Wazazi wote piteni hapa (miaka 20 ya maumivu)

I guess I'll have to watch that, uliichekia wapi naona moviebox haimo
 
Pole kwa kutengana na baby mama wako mkuu, na hongera kwa kuweka nia ya kuwa baba bora kwa wanao.
Usisahau pia kuwaona uso kwa uso kadri utakavyoweza, toka nao out, wanunulie ice cream, cheza nao etc ili wabaki na kumbukumbu nzuri kukuhusu wewe.
 
Asante Elevenn en kwa bandiko zuri
Nowadays unazidi ku glow kwenye mabandiko yako

Hii issue ya wazazi kuonesha upendo kwa watoto ni kizungumkuti

Kwa sababu mzazi mwenyewe hakupewa upendo wa kutosha kwenye makuzi yake na hakupata ushauri nasaha akapona

Mf: Mama angu mzazi alikua mkali kupitiliza saiv kapunguza kwa sababu ya umri

Unadhani ataweza kutoa upendo kwa kiwango gani kwa mtoto?

Utasikia mzazi anasema, Mi nilikuwa napigwa na kijinga cha moto, alama hii hapa (ishara kwamba ana uchungu hajasahau &hajapona)

Anaona kukalipia bila mipaka, kutotoa muda wa kutosha kwa mtoto ni swala la kawaida kwa sababu hata hakupewa

Mzazi kama huyu hawezi kutoa upendo wa kutosha au muda kwa mtoto kwa sababu yeye hana mfano wa hilo

Lakini kwa sasa hivi kuna vitu tunafanya wala sio kwamba tulifundishwa nyumbani

Vingine tumejifunza wenyewe, kama wewe hapo ulivyogundua kwamba hukupewa muda wa kutosha na upendo

Sasa kwa wewe kugundua hilo ni kuanza kujiponya mwenyewe na fix kwa watoto wako yale mambo uliyokosa utotoni upendo, muda na nk....

Kwanzia kwako sasa kinaanza kutengenezwa kizazi kipya chenye history nzuri, huku kile kizazi chenye mtazamo hasi kuhusu muda na upendo kikizikwa

Sorry kwa kuchelewa kuja kuchangia, mdogo wangu, mambo yalikuwa mengi. 🙏🙏
 
Mkuu, pole kwa uliyopitia na asante sana kwa point hii muhimu. Hata wale wanaohalalisha watoto kuchapwa fimbo nyingi utasikia wanasema" sisi enzi zetu tulichapwa sana fimbo 30". Yaani mimi huwa nashangaa, kama wewe uliumizwa na walimu na watoto wetu ndo waumizwe na walimu??? Tukimaliza kuongelea wazazi na hili suala la walimu kuwapa trauma wanafunzi ni janga lingine hapa nchini.
 
Kungekuwa na watz hata laki moja Tz wenye mentality kama yako tungekuwa na taifa bora sana..

You're so kind, so informative, so responsibke na unachuka muda kuelewesha watu waliopotea.

Na huu uzi unazidi kutuongezea nyama. Thanks for that
 
Walimu wana reflect malezi ya familia zilizopo kwenye jamii, mwalimu asiye na trauma hawezi kumchapa mtoto fimbo ishirini,
Kila nikikumbuka idadi ya fimbo ambazo nimeshapigwa sekondari na wale walimu kwa makosa ambayo ni ya kumuelekeza mtoto napata hasira sana
 
Mara nyingi watoto hawahitaji wazazi wakamilifu, wanahitaji wazazi wanaowasikiliza, wanaowaelewa na wanaowapa usalama wa kihisia. Maumivu ambayo hayashughulikiwi yanaweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Kuvunja mzunguko huo ni zawadi kubwa ambayo mzazi anaweza kumpa mtoto wake.

ile Id ya Gemini nayo ni yako ?
 
Mkuu, pole kwa uliyopitia
Shukran sana nimewahi kuweka kisa humu
Jinsi nilivyo safiri kutoka lilongwe hadi dar bila pesa kwa sababu nilipoteza nauli na niliogopa kumwambia mama kua nimepoteza nauli kwa jinsi alivyokua mkali sana baba angu yeye alikua mpole mnoo😊
Hili la waalimu kuchapa watoto kupitiliza lime leta madhara mpka kupelekea vifo kwa wanafunzi
 
Kabisa fimbo 20 za nini mtoto kawa mwizi?
 
Inasikitisha sana
 
Word.. ✍️
 
Sio walimu tu,now kama una mtoto au upo karibu na mtoto na unampenda unaweza kugundua kwa kiasi gani tumekua abused as kids na wazazi,.kupigwa,kufokewa na mambo kama hayo..

Just reflect how you want to treat mtoto wako na how you was treated as a kid utaona gape kubwa sana wazazi wetu walimiss vitu vingi,.
 
Kungekuwa na watz hata laki moja Tz wenye mentality kama yako tungekuwa na taifa bora sana..

You're so kind, so informative, so responsibke na unachuka muda kuelewesha watu waliopotea.

Na huu uzi unazidi kutuongezea nyama. Thanks for that
Asante mkuu, tuseme nina karama ya kugusa maisha ya wengine, kuwatia moyo na kuwaponya kwa maneno ya faraja. Nashukuru Mungu kupitia mimi kuna watu wamepona hata wale waliokuwa wamekata tamaa kwa maneno ya kuumizwa walioambiwa na watu wao wa karibu.
 
Umemaliza vyote mkuu, kwenye jamii yetu abuse inachukuliwa kama ndio malezi,tunakuwa na watoto wenye matatizo mengi sana ya kisaikolojia kisa malezi mabaya . Malezi mazuri inachukuliwa kama kumdekeza au kumharibu mtoto.
 
Umemaliza vyote mkuu, kwenye jamii yetu abuse inachukuliwa kama ndio malezi,tunakuwa na watoto wenye matatizo mengi sana ya kisaikolojia kisa malezi mabaya . Malezi mazuri inachukuliwa kama kumdekeza au kumharibu mtoto.
Kumdekeza ndo lugha za wazazi wetu walitumia ila hawakujua kubalance walipitiliza
 
Hakika mkuu🤝.
 
Yes, love above all else. Wengi hukimbia ku invest elimu, mahitaji, sijui mtoto analindwa kama dhahabu...
Ila nakwambia akijiona less tu, hayo yote hayana maana tena.

That's exactly what happened to me... I didn't know which value I had, I couldn't figure out my reason to be here..

I chased it kila mahala hadi spiritualism niliingia na huko bado huku kunipa jibu.
 
Sio sawa kabisa, nilishapigwa fimbo zaidi ya ishirini matakoni, matako yalivimba yakawa kama ukuni nilikua nakaa upande kwenye kiti kwa wiki mbili, worse enough sikuwa na wa kumwambia sio walimu wengine hata wazazi nyumbani
😂😂😂 si bora wewe,wengine walionisababishia kipindi hicho walivyosikia nimepinda kweli hawatamani hata kunisikia(haiwezekani kwa mfano umsingizie mtu ameua halafu akahukumiwa then baada ya hukumu unamkuta au kusikia yule malehemu na mashahidi wake wanakula bata)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…