sijawahi kumsoma mario puzzo,umeni inspire ngoja nitafute kitabu chake,vinahusu nini umafia kama ninavyoujua mie?
Lizzy darling wanaume huwa hawayumbishwi hovyo hasa na mwanamke aliekwisha mwacha kwa amri yake mwenyewe. Ukiona huyo mume anayumbishwa na mzazi mwenzie mara nyingi huwa kuna hivi vitu.
Kaaazi ni kwakho!
Nilikua napita tu
Mimi nadhani watoto ni vema wakae na mama yao uendege kuwatembelea tu. Ni ngumu sana kukaa na amani kama mama wa watoto yuko hai. Lazima atakuwa anakagua wanae wanaishi vipi, mwisho wa siku ugomvi. Mama wa kambo hata akiwapenda hao watoto bado inaweza kuwa shida vile vile. Yaani sisi wamama ukifikiria ulivyoangaika kuwapata hao watoto leo hii wakuone kama mpita njia, lazima ulete shari tu watoto waendelee kuku value kuliko huyo mama kambo.
Labda nitoke nje ya mada kidogo ili muweze pata picha tofauti,mambo mengi hutegemea mwanamme alivyo imara na kuwa na msimamo.Mimi baba alikuwa na wake wawili na tulikuwa tunaishi karibu na ndugu zangu wa mama mwingine,baba alikuwa anafanya kila kitu sawa kwa wake na watoto wote,tulipendana,tembeleana na ukijiskia unaenda kula au kulala nyumba ingine au wa kule nae anafanya hivyo.Kina mama walikuwa wanafatana sokoni,maharusini,misibani e.t.c naona kila kitu kinategemea mazingira anayoanda mwanamme.
Kila mtoto alelewe na mama yake kama huyo mama yupo hai.....
Mtoto aende kwa mama wa kambo akiwa na umri zaidi ya miaka 15.....
Lizzy ahsante kwa kufungua hii thread.Si nia yangu kujivua nguo humu MMU lakini kwa kuwa umechokoza hii mada ngoja nikupe uzoefu wangu binafsi. Kwa kifupi:
1. Nimezaa na wanawake kadhaa.
2.Nina watoto kadhaa wa kike na wa kiume.
3. Wanangu ni wakubwa,mdogo yuko sekondari ,wakubwa wanajitegemea,wa kati kati hapo wako hatua kadhaa za chuo.
4.Wengine niliwazaa ndani ya ndoa na wengine nje ya ndoa,whatever that means,kwangu mimi mtoto ni mtoto,i don't care about these social semantics.
5.Nimelea wanangu katika mazingara yote,ya kuwa ndani ya ndoa na mke akilea so called watoto wa kambo na ya mimi kuwa single father na wanangu wote.
UZOEFU WANGU:
1. So called mama wa kambo ana cope kirahisi zaidi na watoto wa kiume kuliko wa kike.
2. Utake usitake so long as mwanamke umezaa naye huyo unaye for life,atakufuatilia maisha yako binafsi mpaka siku unaingia kaburini,awe kaolewa awe hajaolewa.
3. Mwanamke ukisha zaa naye atakuwa radhi uzeeke bila kuwa na mke kuliko uoe mwanamke mwingine(hata kama yeye kaolewa).
4. Kama umeoa mkeo siku zote atakuwa suspicious na mahusiano yako na ma ex wako,hata kama wameolewa.
USHAURI:
1.Kama wewe ni kijana wa kiume jitahidi usizae kabla ya kuoa na ukishaoa kama utakuwa na hawara usizae naye.It is too expensive materially ,mentally and emotionally.
2. Kama wewe ni msichana ikiwezekana usizae na mme wa mtu,ikibidi kama unaona miaka inakwenda,ukizaa na mme wa mtu usim harass mkewe na jitahidi uwe na nguvu za uchumi za kulea mwenyewe mwanao.Baba mzazi akichangia,pokea,asipoleta achana naye,ila usizuie contact na mwanae,acha mtoto amjue baba yake,na usimpige baba majungu kwa mtoto,utamharibu mtoto kisaikolojia,hasira zako zitunze kifuani mwako.
