Lizzy ahsante kwa kufungua hii thread.Si nia yangu kujivua nguo humu MMU lakini kwa kuwa umechokoza hii mada ngoja nikupe uzoefu wangu binafsi. Kwa kifupi:
1. Nimezaa na wanawake kadhaa.
2.Nina watoto kadhaa wa kike na wa kiume.
3. Wanangu ni wakubwa,mdogo yuko sekondari ,wakubwa wanajitegemea,wa kati kati hapo wako hatua kadhaa za chuo.
4.Wengine niliwazaa ndani ya ndoa na wengine nje ya ndoa,whatever that means,kwangu mimi mtoto ni mtoto,i don't care about these social semantics.
5.Nimelea wanangu katika mazingara yote,ya kuwa ndani ya ndoa na mke akilea so called watoto wa kambo na ya mimi kuwa single father na wanangu wote.
UZOEFU WANGU:
1. So called mama wa kambo ana cope kirahisi zaidi na watoto wa kiume kuliko wa kike.
2. Utake usitake so long as mwanamke umezaa naye huyo unaye for life,atakufuatilia maisha yako binafsi mpaka siku unaingia kaburini,awe kaolewa awe hajaolewa.
3. Mwanamke ukisha zaa naye atakuwa radhi uzeeke bila kuwa na mke kuliko uoe mwanamke mwingine(hata kama yeye kaolewa).
4. Kama umeoa mkeo siku zote atakuwa suspicious na mahusiano yako na ma ex wako,hata kama wameolewa.
USHAURI:
1.Kama wewe ni kijana wa kiume jitahidi usizae kabla ya kuoa na ukishaoa kama utakuwa na hawara usizae naye.It is too expensive materially ,mentally and emotionally.
2. Kama wewe ni msichana ikiwezekana usizae na mme wa mtu,ikibidi kama unaona miaka inakwenda,ukizaa na mme wa mtu usim harass mkewe na jitahidi uwe na nguvu za uchumi za kulea mwenyewe mwanao.Baba mzazi akichangia,pokea,asipoleta achana naye,ila usizuie contact na mwanae,acha mtoto amjue baba yake,na usimpige baba majungu kwa mtoto,utamharibu mtoto kisaikolojia,hasira zako zitunze kifuani mwako.
3.Vyovyote vile,UWE MWANAMKE/MWANAUME,ukijaliwa mtoto mlee,usikwepe majukumu,tabia ya kutelekeza watoto mwachie nguruwe anayezaa na kula wanae.
4.Kama wewe ni mwanaume piga ua usikubali mwanaume mwingine akulele mwanao,ni aibu.Hata kama mzazi mwenzio kaolewa wewe peleka school fees na vifaa muhimu vya mtoto.
KWA WANAUME:
Ukiona vimekuzidi,tafuta talaka,ishi mwenyewe na wanao,they are too precious to suffer kisa eti ndoa,hakuna raha duniani kama kulea watoto,asikudanganye mtu,wakishakua wakajitegemea then tafuta mwanamke wa kuzeeka naye na siku zote kumbuka hii signature ya mdau mmoja wa MMU:
Happy is a man who is a woman's 1st love and also happy is a woman who is a man's last love.
Ciao na kunradhi kwa mchango mrefu,ningeweza kuongea mengi zaidi ya haya,lakini kwa leo tuishie hapa.
Mchana mwema(Africa),asubuhi njema(America) na jioni njema(Far east)