Wazazi wenza...!

Wazazi wenza...!

sijawahi kumsoma mario puzzo,umeni inspire ngoja nitafute kitabu chake,vinahusu nini umafia kama ninavyoujua mie?

Bishanga vitabu vyake ni adimu saana yahitaji uvumilivu kutafuta...
kama kweli ni mpenzi wa kusoma vitabu, huyo baba ukisoma kitabu chake
utataka tu usome kingine... pia kwa urahisi kama hujaangalia movie yake
hata moja basi waweza enda nunua movie badala ya vitabu..
Tafuta God father 1,2, & 3 maana ni muendelezo na kuna movie ya The last Don (spectacular..)
Huyu baba ndo mwanzilishi wa uwepo wa superman myth in novels, movies and series...
 
Lizzy darling wanaume huwa hawayumbishwi hovyo hasa na mwanamke aliekwisha mwacha kwa amri yake mwenyewe. Ukiona huyo mume anayumbishwa na mzazi mwenzie mara nyingi huwa kuna hivi vitu.

1. Huyo baba pamoja na kuachana na huyo mama bado wanaibanaga akiwa na hamu anaenda ooooh unajua wewe bado ni mke wangu tu, tuna watoto na blah blah nyiiiiiiiiiiiiiingi kama mama nae bado anavutiwa na huyo mzazi mwenzie basi anamgea tu kitasa afungue. Na huyo mama atakua anampelekesha huyo baba na asipindue cause anajua akiwa mbishi siku nyingine akiwa na hamu atanyimwa.

2. Inawezekana wewe mke wa sasa uliingilia hiyo ndoa wakati hawajaachana, ukajifanya mwema mpaka akamuona mkewe hafai, wakaachana. Matokeo yake ulivyoingia kwenye hiyo ndoa kama ilivyo kawaida yetu wamama ukaanza kuonyesha your true colour si yule aliekua mnyenyekevu mpaka baba akaamua kubwaga manyanga kule na kukuoa wewe.

Baba anaanza kulinganisha na kusema dah! sasa nimefanya nini? kumbe wanawake wote ni sawa? tena afadhali hata ya mama fulani kwenye hili alikua anaafadhali, wewe hujui mwenzio anawaza nini, kwa hiyo anaakua anamfanyia huyo mama kila anachodemand kwa mgongo wa watoto na kukudanganya wewe anapelekeshwa kumbe ashachoka vituko vyako so anaamua kutunza kule kwa nguvu zote kwa ajili ya watoto wake.

Angalizo:
Ukiamua kuolewa na mume mwenye watoto kwanza jiulize kwa makini kwa nini aliachana na yule mkewe wa kwanza? sio unakurupuka tu na wengine utasikia yeye kashindwa kumlea mume ngoja tumuonyeshe sie tunaweza, kumbe hujui huyo baba nae ana matatizo yake ambayo yule mke alikua anayashindwa na ukiyakuta unaanza kuleta jeuri mwenzio anamkumbuka wa zamani kwani kwa hayo aliweza kuwa na uvumilivu kidogo.

Pili, mwanaume alieacha mke huwa anakua na maumivu moyoni so ukikosea tu anaunganisha yako na ya mkewe aliemuacha yote unarundikiwa wewe, tena utamsikia kabisa yaani wewe na yule sawa sawa tena wewe umezidi afadhali ya yule mama fulani, kifupi unatakiwa uwe makini sana. Huo ni ushauri tu mdogo kwa wadada mnaotarajia kuolewa na wababa walioacha wake au uko unafanya kila jitihada amuache mkewe aje kuwa wako.

Kaaazi ni kwakho!

Nilikua napita tu
 
Duh! Sisi tuliolelewa na Mama wa Kambo(s) tunayo mengi ya kuandika - A book may be - kuhusu maisha ya kulelewa na Mama wa Kambo!
 
Lizzy darling wanaume huwa hawayumbishwi hovyo hasa na mwanamke aliekwisha mwacha kwa amri yake mwenyewe. Ukiona huyo mume anayumbishwa na mzazi mwenzie mara nyingi huwa kuna hivi vitu.

Kaaazi ni kwakho!

Nilikua napita tu

Maty... me like na dah! umepita kwa kishindo....
 
