Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 17,499
- 25,295
Wanajamvi habari za mapumziko.
Nikiri kwamba mimi nilisoma Mlimani, naumia sana nikisikia serikali hii inayonunua mindege inashindwa kuwakopesha wanafunzi kwa wakati.
Nikiri kwamba nilikuwepo na niligoma na kuandamana haswa pale mwaka 2004, serikali ya srlikali ya CCM chini ya Mzee Mkapa ilipitisha muswada wa bodi ya mikopo.
Kumbuka nilianza chuo kama mtoto wa mkulima nikiwa na mkataba wa kusomeshwa bure kama walivyosomeshwa hawa leo wanaojiita wazalendo na ambao hawalipi mikopo kabisa.
Wakati nasoma UDSM, Miaka ile ilikuwa ni nadra sana kukuta mtu analipiwa na wazazi wake, walikuwepo ila wachache na walihesabiwa kama waliofeli japo sio kweli.
Tuliupinga muswaada ule kwakuwa tulijua ulikuwa na madhara huko mbeleni mfano unaongezewa makato toka 8%- 15% wakati mkopo bado unaendelea kulipwa? Sidhani kama ilishawahi kufanyika popote.
Rais Magufuli kafanya tena katika kipindi ambacho hapakuwa na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma.
Nawakumbuka kina SIRIWA, NDASKOI, TWEVE B TWEVE NA ALBERTO MSANDO hawa waliongoza mapambano kuwakabili makuhani ya CCM.
Narudi kwenye mada, zipo tambo za kisiasa toka kwa watu walewale waliotengeneza tatizo. Wanadai Tanzania kuna elimu bure. Wanadai wanatoa (kama hisani kumbe ni kodi zetu ) bil 18 kila mwezi kulipia elimu.
Ukiwauliza elimu gani wanakwambia msingi hadi secondary (universal/UPE) kama alivyofanya Mwalimu Nyerere. Kwanini wanalipa watakwambia wazazi ni masikini.
Japo hawatuambii hawasemi hiyo bure ni kwenye nini na nini maana watoto wanashinda njaa shuleni? Wazazi wanalipa nauli wakati wanajeshi na mapolisi wenye mishahara na marupurupu wanapanda bure huku watoto wetu wakisukumwa japo wanalipa 200/= zao.
Leo kuna wanafunzi wangapi wanaoshindwa kuendelea na masomo yao kisa mzazi kukosa pesa ya ADA za vyuo?
Kuna wazazi wangapi wanafilisika kwa kuuza mali zao ili kulipia ada za vyuo tena pasi na uhakika wa ajira kwa watoto wao pindi wamalizapo shule?
Najiuliza maswali mengi sana kwamba mzee "MBILIMBI KALI" Wa ulanga aliyeshindwa kulipia da ya shule ya msingi na sekondari anapata wapi mamilioni ya kulipia ada ya vyuo vikuu?
Kama kweli ule ni MKOPO kwanini wanaokopeshwa wakidai mkopo wao wanapaswa kutoa wanawafukuza vyuoni?
Hii serikali inayojitapa kila siku kwamba ina pesa za kutosha inashindwaje kulipa mikopo ya wanafunzi?
Enyi wana UDSM songeni mbele msikatishwe tamaa na hawa wajamaa songeni mbele msikatishwe tamaa na hawa mabeberu wanaojidai wajamaa kumbe wanamiliki mahekalu na watoto wao wanasoma nje wakitwambia na kutuaminisha kwamba wao ni wajamaa kumbe ni wakwasi wakubwa.
VIVA UDSM, VIVA DARUSO, VIVA SOLIDARITY FIREVER, NEVER GIVE UP, MIKOPO NI HAKI YENU
Swali ni je? mzazi masikini wa kule CHATO anayeshindwa kulipa