Ego is the Enemy
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 8,201
- 16,246
Wewe hii shule kwani haipo Tena , ishu watu wengi hawajui mindset za wafanyabiashara wanavyocheza na akili za mteja ili achukue hela zake. Mie kinachonisaidia ni kuwa since standard wani Maisha yangu ni ya dukani naenda shule nikirudi ni kuuza dukani, so huwa najua akili ya mfanya biashara ilivyo, yaani anajua mteja akili ilivyo, mfano watu wengi yaani wengi wanaamini kuwa chenye gharama ndicho kina ubora ,Kuna muda kitu kilikuwa kikiganda dukani nakipandishia Bei yaani hii akili from nowhere sijui Ila ni from universe nashangaa kitu kinanunuliwa na nilikuwa mtt mdogo, pia Kuna muda mchele wa aina moja nagawanya kwa beseni mbili naandika 200/kg na mwingine 250/kg nakuambia wateja Wana concentrate kwa hii ya 250 wananiambia nipunguzie hii nachukua kilo nyingi nabakia nacheka mwenyewe.Home economics ni muhimu sana. Watoto wakiwa nyumbani wajifunze masuala ya nyumbani, uchumi wa nyumbani na mtaani
Sijawa na watoto wakubwa ila mimi wakifika umri wa shule, wakiwa shuleni wafanye ya shuleni, wakiwa nyumbani wafanye ya nyumbani.
Kwangu hakutakua na holiday package wala ujinga gani, na hata homework za shule ni ujinga, kama ipo basi only zoezi la muda mfupi sana.
Hii ni kanuni zinazotumiwa na matajiri kwa watoto wao, ndio maana hukuti hawa watoto wakimaliza shule ma matokeo ya As wala Bs lakini ndio viongozi ama wakuu wa taasisi binafsi ama za umma. Hata kwa wahindi wa hapa Tanzania.
Watoto wakitoka shule hufundishwa maisha halisi ya mtaani. Hii inawafanya watoto kuanza kupata life skills mapema sana kuliko kukomaa na ma As ambayo yanapatikana kwa kuiba mitihani. (Kuna shule kule Serengeti inaitwa Twibhoki, kila mwaka ilikua inakua ya 10 bora kitaifa, inatoa wanafunzi 5 kati ya 10 bora nchini, walivyofuatiliwa ikakutwa inaiba mitihani, watoto wana majibu yanayofanana darasa zima, ikafungiwa na imepotea kabisa)
Pia nimesoma na nimeona kusoma sio kuwa ni hela Bali Kama mtt anao uwezo na anapenda kujisomea that's the gift, nakumbuka la Tano mwalimu alinifahamu akaniuliza unasomaga twisheni akaniambia kalete your maths exercise nikampelekea.
Hata tulivyoenda nje kusoma Russia na through government scholarship bana Kuna wabongo walijifunza kirusi mwaka mmoja wakaanza kusoma university pamoja na warusi Sasa si Kuna watu wanawafundisha warusi hao hao kuwa hapa ni ivi rector alisema.
So naamini kuwa kuelewa kitu sio lugha bana sema watu tunataka ku take pride kuwa tunasomesha na pia Yale machungu ya kukosa elimu na kunyanyaswa na wasomi , pia kuona wasomi jirani yako wanaongea English so unakuwa na maumivu mno ya kuja kuziba ilo PENGO ama maumivu ayo. Cheki msukuma na kishimba wanavyohangaika wanaponda wasomi na huku nafsini mwako ni maumivu yanawasumbua wanadisi elimu na huku vijana wao wanawasomesha, shigonga akagonga mwamba akataka kusoma udsm ili na yeye awe na Ile sifa kusoma chuo kikongwe nchini chenye wanaosoma hapo wenye uwezo mkubwa.
Sasa bana akaombwa cheti cha foo akaja kumaindi mpaka bungeni kuwa amekataliwa.
Msukuma anaponda wasomi huku akaenda kununua cheo cha usiku kuitwa doctor ya heshima.
Akili zetu ama tulivyo wanadamu ni sawa na Ile hadithi ya sizitaki hizi mbichi. Mwanamke kwanza Malaya baada ya kuwa amekukataa unatafuta validation ya roho yako itulie na unaamini ivyo Mana maumivu ni makali ya kukosa mtt mkali.
Ila ingawa Mwanzoni ulikuwa unamtaka kwa cost zote,
English bana sio dili kubwa mno Kuna muda hata mie nilikuwa ama nikiongea na mtu ana doubt Kama mie ni Mtanzania, chuoni kwa bongo nilikuwa natongoza mademu kwa English na ninawala kweli kweli Mana hawajui kujitetea kwa English wanabakia yes and no mara ofcourse.