Asante sana pia kwa post nzuri, inatia moyo na kufundisha pia namna ya kuishiMkuu kwanza pongezi kwa kuwa mkweli na kusema mapito yako hapa..
Nikwambie hiyo inaitwa PTSD yaani post traumatic stress... Yule mtesi wako anakuwa kashaondoka ila bado emotional body inakuwa na Maumivu.. So hata ufanyaje kwa kutumia akilli mwili unakataa
Cha kukushauri kama hauna pesa ya therapy, anza kuwa mkweli... Usimwambie yeye kwanza anza kuwaambia watu wa karibu wenye ukaribu na wewe... Sharing helps alot, ndo kitu nacho penda kuitumia sana...
Kubadilika au hiyo hali kuondoka inaweza kuchukua muda sana, ila inabidi tu uwe mkweli kama ulivyo share nasi experience yako leo.
Usitake mtu aelewe sana ila ajue tu kuwa ulicho pitia kili kuharibu sana.. Na ile yey kujua tu kuna leta confirmation ndani yako, pia watu watakua similar stories na kukufanya usijihisi mnyonge tena.
Best wishes mkuu. Utakuwa sawa tu..
Daah aisee unaona sasa mkuuPole mkuu,. My blood sister alipokua mdogo hata hajaanza shule alichukuliwa na ndugu yetu akaishi nae huyo mama aliemchukua mtu mkubwa sana kiuchumi,fame and all,sister akapelekwa shule nzuri,
Me nakua sister anakuja home kila likizo kama mgeni,mazingira ya home hayawezi vyakula sio vya kitajiri kama alipokulia,but kila December anakuja home,ana nguo mabegi 10 anagawa Kwa kila mtoto wa jirani,.maisha bora right?mama mkubwa wetu hanaga roho mbaya,sister hatukuhisi kama alikosa kitu..
Two years ago nipo na mama na sister sebuleni sister tayari ana watoto,anamuuliza mama kwa uchungu "Hivi mlikua na akili gani kunitelekeza mtoto ugenini???nyie wazazi bure kabisa sababu hakuna namna itakayofanya nimuache mtoto wangu kwa mtu mwingine,na nitawalaumu kwa dhambi yenu siku zote"
Pole sana you are soo strongHuyu kupona ni kwa neema ya Mungu, kwa niliyoyapitia kwenye ndoa kwa sasa my focus ni Mimi kupona na kumchukulia kama alivyo...kikubwa nimeweka strong boundaries kwa ajili ya kujilinda Mimi na watoto.
Imagine mtu aliyezaliwa na Baba aliyelelewa na mama wa kambo, yeye pia akalelewa na mama wa kambo......hadi kufikia miaka yote hii ya ndoa najiona shujaa as nimekata Hiyo generational curse ya watoto kulelewa na wazazi wa kambo au bila malezi ya mzazi mmoja katika umri mdogo, though I did a very hardwork jamani.
I'll have to check on those too.. Thanks mkuuHali halisi hiyo ndio maana mimi sio shabiki wa Mawaidha potovu,siwezi kuhukumu sababu kila mtu Ana story amepitia na kushape tabia yake,so kuliko kuhukumu,kuhubiri negativity ku point finger ni vyema kujifunza na kuambukizana Positivity na kupeana moyo for the good cause..
Kuna kitabu nimesoma kinaitwa SMALL FRY kimeandikwa na Lisa mtoto wa Steve Jobs,.
Anaeleza kwa nini Steve Jobs pamoja na kua multi bilionea lakini alikua hampendi binti yake waziwazi,computer ya kwanza ya Apple iliitwa Lisa after her name,.you know why nimesoma hicho kitabu?sababu nilimchukia sana Steve Job alivyokua anamtendea binti yake katika documentary JOBS..
Kumbe Steve Jobs katika umri mdogo kabisa alikua adopted hakuwahi kujua his biological parents,Hali hiyo imemfanya(anaongea doctor wa Steve Jobs) awe na deep seated fear of abandonment and rejection..kwahiyo Steve hajawahi kumpenda mtu angalia movie yake ndio utajua jamaa kiasi gani alikua EVIL
Na tatizo hilo linawapata watoto ambao wanakulia vituo vya yatima or adopted..
Hakika it's part of the game...controlUpande dhaifu daima hupenda kulisha sumu kwa watoto, wakiamini atakuwa na mshirika wa kuunganisha naye nguvu dhidi ya upande unaaonekana strong pasipo kujua damage ya hiyo sumu wanayolisha watoto.
Na bahati mbaya elimi yetu haina mtaala unaozungumzia juu ya malezi na ndoa. Ili kila upande ujue Do's na Dont's katika malezi. Hii ni kwasababu hatima ya maisha na uhai wa Taifa unategemea kwa kiasi kikubwa sana juu ya kizazi kinachoandaliwa
Mimi nimemwelewa sana anaangalia future ya watoto wake ndo maana ana tolerance.Mkuu,kupona ni neema ya Mungu nakubali lakini lazima jitihada zifanyike. Hata wewe ukiumwa lazima utaenda hospital huku ukitegemea neema ya Mungu ya uponyaji ikushukie upone. Kauli za " namchukulia kama alivyo" ni kukubali kubeba maumivu ambayo hautakiwi kuyabeba.
Pia issue sio tu watoto wamelelewa na wazazi halisi, quality ya malezi pia ipoje? Mtu anaweza kulelewa na mzazi wake na bado huyo mzazi akamhamishia trauma kwa kuwa hajapona. Siishi na wewe ila nahofu, what if watoto wenu kuna siku waliwahi hata kuhisi kwamba baba yao anakufanyia wewe mama kitu chochote kisichofaa eg kukufokea?. Una uhakika watoto wenu hawajawahi kuona baba yao anakufanyia wewe mama kitu kibaya ?. Kuna couple fulani nilikuwa naipenda sana nikiwa mtoto, siku moja tukiwa Kanisani nikashuhudiaa mume anamnyooshea mkewe kidole kama anamkaripia fulani hivi, lile tukio liliniumiza sana . Watoto wako je hawajawahi kushuhudia tukio kama hilo?
Mwisho wewe kama mama, afya yako ya akili inatakiwa kulindwa maana wewe ndo moyo wa nyumba. Sio sahihi kuendelea kuumizwa na mtu ambaye hajapona, moyo wa nyumba ukiumia nyumba nzima lazima ihisi maumivu. Jiulize, je haijawahi kutokea hata siku moja kuwatendea watoto wako isivyo kwa sababu ya yaliyojiri kati yako na mumeo???.