Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Wavulana naona mnatokwa povu ila hakuna mzazi anayefurahia mwanae kuolewa na mwanaume asiye na kipato. Subirini nanyi muwe baba mtafanya the same.
Hawa ndo wazazi wenye mindset mbovu, kama hupendi binti yako aolewe na mtu asiwe na kipato mtengeneze binti yako kwanza kujitegemea.

Wazee wa kisasa wanapambana kuwateneza mabinti zao kujitegemea.
Miaka ya kusubiri binti aolewe ndo shida ziishe ilishapita huu ulimwengu mwingine kabisa.
 
Sio kwamba aolewe ndio shida ziishe laa!! Ila jukumu la kutunza familia ni la mwanaume haijalishi binti ana kipato kiasi gani. Kwa hawa wazazi sidhani kama wana shida kihivyo maana kama kabati lake tu ni 3+m sio hawa wenzangu na mie.

Hapo anawaza ikiwa tu mahari ya 3m ni shida, sasa maisha yatakuwaje?
 
Mahari milioni 10 hyo baba mbona amevuka mipaka ya utu? Au ana mkopo bank anataka akaumalizie kwa hyo pesa?
 
bibie mfate jamaa mzalie kitoto kimoja tu
 
dah mwisho unaishia nyumbani, inabidi ujue yye alitoa mahari sh ngapi? mm hata laki tano sitoi
 
Uongo uongo, huu muandiko wa kiume ni story ya kubumba kama hadithi za kina kalimakenge
 
Yani wazazi wengine hawajui tuu ila ki ukweli hawa wanaume waoaji ukiwa treat kama watt wenu mtafaidika sana baadae waume zetu ni msaada mkubwa. Sasa unamuomba milioni 10 kesho umeugua au janga lolote limetokea atawasaidia kweli?
 
ufanye ivo kwa binti zako
Binti zangu nitawalea kwa kufuata kanuni, taratibu, sheria, Amri na misingi ya KIKRISTO.

Wakifika umri wa kuolewa tayari watakuwa wanajua mipaka yao na mipaka ya wazazi wao. Watakuwa wanajua mamlaka ya baba na mama ni yepi na watakuwa wanajua fika nini maana ya UTIIFU sio tu kwa wazazi wao, bali zaidi sana kwa MUNGU muumba wao.

Tatizo la mabinti na vijana hawajui mipaka na mamlaka ya wazazi wao. Kutokujua huko kunakosababishwa na malezi mabovu ndiyo kumepelekea watoto kuwa na viburi na kufikia hata mabinti kudharau mamlaka ya baba zao.

Narudia tena kusema; baba anayo mamlaka yote juu ya kumuoza binti yake, ikiwa ni pamoja na kuamua kiwango cha mahari. Tena baba anayo mamlaka yote ya kumkubali au kumkataa mchumba wa binti yake.

Rejea kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia utaona kuwa Eva hakumchagua Adamu, bali MUNGU akiwa kama Baba ndiye aliyempeleka Eva kwa Adamu.

Kitabu hicho hicho cha Mwanzo utaona Abrahamu ndiye alimtafutia mwanae Isaka mke. Rebeka aliletwa kwa Isaka na walikuwa hawajuani na hawajawahi kuonana. Lakini walioana na waliishi maisha ya raha mstarehe

Ukisoma Agano jipya utaona kuna pahala pameandikwa kuwa mambo hayo ya Agano la kale yaliandikwa kwa makusudi ili kizazi hichi kijifunze kutoka kwao.

Mwenye masikio na asikie!!!
 
Tatizo lako ni kuwachukulia wazazi wako kama "miungu" wako . Kuna mazingira unatakiwa uwaoneshe watu ikiwemo wazazi wako kwamba wewe ni mtu huru kimaamuzi.

Unashikilia msimamo kama una damu ya Mkwawa vile. With time watajifunza kuheshimu hisia zako. Tumia njia ngumu kuwapa funzo.
 
Ndo nyie mnaokufa kwa kukosa maarifa!! Endelea kukaza hilo fuvu
Leta hilo andiko linalosema wazazi kuwachaguliwa watoto wachumba
Siyo kila kitu kimeandikwa kwenye Biblia kama Amri isipokuwa mengine yameandikwa kama "muongozo" wa nini kifanyike.

NENO la MUNGU ndiyo MAARIFA tosha na mimi siwezi kufa kwa kukosa maarifa sababu MAARIFA hayo ninayo.
Soma Biblia kwa wakati wako utaona jinsi Abrahamu mtu aliyekuwa anapendwa sana na MUNGU, alimchagulia kijana wake mke.

Kijana wake aliitwa Isaka na mke aliyeletewa na baba yake aliitwa Rebeka. Isaka alipoletewa mke hakubishana na baba yake, bali alimpokea Rebeka kwa utiifu.

Soma kuhusu binti aliyeitwa Lea, jinsi alivyopewa Mume na baba yake. Lea hakubishana na baba yake bali alimpokea Yakobo na kuwa mumewe kwa utiifu mkubwa.

Soma kuhusu Yakobo, mama yake anamwambia usioe mke wa eneo hili bali nenda kijijini kwetu kwa mjomba wako na huko utajipatia mke. Yakobo hakubishana na mama yake bali allifanya kama alivyoagizwa kwa utiifu mkubwa.

Hawa wote walibarikiwa na MUNGU na moja ya sababu ya wao kubarikiwa ni UTIIFU kwa wazazi wao.

Mifano iko mingi sana kwenye Biblia, nikiandika yote nitajaza gazeti.
 
Pole
 
Unataka uolewe na mtu masikini ili uendeleze kizazi cha watu masikini......mimi nikichumbia sehemu wakanikataa huwa naogeza nguvu zaidi ya kupambana..najua kabisa wamenikataa kwa sababu ya umasikini wangu
 
Sema tu kwakua ni mzazi leo ningetoa tamko kali.
 
Alfa female speaking..! [emoji16][emoji16]
 
Muhaya na myakyusa utamjua tu hata bila utambulisho wa sura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…