Lizzy ahsante kwa kufungua hii thread.Si nia yangu kujivua nguo humu MMU lakini kwa kuwa umechokoza hii mada ngoja nikupe uzoefu wangu binafsi. Kwa kifupi:
1. Nimezaa na wanawake kadhaa.
2.Nina watoto kadhaa wa kike na wa kiume.
3. Wanangu ni wakubwa,mdogo yuko sekondari ,wakubwa wanajitegemea,wa kati kati hapo wako hatua kadhaa za chuo.
4.Wengine niliwazaa ndani ya ndoa na wengine nje ya ndoa,whatever that means,kwangu mimi mtoto ni mtoto,i don't care about these social semantics.
5.Nimelea wanangu katika mazingara yote,ya kuwa ndani ya ndoa na mke akilea so called watoto wa kambo na ya mimi kuwa single father na wanangu wote.
UZOEFU WANGU:
1. So called mama wa kambo ana cope kirahisi zaidi na watoto wa kiume kuliko wa kike.
2. Utake usitake so long as mwanamke umezaa naye huyo unaye for life,atakufuatilia maisha yako binafsi mpaka siku unaingia kaburini,awe kaolewa awe hajaolewa.
3. Mwanamke ukisha zaa naye atakuwa radhi uzeeke bila kuwa na mke kuliko uoe mwanamke mwingine(hata kama yeye kaolewa).
4. Kama umeoa mkeo siku zote atakuwa suspicious na mahusiano yako na ma ex wako,hata kama wameolewa.
USHAURI:
1.Kama wewe ni kijana wa kiume jitahidi usizae kabla ya kuoa na ukishaoa kama utakuwa na hawara usizae naye.It is too expensive materially ,mentally and emotionally.
2. Kama wewe ni msichana ikiwezekana usizae na mme wa mtu,ikibidi kama unaona miaka inakwenda,ukizaa na mme wa mtu usim harass mkewe na jitahidi uwe na nguvu za uchumi za kulea mwenyewe mwanao.Baba mzazi akichangia,pokea,asipoleta achana naye,ila usizuie contact na mwanae,acha mtoto amjue baba yake,na usimpige baba majungu kwa mtoto,utamharibu mtoto kisaikolojia,hasira zako zitunze kifuani mwako.
3.Vyovyote vile,UWE MWANAMKE/MWANAUME,ukijaliwa mtoto mlee,usikwepe majukumu,tabia ya kutelekeza watoto mwachie nguruwe anayezaa na kula wanae.
4.Kama wewe ni mwanaume piga ua usikubali mwanaume mwingine akulele mwanao,ni aibu.Hata kama mzazi mwenzio kaolewa wewe peleka school fees na vifaa muhimu vya mtoto.
KWA WANAUME:
Ukiona vimekuzidi,tafuta talaka,ishi mwenyewe na wanao,they are too precious to suffer kisa eti ndoa,hakuna raha duniani kama kulea watoto,asikudanganye mtu,wakishakua wakajitegemea then tafuta mwanamke wa kuzeeka naye na siku zote kumbuka hii signature ya mdau mmoja wa MMU:
Happy is a man who is a woman's 1st love and also happy is a woman who is a man's last love.
Ciao na kunradhi kwa mchango mrefu,ningeweza kuongea mengi zaidi ya haya,lakini kwa leo tuishie hapa.
Mchana mwema(Africa),asubuhi njema(America) na jioni njema(Far east)
 
Mimi nadhani watoto ni vema wakae na mama yao uendege kuwatembelea tu. Ni ngumu sana kukaa na amani kama mama wa watoto yuko hai. Lazima atakuwa anakagua wanae wanaishi vipi, mwisho wa siku ugomvi. Mama wa kambo hata akiwapenda hao watoto bado inaweza kuwa shida vile vile. Yaani sisi wamama ukifikiria ulivyoangaika kuwapata hao watoto leo hii wakuone kama mpita njia, lazima ulete shari tu watoto waendelee kuku value kuliko huyo mama kambo.

Hapo pa kwenda kuwatembelea napo issue. Assuming huyo mzazi mwenza ameshaolewa na ana nyumba yake, unaenda kumgongea mume mwenzio kuwa umekuja kuwaona wanao? Kwa wababa wa Kiafrika nnavyowaelewa mie (kwa uelewa mdogo tu), siamini kama ni kitu watakachokifurahia.

Haya twende upande wa pili ambao mzazi huyo hajaolewa anaishi mwenyewe, huyo baba akienda kutembelea wanae mmh, kama naona. Enhe, anapewa kikombe cha chai na chakula. Macho makavu kuwa amekuja kuwaona wanae, anakaa masaa yake mawili matatu anaaga anaondoka. Mmh kwa wababa wa kiafrika wale wale nnaowakumbuka mie kwa uelewa wangu mdogo! mmh...ngoja niishie hapa jamani, khaa!
 
Mada ngumu kwa kweli. Ukweli unabaki pale pale, kuzaa nje ya ndoa kunaleta matatizo baada ya ndo. If you can choose bora kuolewa/kuoa mtu asiye na mtoto.

Tena naona ni better kwa wale wanaooa wake wengi kwani watoto wanakuwa chini ya uangalizi wa mama zao Ila hii ya nilizaa kabla sijaoa; in most cases watoto wanateseka, kama si watoto basi kama mume ataweza kumantain mapenzi kwa wanawe basi mke cha moto anakiona.
 
