Wazazi Wenzangu: Kuna umuhimu (faida) gani kwa baadhi ya watoto kuwa na majina mawili? Jina la shuleni pamoja na lile la nyumbani?

Hii ni mara ya kwanza kusikia mtu ana majina mawili ya kizungu na yanatumika moja nyumbani na lingine kijamii (shuleni).
Nimezoea kusikia majina ya kikabila ya asili yakitumika nyumbani zaidi, na ya kizungu yakitumika shuleni.
Sijui nia hapo ni nini kwa mfano uliotoa, ila kwa mfano wa pili ndio imezoeleka hivyo.
 
Mimi pia nina mawili la kiarabu na kinyumbani...matokeo la kinyumbani ndo limeshika kila mtu hadi kwenye mambo ya kazini ni hilo...wazee walikuwa wanaoneshana umwamba mana ndo "festi boni"
wazee walikuwa wanaoneshana umwamba
 
Mbona nikawaida tuu, la nyumbani ninaitwa Rwechungura, na shule naitwa John. Tembea uone
 
Hii system ipo sana Uhayani kama alivyocomment chief hapo juu. Unakuwa na jina la nyumbani la Kihaya halafu baadae ukibatizwa unakuwa na jina la kizungu. At last, la kubatizwa ndo linakuwa first name, la kilugha la kati halafu la baba linakuwa la mwisho. Mfano Gabriel Rugarabamu Pastory au Christina Kengonzi Salvatory. In this case, Kengonzi na Rugarabamu ni majina ya nyumbani, Gabriel na Christina ya kubatizwa. Na ni kwa sababu hii, wahaya wengi hawana majina ya ukoo maana la tatu linakuwa la baba.
 
Nina jina moja tu
Sioni umuhimu wa kuwa na jina zaidi ya moja aisee
 
Mimi nina majina mawili yanayofahamika sehemu tofauti. Jina la kwanza linafahamika nyumbani nilikozaliwa na hata mama yangu anajulikana kwa jina hilo (mama .......) . Hili la pili linajulikana na wanafamilia, nje ya nyumbani na ndio hilo lipo hata kwenye documents. Siku moja kuna rafiki yangu mmoja alitoka mjini kwenda kuzika mfanyakazi mwenzake karibu na kijijini kwetu. Akanipigia nimuelekeze namna ya kufika hadi nyumbani, maana uelekeo wa kijiji chetu anaujua alishawahi kufika siku za nyuma....mimi sikumuelekeza nilijua anatania maana kutoka pale alipokuwa hadi kwetu ni parefu kidogo. Ye kaona namzingua huyooo kafika mpaka kijijini akijua atauliza tu kwa kina XY. Kiukweli alifika hadi nyumbani ya pili kutoka kwetu ila hakufanikiwa kufika kwetu maana jina alilouliza kule halifamiki kabisa [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…