Hata mimi nimesoma kayumba ya enzi zile, ilikuwa Zanaki Primary, lakini kipindi kile elimu ilikuwa inaufadhali hizi shule, tulikuwa tunasoma na wahindi na waraabu wenye hela, fikiria nilikuwa darasa moja na mtoto wa hawa Suchak wenye ukwasa sasa hivi, na pia kulikuwa na walimu wahindi wanatufudisha miaka ile.
Kwa sasa kama najiweza sipeleki mtoto wangu hizi shule, zimekuwa choka mbovu ndio maana huoni mtoto hata mmoja wa kihindi au mwarabu yuko hizi shule. kwanini hujiulizi hilo, na zamani walikuwa wengi, ile Upanga Primary ilikuwa kama shule ya wahindi tupu na ilikuwa st kayumba.......