Wazazi wengi hawana Home Curriculum ( Mtaala wa Nyumbani)

Wazazi wengi hawana Home Curriculum ( Mtaala wa Nyumbani)

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
1. Wazazi wengi hawana home Curriculum. Wazazi wanapaswa kuwa na mtaala wa Nyumbani maalumu Kwa ajili ya kuwafundisha watoto wao stadi za maisha .

2. Kwa sababu ya kukosa mtaala wa Nyumbani wazazi huwaona watoto Kero Wawapo nyumbani jambo ambalo ni upumbavu WA Hali ya juu sana... Ndio maana watoto wakifanya utundu nyumbani wakati WA likizo utamsikia mzazi anasema " Bora shule zifunguliwe " ni kauli ya kipumbavu Sana Kwa mzazi kuongea ujinga huu lakini yote Kwa sababu wazazi wengi wa kitanzania hawajitambui.

3. Wazazi wanao wapeleka watoto wao shule za English Mediums hawana Akili na hawajitambui . Akaulizwa wasio na hela tu na wenye hela? Akasema wote tu Kwa sababu kwenye shule za English Mediums watoto hawapewi kinacho endana na thamani ya hela inayo lipwa .

Shule inatakiwa isaidie kutoa nje kilichopo ndani ya mtoto kitu ambacho shule za EMs hawana. Unapopeleka mtoto kwenye shule unayolipia kitu cha kwanza kabisa lazima waalimu wagundue kipaji na talanta iliyomo ndani ya mtoto na kisha wamsaidie kumjenga na kumuendeleza kitu ambacho shule za EMs hawana uwezo huo.

4. Tajiri hawezi mpeleka mtoto wake shule ya English Medium. Matajiri huwapeleka watoto Wao shule za mtaala wa Cambridge ( International Schools) ambako watoto hupewa kinacho endana na thamani ya mtoto ). Matajiri hawatumii hela zao kizembe

Masikini ndio Wanao tumia hela zao kizembe . Wanao peleka watoto Wao shule za EMs wengi Wao ni masikini na hawana uelewa. Ndio maana kila Ikifika wakati WA kulipa ada utawasikia wakisema " Aisee nna mambo mengi Mie, ada sijalipa, shule zinakaribia kufunguliwa. Upumbavu mtupu. Yani hawana tofauti na masikini lofa mwenye kadi Kumi za michango ya harusi anasema " Aisee nina michango mingi ya harusi!" Kwani umelazimishwa kuchangia harusi?

5. Shule za English Mediums Sio shule za private, ni shule za Public zenye majengo binafsi. Shule ya private lazima itumie mtaala tofauti na public.

6. Shule za English Mediums hazifundishi Kwa kiingereza ila masomo yanakuwa manetioned Kwa lugha ya kiingereza.

7. Shule za mtaala wa NECTA watoto hawaendi kusoma shule ila wanaenda kukusanya notes .

8 . Watoto waende shule saa 4 asubuhi warudi nyumbani saa 8. Wasome Kwa lisaa limoja au mawili masaa mawili wacheze.

9. Watoto wakiwa shuleni wanafurahia Zaidi michezo na wenzao Kuliko kusoma Kwa sababu watoto wanaenjoy Zaidi kusoma. ( NA KWELI NIMEKUMBUKA MIAKA YETU KULIKUWAGA NA WAASUBUHI NA WA SAA4 HADI TUKAWA NA WIMBO WA SAA4 MAKOMBO WA ASUBUHI OYE OYE.

10. Watoto wana michezo mingi Sana hulala wakiwa wamechoka. Mnawaamsha saa Kumi na moja waende shule wanaenda kulala kwenye bus la njano na darasani. Mna watesa watoto wenu.

Hayo si maneno yangu ila maneno ya Jospeh Mrindolo WA WACHOKONOZI
 
Attachments

  • Screenshot_20250119-104802.png
    Screenshot_20250119-104802.png
    385.3 KB · Views: 4
Heading inasema HOME CURRICULUM lakini mada yote imeongelea watu kusomesha watoto English Medium.

Mzee tafuta hela au kama unakwamwa omba watu wakuonyeshe mirija ya hela ilipo.

Ukishindwa kabisa nenda kausha damu mrudishe huyo uncle wetu kule English Medium ulipomtoa.
 
