Wazazi wetu:-Mgeni akiwa anakula ukimuangalia unapigwa, ukipigwa ukalia unapigwa na usipolia unapigwa

Wazazi wetu:-Mgeni akiwa anakula ukimuangalia unapigwa, ukipigwa ukalia unapigwa na usipolia unapigwa

Mimi nilikuwa na tabia ya kujificha kila nionapo mgeni/wageni; kama nipo ndani sitoki na kama nipo nje napotea mazima. Lakini ajabu nikaja kuwa 'mteule' wa kula chakula na wageni maalum. Hapa juhudi ilikuwa kunitafuta ili nile na wageni, wazee waliona ninao 'ustaarabu' niwapo mezani!!!
 
Unasema tu mkuu..
Nakumbuka wakati niko primary nilianguka kwenye bembea shuleni nikavunjika mkono na hapo nyumbani mzee alikua ananiambia kila siku nisibembee bembea za shuleni ni mbovu sikuskia.. Alivyopigiwa simu akaja kabla ya kufanya chochote akachukua kamba akanifunga mkono usioumia kwenye chuma la bembea nikawa naning'inia alinichapa vibaya mno😭😭😭..
Halafu ndo akanifungua tukaenda hospitali, ile siku nilichekwa sitakaa nisahau 😂😂😂
Acha kunipa chai jua kali loote hili🤣

Mimi sasa kuna siku tulienda kuwinda ndege, af mzee ashasemaga tusicheze na majirani, kulikua na jiran mmoja tu ndo tulikua tunaenda kucheza hapo, sasa sku hyo huyo rafiki si kapitiwa na wenzake tukafunga safari hadi maporini kuwinda, tume pambana huku na kule mpaka jioni ndo tuna pata ndege mmoja. Hapo mind yangu najua mzee kurudi usiku!

Asee nilipofika home nakuta mmfanyakazi alikua mdada kashachuma mipera ya kutosha sito sahau shoo ya sku hiyo mpk leo. Kesho yake skuli desk langu halikukalika buts zilivimba🤣
 
Nakumbuka nilivyokuwa mdogo, kuna watu walikuwa wanakuja pale nyumbani kusali na mama(walikuwa na kikundi flani hivi)

Sasa siku moja walikuja usiku tumepika wali nyama, walishtukiza tu sio kawaida yao

Wakati mama anawapakulia nikapeleka kiherehere changu huko jikoni nikaropoka 'sasa mboga itatosha kweli?'

Aisee klichofuata siwezi sahau. Hadi mwiko ulihusika....
Aisee ulikuwa una pambania haki yako isi ishe😂🤣
 
Enzi zetu za kucheza mpira barabarani, akipita mkubwa mpira unasimama, kama ndo wa mtaani anamzigo, mtaubeba kuupeleka kwake. Maana kipindi hicho mzazi yeyote ukizingua anakata fimbo ni mwendo wa njiti tu. Ukizingua zaidi unashikwa shati-kaptula 🤣🤣🤣 unakula njiti hadi kwenu na kule unapokelewa na njiti
 
Usipo lia unapigwa (unakiburi), ukilia unapigwa ili unyamanze, ukinyamanza unapigwa ( unadharau).
 
Acha kunipa chai jua kali loote hili🤣

Mimi sasa kuna siku tulienda kuwinda ndege, af mzee ashasemaga tusicheze na majirani, kulikua na jiran mmoja tu ndo tulikua tunaenda kucheza hapo, sasa sku hyo huyo rafiki si kapitiwa na wenzake tukafunga safari hadi maporini kuwinda, tume pambana huku na kule mpaka jioni ndo tuna pata ndege mmoja. Hapo mind yangu najua mzee kurudi usiku!

Asee nilipofika home nakuta mmfanyakazi alikua mdada kashachuma mipera ya kutosha sito sahau shoo ya sku hiyo mpk leo. Kesho yake skuli desk langu halikukalika buts zilivimba🤣
Mzee wako ni mjeshi??😂😂😂
 
Chakula kikitengwa kuna bakuri la baba ,huwa ndio kuna mapaja na nyama nyingi ,ole wako ukaweke mkono huko ...kichapo mpaka baba mwenyewe akupe[emoji23]

KHe 🤔🤔🤔 mlikua mkitendewa na hivi????

