Wazazi Wenzangu: Kuna umuhimu (faida) gani kwa baadhi ya watoto kuwa na majina mawili? Jina la shuleni pamoja na lile la nyumbani?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu wamama na wababa wa Tanzania;

Kuna umuhimu (faida) gani kwa baadhi ya watoto kuwa na majina mawili? Jina la shuleni pamoja na lile la nyumbani?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana jana nikiwa ninatoka katika shughuli zangu niliamua kupita katika shule moja ya msingi ya boarding kumsalimia mtoto wa kaka yangu mkubwa. Huyu dogo jina lake ambalo linalijua siku zote tangia akiwa mdogo ni Immanuel na nilipofika kwa academic master nikamuulizia kwa jina hilo hilo sema nikaongeza na jina la kaka yangu (********) ila wao wakasema hawamtambui mtoto huyo. Sasa kwa kujiongeza tu ikanibidi nimpigie tena simu baba yake mzazi ili kuweza kujua huyu ndugu yangu anajulikana kwa jina lipi hapa shuleni ili niweze kumsabahi kisha niendelee na mishe zangu. Ndio hapa baba yake akasema hilo IMMANUEL ni jina lake la nyumbani lakini shuleni anajulikana kwa jina la Alexander (*******). Hapo kwenye mabano ndio jina la baba yake.

Sasa tangia hapa nikawa ninajiuliza, kuna umuhimu/faida gani kwa mzazi kumpa mtoto jina la nyumbani pamoja na shuleni?

Je, na wewe mwana JF ulikuwa na jina la nyumbani pamoja na shuleni pindi unasoma? (Sio lazima ulitaje jina lako ila unaweza ukasema tu NDIO au HAPANA)

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hayo majina mengine ni ya bibi na babu,unakuta wamekomaa kumpa mjukuu wao jina la jadi lenyemaana ya kijadi.

Kwa kuwapa heshima yao basi unakubali jina lao na wewe unampa la kwako lakizungu au kiarabu basi ndio inavyotokeaga.
 
Hayo majina mengine ni ya bibi na babu,unakuta wamekomaa kumpa mjukuu wao jina la jadi lenyemaana ya kijadi.
Kwa kuwapa heshima yao basi unakubali jina lao na wewe unampa la kwako lakizungu au kiarabu basi ndio inavyotokeaga.
Je, na wewe ulikuwa na jina la nyumbani pamoja na shuleni pindi unasoma? (Sio lazima ulitaje jina lako ila unaweza ukasema tu NDIO au HAPANA)
 
Je, na wewe mwana ulikuwa na jina la nyumbani pamoja na shuleni pindi unasoma?
Hapana ila nilibalishwa jina na sijataka kusumbuka kujua ilikuwaje maana haitaongeza kitu kwenye maisha yangu.

Kwenye cheti changu cha mwanzo kabisa cha kuzaliwa kulikuwa na jina A baadae lilikatwa na peni maana liliandwikwa kwa peni.

Alafu kwachini likaandwika jina Y.hilo jina Y ndio nililotumia shule na mpaka sasa.
 
Umewaza nini mpaka umeuliza swali kama hili mkuu? Ngoja wazazi wenzio waje kwa maana mimi sina mtoto hata wa kusingiziwa mpaka sasa.
 
Ukiachilia mbali jina la baba na la ukoo mimi nilipewa majina matatu. Moja la babu, jingine kumaanisha mimi ni kitindamimba na la tatu ndo la kikristo. Hilo la babu linafahamika kwa baba na mama pamoja na wife (aliliona kwenye birth certificate),

Ila hata kaka na dada zangu wa tumbo moja hawalifahamu. Kwa sasa la kitindamimba ndo linatumika kama first name na la kikristo kama surname.
 
Ninalo jina moja tu

Sioni umuhimu wa kuwa na jina la nyumbani na shuleni
 
Hayo majina ya nyumbani yanaitwa Ni ya kishenzi ukijaribu kumbatiza mtoto Kanisani kwa Wakristo
Kwa Waislam pia mtoto anatakiwa apewe jina la Kiarabu ndio ataonekana Muislam kamili

Lakini siku hizi naona imepungua, maana wazazi wengi wanawapa majina ya Kizungu au Kiarabu pekee, ya nyumbani yanaachwa
 
Mwanangu wa kike akiwa na miezi kadhaa akaenda kwa wazee kijijini. Akiwa kule mama yake akawa hamuiti jina lake akawa anamuita jina la kijiji chetu. Wazia awe anamuita Kilimanjaro au Mtwara, naona hii nickname imekuja kwa kasi kuliko jina Og na jina la kijiji chetu ni zuri, sijakataza asiitwe hivyo so akikua na akilikuta akiendelea nalo sioni shida.

Nje ya hapo sioni logic ya mtu mmoja kumiliki majina mengi. Kwako Don Nalimison
 
Kawaida tu, Jina la kazi ni "Mla bata", nikirudi nyumbani nina jina jingine.




Let's meet at the top, cheers πŸ₯‚
 
Moja ya vitu najutia sana ni kuwa na jina la kidini, Wanangu watakuwa na majina ya Kitanzania kama Jamhuri, Amani, Madaraka na ya asili ya babu zao Ujinga wa mtoto kuitwa Jacqueline Peter Christopher sitaki kabisa sijafika ujinga wa ivo ila pia tangu nifike secondary natumia jina la babu popote kama jina maarufu na niko proud sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…