Wanaosema kwamba Bora shule zifinguliwe ili mtoto atoke nyumbani ni dalili ya umasikini.Maana unakuta mtu Hana shughuli yeyote nyumbani ya kufanya mwanafunzi aifanye ili asionekane kama kero. Wewe mtu anakajumba kiwanja Cha 20×20 hakuna hata ufugaji nyumbani zaidi ya kuangalia TV hapo lazima atamani shule zifunguliwe.Pamoja na Hivyo,EM ni nzuri kuliko shule za serikali.
 
Huwa nawahurumia sana watoto wanaoamka saa 10 au 11 alfajiri ili wawahi school bus, dogo hata halali vizuri na ndo kwanza ana miaka chini ya kumi.
Akiondoka hiyo saa 12 asubuhi ni mpaka school bus imrudishe saa 12 jioni.

Hizi shule zizingatie utoto wa watoto, baadhi ya shule ni kama jela.
 
Kusomesha EM ili hali kipato ni kidogo ni moja ya dalili za utumwa. ila watoto walio na wanaosomea kayumba wana advantage kubwa hapo mbeleni hata wakikosa ajira watajiajiri wenyewe, hawa EM wakikosa ajira ndo tunazalisha "kuluna" (sorry kama nimekosea jina) ya DRC kwa sababu wakat anasoma,ali deal na kusoma tu pasipo kujishughulisha na kazi zingine huku akiamini akimaliza shule ajira ni uhakika,mambo yakiwa kinyume chake ndo mwanzo wa kutengeneza magenge ya kiharifu.
 
Tulijua umewaachia walimu wa kayumba wamalize kila kitu na watoto wako 🤣🤣🤣

ANYWAY...

KURUDISHA MTOTO KAYUMBA NI MOJA LA JAMBO LA KIPUUZI KUWAHI KUFANYIKA NA AKILI YA KIMASIKINI YA MWAFRIKA.
Na kumpeleka mtoto wako shule ya EM wakati wewe ni masikini huna hela unapanda daladala ni mental case.

The proof is here 👇👇👇👇
 
Attachments

  • Screenshot_20250119-115202.png
    Screenshot_20250119-115202.png
    150.8 KB · Views: 3
Kusomesha EM ili hali kipato ni kidogo ni moja ya dalili za utumwa. ila watoto walio na wanaosomea kayumba wana advantage kubwa hapo mbeleni hata wakikosa ajira watajiajiri wenyewe, hawa EM wakikosa ajira ndo tunazalisha "kuluna" (sorry kama nimekosea jina) ya DRC kwa sababu wakat anasoma,ali deal na kusoma tu pasipo kujishughulisha na kazi zingine huku akiamini akimaliza shule ajira ni uhakika,mambo yakiwa kinyume chake ndo mwanzo wa kutengeneza magenge ya kiharifu.
100%Fact
 
Home economics ni muhimu sana. Watoto wakiwa nyumbani wajifunze masuala ya nyumbani, uchumi wa nyumbani na mtaani

Sijawa na watoto wakubwa ila mimi wakifika umri wa shule, wakiwa shuleni wafanye ya shuleni, wakiwa nyumbani wafanye ya nyumbani.

Kwangu hakutakua na holiday package wala ujinga gani, na hata homework za shule ni ujinga, kama ipo basi only zoezi la muda mfupi sana.

Hii ni kanuni zinazotumiwa na matajiri kwa watoto wao, ndio maana hukuti hawa watoto wakimaliza shule ma matokeo ya As wala Bs lakini ndio viongozi ama wakuu wa taasisi binafsi ama za umma. Hata kwa wahindi wa hapa Tanzania.

Watoto wakitoka shule hufundishwa maisha halisi ya mtaani. Hii inawafanya watoto kuanza kupata life skills mapema sana kuliko kukomaa na ma As ambayo yanapatikana kwa kuiba mitihani. (Kuna shule kule Serengeti inaitwa Twibhoki, kila mwaka ilikua inakua ya 10 bora kitaifa, inatoa wanafunzi 5 kati ya 10 bora nchini, walivyofuatiliwa ikakutwa inaiba mitihani, watoto wana majibu yanayofanana darasa zima, ikafungiwa na imepotea kabisa)
 
Huwa nawahurumia sana watoto wanaoamka saa 10 au 11 alfajiri ili wawahi school bus, dogo hata halali vizuri na ndo kwanza ana miaka chini ya kumi.
Akiondoka hiyo saa 12 asubuhi ni mpaka school bus imrudishe saa 12 jioni.

Hizi shule zizingatie utoto wa watoto, baadhi ya shule ni kama jela.
100% Fact
 
Back
Top Bottom