3.Vyovyote vile,UWE MWANAMKE/MWANAUME,ukijaliwa mtoto mlee,usikwepe majukumu,tabia ya kutelekeza watoto mwachie nguruwe anayezaa na kula wanae.
4.Kama wewe ni mwanaume piga ua usikubali mwanaume mwingine akulele mwanao,ni aibu.Hata kama mzazi mwenzio kaolewa wewe peleka school fees na vifaa muhimu vya mtoto.
KWA WANAUME:
Ukiona vimekuzidi,tafuta talaka,ishi mwenyewe na wanao,they are too precious to suffer kisa eti ndoa,hakuna raha duniani kama kulea watoto,asikudanganye mtu,wakishakua wakajitegemea then tafuta mwanamke wa kuzeeka naye na siku zote kumbuka hii signature ya mdau mmoja wa MMU:
Happy is a man who is a woman's 1st love and also happy is a woman who is a man's last love.
Ciao na kunradhi kwa mchango mrefu,ningeweza kuongea mengi zaidi ya haya,lakini kwa leo tuishie hapa.
Mchana mwema(Africa),asubuhi njema(America) na jioni njema(Far east)
Labda nitoke nje ya mada kidogo ili muweze pata picha tofauti,mambo mengi hutegemea mwanamme alivyo imara na kuwa na msimamo.Mimi baba alikuwa na wake wawili na tulikuwa tunaishi karibu na ndugu zangu wa mama mwingine,baba alikuwa anafanya kila kitu sawa kwa wake na watoto wote,tulipendana,tembeleana na ukijiskia unaenda kula au kulala nyumba ingine au wa kule nae anafanya hivyo.Kina mama walikuwa wanafatana sokoni,maharusini,misibani e.t.c naona kila kitu kinategemea mazingira anayoanda mwanamme.
Partner mi siogopi bwana sema basi tu sijamwona wakunifanya nitamani!!
Me is waiting.......
Ndoa hizi ambazo mmoja ana mtoto huwa zinachanganya sana wanandoa hasa yule mzazi mwenza anapoingilia, mie nashangaa huyu mwanamke aliyeachana huwa anakuwa na maisha yake na mtu mwingine , huku bado anataka amshikie mwenzake balls zake, hapa mwanamme asipokuwa makini ndoa inayumba haswa, mwanaume kuwa na mipango na mipaka na umwonyeshe mzazi mwenzako hutaki akuingilie kwenye maamuzi yako.
Kuhusu shule unaweza ukawa unalipa moja kwa moja kwenye account ya shule kuepusha usumbufu kama mwanamke anakuwa na tamaa. Mie nashangaa mwanamke utahamisha watoto wako shule nzuri sababu ya pesa kweli?
Mimi shule,medical insurance nalipa mwenyewe na soon nitaanza kwenye mambo mengine! maana longolongo kibao mara mtoto anaumwa, mara anataka nini! ilimradi tu akupe attention na utoe pesa! mwanzo niliona poa lakini baada ya kugundua hata vitu muhimu ukimpa pesa amfanyii mtoto nimebadilika mbaya!
Duhh!............haya bana!
Well hongera kwa kutambua situátion na kwakujitambua pia....komaa hivyo hivyo ili mradi tu mahitaji ya mtoto ufikishe!Mimi shule,medical insurance nalipa mwenyewe na soon nitaanza kwenye mambo mengine! maana longolongo kibao mara mtoto anaumwa, mara anataka nini! ilimradi tu akupe attention na utoe pesa! mwanzo niliona poa lakini baada ya kugundua hata vitu muhimu ukimpa pesa amfanyii mtoto nimebadilika mbaya!
Duh! Sisi tuliolelewa na Mama wa Kambo(s) tunayo mengi ya kuandika - A book may be - kuhusu maisha ya kulelewa na Mama wa Kambo!