Kwetu ilikua watoto tunapakuliwa kwanza ndio anafuata Baba
 
Mzee wako ni mjeshi??😂😂😂
Hamna 🤣🤣,
Umesoma ID yangu nini! Ni self employee, ila balaa lake wanajeshi wakasome. Zaman tulikua tukiwa tunacheza, ukisikia tu mlio wa gari unachunguza kama ni yeye anakuja, unaruka fensi fasta kurudi nyumbani.
 
Hanna nimewaza tu kwa ukali huo atakua mwanajeshi😃
 
Nakumbuka nilivyokuwa mdogo, kuna watu walikuwa wanakuja pale nyumbani kusali na mama(walikuwa na kikundi flani hivi)

Sasa siku moja walikuja usiku tumepika wali nyama, walishtukiza tu sio kawaida yao

Wakati mama anawapakulia nikapeleka kiherehere changu huko jikoni nikaropoka 'sasa mboga itatosha kweli?'

Aisee klichofuata siwezi sahau. Hadi mwiko ulihusika....
[emoji16][emoji16]
 
Kuna jicho Moja mama alikuwa akinikata la message sent,delivered na anwered....yaani linatuma ondoka hapa dk hii....mwili unatii...ole wako usisikilize hahaaaaaaa Wacuba hoyeee
 
Mgeni akija ukamuomba Hela ,unapigwa

Mgeni akija usipo msalimia ,unapigwa

Ukipigwa ukawa haulii ,unapigwa maana unaonekana sugu [emoji23]

Chakula kikitengwa mezani ukaanza kunawa kabla ya wakubwa ...unapigwa

Mgeni akija ukaanza kumlilia uondoke nae ..Unapigwa

Chakula kikitengwa kuna bakuri la baba ,huwa ndio kuna mapaja na nyama nyingi ,ole wako ukaweke mkono huko ...kichapo mpaka baba mwenyewe akupe[emoji23]

Baba akija nyumbani akakuta umekaa kiboya sebuleni ..unapigwa Bila hata sababu..

Ukitumwa dukani ukachelewa ..fimbo ..

Kwenye kabati huwa kuna vyombo vya kutumia siku wageni wakija tu ,siku mama akikuta unatumia hizo sahani au vikombe wakati Hakuna mgeni ..utapigwa fimbo na ngumi juu ,usipokimbia shauri yako

Hawa watoto WA siku hizi wanapelekwa hadi Shule aiseee ...Sisi tunaenda Shule wenyewe na njia tunayopita asubuhi kuna mbwa hatari ,kama huna mbio imekula kwako..na Hakuna njia nyingine [emoji28]
[emoji16][emoji16]
 
mtindo wa malezi imabadilika sana...

mfano,
wakati naishi nyumba za kupanga jirani yangu moja alikua na mtoto wa kiume anasoma chekechea....

sasa yule mtoto akirudi kutoka shule mama yake alimzoesha kumkagua alichofundishwa siku hiyo huko shuleni. Na mtoto nae, alizoea hali hiyo, na kwahivyo alikua akimsomea mama yake picha, michoro ya wanyama na vitu mbalimbali walivyo fundishwa huko shuleni, kwa ufasaha sana, na daima mama alifurahi na mtoto alifurahia sana malezi na upendo wa mama yake elimu [emoji205]

Tatizo sasa,
Baba yake akirudi, na kumuita mtoto yule kwaajili ya ukaguzi ule ule kama aloufanya mama yake, nadhani yule mtoto huwa anajawa woga, hasira iliyojaa kiburi, mithili ya nyoka mweusi aliebugudhiwa [emoji205]

ndugu zangu mtoto hua anavibreti kwa kilio kile cha hasira na sauti ya kujizuia huku akitetemeka kama kiswaswadu.

akiambiwa soma hiki ni nini, au hii picha ni ya nini, mtoto hugoma kabisa... ni kilio na kutetemeka tu.....

unajua kwanini anafanya hivyo,
anajua akisoma kwa kukosea, atapigwa na akisoma kwa usahihi atapigwa tu vilevile [emoji205]

kwahivyo amechagua best option ni kukaa kimya apigwe tu yaishe.
sasa ndio malezi gani hayo [emoji205]

Tuwalee watoto wetu kwa upendo ndrugo zango [emoji205]
Weeee mtoto asinyimwe fimbo sema ziwe kiasi Kwa ngozi nyeusi Tena Tz zinasaidia mno...
 
Back
Top Bottom