Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.
Eti ndugu zangu wamama na wababa wa Tanzania;
Kuna umuhimu (faida) gani kwa baadhi ya watoto kuwa na majina mawili? Jina la shuleni pamoja na lile la nyumbani?
Nimeamua kuuliza hivi kwa maana jana nikiwa ninatoka katika shughuli zangu niliamua kupita katika shule moja ya msingi ya boarding kumsalimia mtoto wa kaka yangu mkubwa. Huyu dogo jina lake ambalo linalijua siku zote tangia akiwa mdogo ni Immanuel na nilipofika kwa academic master nikamuulizia kwa jina hilo hilo sema nikaongeza na jina la kaka yangu (********) ila wao wakasema hawamtambui mtoto huyo. Sasa kwa kujiongeza tu ikanibidi nimpigie tena simu baba yake mzazi ili kuweza kujua huyu ndugu yangu anajulikana kwa jina lipi hapa shuleni ili niweze kumsabahi kisha niendelee na mishe zangu. Ndio hapa baba yake akasema hilo IMMANUEL ni jina lake la nyumbani lakini shuleni anajulikana kwa jina la Alexander (*******). Hapo kwenye mabano ndio jina la baba yake.
Sasa tangia hapa nikawa ninajiuliza, kuna umuhimu/faida gani kwa mzazi kumpa mtoto jina la nyumbani pamoja na shuleni?
Je, na wewe mwana JF ulikuwa na jina la nyumbani pamoja na shuleni pindi unasoma? (Sio lazima ulitaje jina lako ila unaweza ukasema tu NDIO au HAPANA)
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.