Labda nitoke nje ya mada kidogo ili muweze pata picha tofauti,mambo mengi hutegemea mwanamme alivyo imara na kuwa na msimamo.Mimi baba alikuwa na wake wawili na tulikuwa tunaishi karibu na ndugu zangu wa mama mwingine,baba alikuwa anafanya kila kitu sawa kwa wake na watoto wote,tulipendana,tembeleana na ukijiskia unaenda kula au kulala nyumba ingine au wa kule nae anafanya hivyo.Kina mama walikuwa wanafatana sokoni,maharusini,misibani e.t.c naona kila kitu kinategemea mazingira anayoanda mwanamme.
 
Uporoto hiyo iliwezekana sababu mzee wako alikua stable na alijenga msingi mzuri saana katika familia yenu... familia za sasa hivi wanawake tumeota mbawa - hata ukiwa na wanawake wawili woote wawili hawaki kua karibu; alafu ukweli usiopingika ni kua mara nyingi akina baba akiachana na mke wa kwanza hata awapende vipi watoto wake akioa wa pili na akazaa nae huyo mpya in time mapenzi yanahamia zaidi kwa hawa watoto ambao wako within reach... inasikitisha.. wengine hata haangaiki mradi anawarushia vipesa vya hapa na pale..
 
Lizzy ahsante kwa kufungua hii thread.Si nia yangu kujivua nguo humu MMU lakini kwa kuwa umechokoza hii mada ngoja nikupe uzoefu wangu binafsi. Kwa kifupi:
1. Nimezaa na wanawake kadhaa.
2.Nina watoto kadhaa wa kike na wa kiume.
3. Wanangu ni wakubwa,mdogo yuko sekondari ,wakubwa wanajitegemea,wa kati kati hapo wako hatua kadhaa za chuo.
4.Wengine niliwazaa ndani ya ndoa na wengine nje ya ndoa,whatever that means,kwangu mimi mtoto ni mtoto,i don't care about these social semantics.
5.Nimelea wanangu katika mazingara yote,ya kuwa ndani ya ndoa na mke akilea so called watoto wa kambo na ya mimi kuwa single father na wanangu wote.
UZOEFU WANGU:
1. So called mama wa kambo ana cope kirahisi zaidi na watoto wa kiume kuliko wa kike.
2. Utake usitake so long as mwanamke umezaa naye huyo unaye for life,atakufuatilia maisha yako binafsi mpaka siku unaingia kaburini,awe kaolewa awe hajaolewa.
3. Mwanamke ukisha zaa naye atakuwa radhi uzeeke bila kuwa na mke kuliko uoe mwanamke mwingine(hata kama yeye kaolewa).
4. Kama umeoa mkeo siku zote atakuwa suspicious na mahusiano yako na ma ex wako,hata kama wameolewa.
USHAURI:
1.Kama wewe ni kijana wa kiume jitahidi usizae kabla ya kuoa na ukishaoa kama utakuwa na hawara usizae naye.It is too expensive materially ,mentally and emotionally.
2. Kama wewe ni msichana ikiwezekana usizae na mme wa mtu,ikibidi kama unaona miaka inakwenda,ukizaa na mme wa mtu usim harass mkewe na jitahidi uwe na nguvu za uchumi za kulea mwenyewe mwanao.Baba mzazi akichangia,pokea,asipoleta achana naye,ila usizuie contact na mwanae,acha mtoto amjue baba yake,na usimpige baba majungu kwa mtoto,utamharibu mtoto kisaikolojia,hasira zako zitunze kifuani mwako.
3.Vyovyote vile,UWE MWANAMKE/MWANAUME,ukijaliwa mtoto mlee,usikwepe majukumu,tabia ya kutelekeza watoto mwachie nguruwe anayezaa na kula wanae.
4.Kama wewe ni mwanaume piga ua usikubali mwanaume mwingine akulele mwanao,ni aibu.Hata kama mzazi mwenzio kaolewa wewe peleka school fees na vifaa muhimu vya mtoto.
KWA WANAUME:
Ukiona vimekuzidi,tafuta talaka,ishi mwenyewe na wanao,they are too precious to suffer kisa eti ndoa,hakuna raha duniani kama kulea watoto,asikudanganye mtu,wakishakua wakajitegemea then tafuta mwanamke wa kuzeeka naye na siku zote kumbuka hii signature ya mdau mmoja wa MMU:
Happy is a man who is a woman's 1st love and also happy is a woman who is a man's last love.
Ciao na kunradhi kwa mchango mrefu,ningeweza kuongea mengi zaidi ya haya,lakini kwa leo tuishie hapa.
Mchana mwema(Africa),asubuhi njema(America) na jioni njema(Far east)

