwa ipewe jina lingine sio elimu
100% Fact. Ndio maana Kila siku nasema elimu hii ya mtaala wa Necta haistahili kulipiwa kwa sababu haina inacho kitoa ndani ya mwanafunzi na kukileta nje kwenye uhalisia. Naambiwaga nitafute hela eti sina hela🤣🤣🤣🤣
 
Binafsi kwa jinsi elimu yetu ilivyo,mwanangu ataanza rasmi kwenda shule akifikisha miaka 6~7,kabla ya hapo tutakuwa nae nyumbani tukimfundisha vitu mbali mbali kuhusu maisha
Mambo yababadilika ndgu, miaka 7 ni mkubwa huyo afaa kua darasa la 3 kwa miaka hii.

Wewe ndo utafanya mwanao azeekee shule.
Mpeleke shule za karibu acheze na watoto wenzie, mbona shule zetu za st.kayumba watoto hao wadogo wanaenda saa moja na saa tano au sita kesharudi
 
Wewe una mtoto/watoto ? Je unawaleaje hasa linapokuja swala la shule?

Issue za masjid weka pembeni.
Bila shaka na ww utakuwa unafanya huo ujinga ndo maana umeacha kujadili mada iliyoko mezani ww unaleta mambo ya masijdi hii mada ina uhusiano gani na masjidi zaidi ya kutaka kuanzisha marumbano ya kipuuzi?

Mm nina mtoto 1 ana miaka 3 lakini siwezi mpeleka kumuanzisha shule nitasubiri ubongo wake ukomae ndo nitampeleka ,walio sema mtoto mtoto anatakiwa kuanza shule akiwa angalau na miaka 6.
 
Back
Top Bottom