mtindo wa malezi imabadilika sana...
mfano,
wakati naishi nyumba za kupanga jirani yangu moja alikua na mtoto wa kiume anasoma chekechea....
sasa yule mtoto akirudi kutoka shule mama yake alimzoesha kumkagua alichofundishwa siku hiyo huko shuleni. Na mtoto nae, alizoea hali hiyo, na kwahivyo alikua akimsomea mama yake picha, michoro ya wanyama na vitu mbalimbali walivyo fundishwa huko shuleni, kwa ufasaha sana, na daima mama alifurahi na mtoto alifurahia sana malezi na upendo wa mama yake elimu [emoji205]
Tatizo sasa,
Baba yake akirudi, na kumuita mtoto yule kwaajili ya ukaguzi ule ule kama aloufanya mama yake, nadhani yule mtoto huwa anajawa woga, hasira iliyojaa kiburi, mithili ya nyoka mweusi aliebugudhiwa [emoji205]
ndugu zangu mtoto hua anavibreti kwa kilio kile cha hasira na sauti ya kujizuia huku akitetemeka kama kiswaswadu.
akiambiwa soma hiki ni nini, au hii picha ni ya nini, mtoto hugoma kabisa... ni kilio na kutetemeka tu.....
unajua kwanini anafanya hivyo,
anajua akisoma kwa kukosea, atapigwa na akisoma kwa usahihi atapigwa tu vilevile [emoji205]
kwahivyo amechagua best option ni kukaa kimya apigwe tu yaishe.
sasa ndio malezi gani hayo [emoji205]
Tuwalee watoto wetu kwa upendo ndrugo zango [emoji205]