Wazazi wa siku hizi wamewafanya watoto kuwa watumwa wa elimu

Wazazi wa siku hizi wamewafanya watoto kuwa watumwa wa elimu

Elimu ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu lakini hutakiwi kuwa mtumwa elimu kwa sababu kuna maisha nje ya elimu.

Wazazi wa siku hizi sijui ni ujinga au ni ulimbukeni yaani unaamka 12:00 asubuhi kwenda kwenye mishe zako unakutana na rundo la watoto wa miaka 5,4,3 wakiwa wanasuburi daladala wengine kwenye bodaboda eti wanawahi shule asubuhi penyewe kunakuwa na baridi kali.

Hivi nyinyi wazazi mmeshindwa kuzishinikiza uongozi wa hizo shule zenu wakabadilisha muda wa kilipoti shule angalau ikawa 2:30 kwa hivi vitoto vidogo vya kindagat?

Yaani mzazi una akili timamu una muamusha mtoto wako wa miaka 3,4,5 uliye mzaa kwa uchungu usiku wa baridi kali eti unampeleka shule kweli? Kwanza mtoto wa miaka miaka 3 unampeleka shuleni akasome nini zaidi ya kuchocha ubongo wake tu?

Leo nimeamka mapema sana kwenda kwenye mishe nimekutana na kisa kimoja ndo kimenifanya niandike mada hii.

Nimekutana na watoto 3 nadhani ni watoto wa familia Moja kwa sababu walikuwa wanafanana walikuwa na binti nadhani ni binti wa kazi alikuwa anawasindikiza shuleni, mmoja alikuwa mkubwa kidogo kwa kumkadilia ana wasitani wa miaka 7 wa pili kwa kumkadilia ni miaka 5 sasa haka ka 3 ndo nimekaonea huruma kweli kalikuwa kadogo sana nadhani hata miaka 3 kalikuwa hakajakamilisha vizuri kalikuwa ka kike.

Sasa wenzake wakawa anatembea haraka wana kaacha nyuma kale kadogo kakawa kanalia, sasa nikamuuliza yule binti aliye kuwa nao kuwa kwanini usimbebe huyo mtoto huoni kwa kwamba ni mdogo hawezi kutembea kama wenzake? Akanijibu kuwa kama wazazi wake walijua ni Mtoto kwanini walimpeleka shule acha apambane aisee nilijisikia vibaya na kumuonea huruma yule mtoto.

Kuna wale wazazi wengine hawawapi nafasi watoto wao kufanya mambo mengine nje ya kusoma, unakuta mtoto anatoka shule, anamaliza kula anaenda tuition akirudi tuition bado usiku ana rundo la homework, mambo yanaendelea hivyo mpaka wakifunga shule ,wakisha funga shule ana mlipia tuition yaani mtoto hana muda wa kupumzika na kufanya na kujifunza mambo mengine nje ya kusoma.

Yaani mzazi anamjengea mtoto fikra kichwani kuwa hakuna maisha mengine nje ya kusoma hapa duniani alafu huyo mtoto akisha hitimu hiyo elimu aliyo muaminisha ndo kila kitu, akikosa ajira anaanza kumfukuza mtoto nyumbani eti aende apambane akatafute maisha,hivi aende atafute maisha yapi ambayo ww huhawahi kumfundisha?

Utamuambiaje mtoto ambaye ulimuaminisha kuwa kusoma ndo kila kitu eti ashike jembe akalime?
Utamuambije mtoto akawe, boda boda, asukume tolori, asaidie fundi, atembeze matunda,apike chips hali yakuwa umemkuza katika fikra za kuamini kuwa hizo ni kazi za wasio na elimu?

Mzazi hakikisha unamlea mtoto katika maisha ambayo una uhakika na uwezo wa kumpatia hata pale atakapo mkubwa , sio mtoto unalea kama sungura alafu unataka akikuwa aishi kama simba au chui.
Punguzeni kuzaa hovyo haya yote hayawezi kuyapata, African hasa watanzania wanaishi life style mbovu sana.
 
Wazazi wa aina hio wengi walikuw vilaza. Wameungaunga sana hadi kupata kielimu kwahio hawataki watoto wao wawe kama wao matokeo ya yake wanaishia kuwatesa.
Mkuu ni kweli ni ukosefu wa akili.
 
Bila shaka na ww utakuwa unafanya huo ujinga ndo maana umeacha kujadili mada iliyoko mezani ww unaleta mambo ya masijdi hii mada ina uhusiano gani na masjidi zaidi ya kutaka kuanzisha marumbano ya kipuuzi?

Mm nina mtoto 1 ana miaka 3 lakini siwezi mpeleka kumuanzisha shule nitasubiri ubongo wake ukomae ndo nitampeleka ,walio sema mtoto mtoto anatakiwa kuanza shule akiwa angalau na miaka 6.
Ila wakati unasubir ubongo wake ukomae unamuanzisha masjid kwanza au sio?

Mimi wangu ana miaka mi5 Yuko KG2 namuamsha saa 12:45 asbhi na shule anaenda saa 1:30 na mara nyingi hapo mtaani yeye ndio mtoto wa mwisho siku zote kwenda shule na hapo anaposoma ni umbali wa dk 5 tu.
 
Nashangazwa sana na kuhesabu namba, mtoto anawahi akahesabu namba huku kuna wanaoamka saa11 wawahi kuhesabu namba dah!
 
shida ninayoiona ni hao wazazi kupeleka watoto wadogo shule za mbali, lazima tukubali kuwa mambo yamebadilika, nyakati hizi mama wa nyumbani hamna, na mbaya zaidi kumekuwa na changamoto nyingi sana kuhusu hawa wasichana wa kazi kiasi kwamba kimbilio la wazazi ni hizo Daycare

Sasa mzazi anaamka saa 12 kwenda kazini kwake analazimika kwenda na mwanae ili akamuache shule, kuhusu muda shule nyingi zinataka mtoto afike saa 1:30 asubuhi kwahiyo kama yuko mbali na shule ndio hayo ya kuamka saa 11
 
Back
Top Bottom