Dah! nimekukubali sana sana sana, ngoja niprint kabisa hii niiweke kwenye file mimi nimeshachelewa ila wajukuu zangu na wanangu nitakua nawatolea copy kila mmoja.
The Following 3 Users Say Thank You to Bishanga For This Useful Post:

Asha D (Today), Dina (Today), Maty (Today)​
 
Ndio maana nikasema kama wake wawili wote wapo, there is no way mtoto akateseka. Utatesaje mtoto na mama yake yupo anakuangalia? Hata mimi nimeshaona wale ambao wamelelewa kwenye familia za wake zaidi ya mmoja, watoto wanakuwa wanapendana tu. Tena ni wengi. Jaribu kuangalia mikoa ambayo wanaoa wake wengi. Hawana shida kabisa ya watoto kuteswa. Issue unapokuwa na mke mmoja na watoto wa mwanamke zaidi ya mmoja.

Labda nitoke nje ya mada kidogo ili muweze pata picha tofauti,mambo mengi hutegemea mwanamme alivyo imara na kuwa na msimamo.Mimi baba alikuwa na wake wawili na tulikuwa tunaishi karibu na ndugu zangu wa mama mwingine,baba alikuwa anafanya kila kitu sawa kwa wake na watoto wote,tulipendana,tembeleana na ukijiskia unaenda kula au kulala nyumba ingine au wa kule nae anafanya hivyo.Kina mama walikuwa wanafatana sokoni,maharusini,misibani e.t.c naona kila kitu kinategemea mazingira anayoanda mwanamme.
 
Ngoja nisome uzoefu wa wenzangu kwani mimi pia nimo humohumo lkn sina mauzoefu jinsi ya kuhandle!
 
Ndoa hizi ambazo mmoja ana mtoto huwa zinachanganya sana wanandoa hasa yule mzazi mwenza anapoingilia, mie nashangaa huyu mwanamke aliyeachana huwa anakuwa na maisha yake na mtu mwingine , huku bado anataka amshikie mwenzake balls zake, hapa mwanamme asipokuwa makini ndoa inayumba haswa, mwanaume kuwa na mipango na mipaka na umwonyeshe mzazi mwenzako hutaki akuingilie kwenye maamuzi yako.
Kuhusu shule unaweza ukawa unalipa moja kwa moja kwenye account ya shule kuepusha usumbufu kama mwanamke anakuwa na tamaa. Mie nashangaa mwanamke utahamisha watoto wako shule nzuri sababu ya pesa kweli?

Mimi shule,medical insurance nalipa mwenyewe na soon nitaanza kwenye mambo mengine! maana longolongo kibao mara mtoto anaumwa, mara anataka nini! ilimradi tu akupe attention na utoe pesa! mwanzo niliona poa lakini baada ya kugundua hata vitu muhimu ukimpa pesa amfanyii mtoto nimebadilika mbaya!
 
Safi kabisa, Mimi wangu niliamua aende boarding tu tusikabane, asinibane nisimbane na tusibanane kuharibiana mahusiano
 
Duhh!............haya bana!

Haya bwana nini tena???Kama unataka jaribu bahati yako!!Hhheehehe!!

Mimi shule,medical insurance nalipa mwenyewe na soon nitaanza kwenye mambo mengine! maana longolongo kibao mara mtoto anaumwa, mara anataka nini! ilimradi tu akupe attention na utoe pesa! mwanzo niliona poa lakini baada ya kugundua hata vitu muhimu ukimpa pesa amfanyii mtoto nimebadilika mbaya!
Well hongera kwa kutambua situátion na kwakujitambua pia....komaa hivyo hivyo ili mradi tu mahitaji ya mtoto ufikishe!
 
Bishanga asante sana kwa kutupa udhoefu wako...nafurahi kweli nikisikia mwanaume anafurahia na kujigamba kuhusu uzao wake bila kusahau kuwapendea na kuwatimizia mahitaji yao ipasavyo!!!

Maty asante sana kwa angalizo mpendwa ila wanaume wengine ukisikia kwanini waliwakimbia waliozaa nao unaweza kulia!!Kuna wanawake wa ajabu kama ambavyo kuna wanaume wa ajabu....cha muhimu ni mtu kua mwangalifu bila kusahau mwelewa!!Kwasababu tu kashindwana na Mwajuma haina maana atashindwana na Ashura......:grouphug:
 
Duh! Sisi tuliolelewa na Mama wa Kambo(s) tunayo mengi ya kuandika - A book may be - kuhusu maisha ya kulelewa na Mama wa Kambo!

BE nasubiria kitabu hicho....nimeshatenga buku kadhaa ya kununua!!
Ila pole sana kama mambo yalikua magumu....hopefully ulishasamehe hata kama huwezi kusahau!
 
Back
Top Bottom