GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Acheni kuwachagulia Watoto wenu Fani ambazo nyie mmezifanya huku hadi kuwatishia kuwa wasipofuata basi mtawavulia Nguo zenu kwa Kuwalaani. Hivi inaingia Akilini kabisa Wewe Mzazi ni Injinia na kila Siku unaona Mwanao katika Masomo ya Sayansi anatepeta / hayawezi ila kule katika mengineyo ya Sanaa au Biashara anawakimbiza ile mbaya lakini bado unamlazimisha Mwanao ajikite katika Sayansi ili aje kuwa Injinia kama Wewe. Acheni huu Upuuzi na Heshimuni Hisia za Watoto wenu. Taaluma hairithishwi Kilazima bali matakwa na mapendeleo ya Mtoto juu ya kile anachokimudu na anachokiweza ndiyo Kipaumbele.
Leo GENTAMYCINE nimejivika Bomu la Kuwatetea Watoto kwani nimeona kuna mahala Wazazi tunawakosea pakubwa.
Leo GENTAMYCINE nimejivika Bomu la Kuwatetea Watoto kwani nimeona kuna mahala Wazazi tunawakosea pakubwa.