ππTena Umechukia balaahuyo babaako aache akili za kivuta bangi, mwanaume utaishi nae wewe sasa yeye anatia kauzibe ya nini? mahari 10m kwamba anakuuza au? wazazi kama hao ndio hua wanafanya wanaume wanakua na hasira hadi wanaua wake zao kwa kosa dogo tuu... mwambie ameniudhi sana.
Kwanini uwasaidie ukweni?..kwani huko ukweni hakuna wa kuwasaidia ?...πππUkweni.
Ni kweli mkuu uwasaidie ukweni kivipi haiingii akili mfano mume wa dada yangu awe anatusaidia kwenye familia yetu wakati sisi tupo vijana tuna nguvu za kuwatunza wazazi wetu .Kwanini uwasaidie ukweni?..kwani huko ukweni hakuna wa kuwasaidia ?...[emoji3][emoji3][emoji3]
Ndo namsubiria huyu jamaa aje aseme kwanini wasaidiwe.... naona umesema yaliyokua kichwani kwangu..πππNi kweli mkuu uwasaidie ukweni kivipi haiingii akili mfano mume wa dada yangu awe anatusaidia kwenye familia yetu wakati sisi tupo vijana tuna nguvu za kuwatunza wazazi wetu .
Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Na wewe ni miongoni mwa wanaotakiwa kusaidiaKwanini uwasaidie ukweni?..kwani huko ukweni hakuna wa kuwasaidia ?...πππ
Wewe umekuja kuomba ushauri au kufanya criticism kwa hoja zinazotolewa, nimefuatilia replies zako tu nimegundua hata huyo jamaa anayetaka kukuoa pengine kaingia cha kike, una kaujeuri fulani pengine pia umerithi toka kwa wazazi, who knowskwa io imeandikwa baba akuchagulie mume..Kama huna ushauri tulia
Nionyeshe ni wapi iliandikwa baba anaweza kukutafutia mume..Tumieni vizur maandiko sio kupotosha watu
Just for being sarcastic, pata mimba kushusha value ya mzigo.Habari zenu wana JF,
Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.
Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.
Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.
Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.
Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.
Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.
Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.
Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.
Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.
Habari zenu wana JF,