Wazazi wote piteni hapa (miaka 20 ya maumivu)

Wazazi wote piteni hapa (miaka 20 ya maumivu)

Kama mzazi najifunza sanaaa kupitia haya mambo...nina vijana napata picha na mwanga wa jinsi naweza kuwapa aina fulani ya malezi kwao...japo sio asilimia mia kucopy but kuna some information tunazipata na zinajenga sana
Wishing you luck na malezi yaliyo bora
 
Screenshot_20260810_121859.jpg


Mkuu lost files naona bado hawaja upload na ku stream kwangu huwa naona Kuna distraction nyingi..
 
Siku nimesikia Steve Jobs ni mwarabu kutoka Syria nilishangaa, kumbe alikuwa adopted.
Ongezea Genius ila binadamu mshenzi kupata kutokea,jana tu nilikua nasoma habari za Steve Wozniak alipowapa wafanyakazi wa kwanza wa apple Share zake zote sababu Jobs aliwadhulumu,.na Steve Jobs mwenyewe aliwahi kukiri maisha yake ya utoto yameathiri kiasi kikubwa sana mahusiano yake na watu,na binti yake,.

Alimwambia binti yake "Nisamehe I’m not cruel I’m just not kind,You can’t make me love you because I’m poorly made"
 
Yes ndio hiyo kwenye Cover juu,.Movie Box documentaries nyingi hawana,.hapo njia nzuri ambayo ita work out for you 100% Shusha torrent tu..
Naomba torrent site inayo faa nyingi zinasumbua
 
Juzi kati baada ya kusoma bandiko la mlevi min -me la kuhusu bintiye na kukosa upendo kwa mama yake, ambaye Wali kuwa separated na kumfanya min kuwa single father, so mtoto kukosa motherly presence ila fanya amchukie..

actually, ile issue ilinifanya nijione ndani yake.

Why..?

Kwa sababu scenario hiyo ilinifanya nibebe maumivu kwa takriban miaka 20, ya maumivu, na kuanza kuona kuwa ili stem from family issues..

Sitaki kueleza stori yangu, because Nitakuwa nafanya repetition na ni ndefu sana.. Ila ukweli useme ya kuwa...

Zawadi pekee na bora utakayo mpa mtoto wako ni kumfanya ajihisi anatosha, anapendwa, anaweza, na ana deserve kile anataka kutimiza... Ili mradi kiwe na manufaa both kwake na jamii inayo mzunguka.

Binadamu yuko so hardwired kwa ajili ya connection(ukaribu na watu au jamii imzungukayo)... Ila hii huwa inakaziwa sana akiwa bado yu mtoto. Yaani mwaka wa kwanza hadi wa 7.. Na Aristotle alishawahi kuliweka wazi hilo...
View attachment 3646873

Ila bado hiyo sio kigezo mtoto yaani akiwa under 18 bado hajapevuka both psychological and emotional...

Ngoja niwape siri wazazi, wengi hupenda kudhani kuwa trauma and depression inatokea pale unapo mwdhibu mtoto au kumnyima mahitaji, la hasha.. Mtoto huumia zaidi pale Atakapo achwa kusikiliza, atapo nyimwa uhuru, atakapo fanyiwa kujiona hafai...

Ubaya ni kuwa mtu akiumizwa na trauma, ku reverse au kupona juea ni almost impossible... Maana ile crack inaenda deep na inaficha na shade aspect...

Unashangaa mtoto ana zamia madawa ya kule ya, ushoga, umalaya, kuvuta ganja, anakuwa mtu mwenye hasira, aside shaurika.... Inshort ni kuwa hii demage hata yeye mwenyewe hawezi kuitrack... Na ata akijaribu huwa anaishia kupata maumivu kwa sababu reality ya ndani inakuwa tayari imesha kuwa ngumu kubadilika.

Binafsi niliingia katika uraibu mbaya sana wa porno graphics... Mimi ni soo sensitive person, na as I said before malezi kidogo ilikuwa changamoto. Sikupata ile fatherly love ya kunikanya vyema, soo nikawa soo reserved, badala ya kufuata stimu za nje kama pombe(japo nilijaribu ila sikuipenda), wala kufatilia mademu(nilitokea kuwachukia kwa sababu ya kuishi na step mother.. Alinifanya niwachukie wanawake).. So basically nilikuwa exposed kingono at a very young age. Kufupisha stori kwa sababu ya hate na insecurity nilokuwa nayo kwa wanawake sikupendelea sana kuwa kwenye mahusiano. Niliingiwa kwenye uraibu wa sheria mkononi. Na kwa kuwa huwa nina sensitivity kubwa haikuwa shida kwangu kufika climax.

Na hiyo ni just one aspect ya madhara ya childhood wounds.. Ila nikianza kueleza how deep this rabbit hole goes. Itabidi niweke iwe series.. Ila ni kuwa matokeo ya maumivu ya utotoni hubadilisha world view ya mtoto akuwapo mtu mzima. Na tena hawezi kutambua maana inaingia kwenye operating system yake, anaishi na kuona dunia kupitia lens ya hayo maumivu.

Wazazi mlio na watoto wadogo, nawaomba sana mzingatie kidogo nilicho andika... Muhimu ni kuwa mtoto akiwa na shida hasa ya mahusiano na nyie kama wazazi angalieni na mtoe msaada wa kihisia mapema iwezekanavyo, wakubwa mtoto alisha pita umri wa labda miaka 15 hvi huwa ni kama haiwezekani tena kurudi.

Kuna hii tabia ya wazazi kuwafanya watoto wabebe msalaba yao, yaani just because alipitia maisha flani, basi anasambza hiyo trauma kwa wanawe ili nao wawasambazie watoto wao.

Tuache huu ujinga, ni waambie tu ya kuwa ukifanya upendo na kutosambaza hiyo trauma uliyo nayo... Kwa kiasi kikubwa Uta heal pia japo itakuwa soo gradual ila utaona mabadiliko pia.

Mimi sio mtaalamu wa kisaikolojia ila hata hii industry kwa huku kwetu imekaa kiupigaji tu, hawajui chochote ila kumezeshwa tu vitu visivyo akisi uhalisia. Wazazi ndo mnajua watoto wenu vizuri, jitahidini kuwa mwanga kwa kizazi kijacho, acheni kufanya vitu kwa mihemko na kukua ego zenu. Ni ujinga na ushamba, which mtoto wako akikuwa atakuchukia na utakufa vibaya tu

Mabadiliko ya naanza na wewe mwenyewe sio mzazi tu hata wewe dada, kaka, mjomba, shangazi... Do good to these innocent souls...

Nawishi huu ujumbe ueleweke watu wasirudie nilicho pitia kwa miaka 20.

In peace and light..

de Gunner

binti kiziwi Tsh Mshana Jr mshamba_hachekwi ShesRise_1 Binti wa zamani Me and me Yoda Joanah
Upande dhaifu daima hupenda kulisha sumu kwa watoto, wakiamini atakuwa na mshirika wa kuunganisha naye nguvu dhidi ya upande unaaonekana strong pasipo kujua damage ya hiyo sumu wanayolisha watoto.

Na bahati mbaya elimi yetu haina mtaala unaozungumzia juu ya malezi na ndoa. Ili kila upande ujue Do's na Dont's katika malezi. Hii ni kwasababu hatima ya maisha na uhai wa Taifa unategemea kwa kiasi kikubwa sana juu ya kizazi kinachoandaliwa
 
That's being judgemental

Kwanini hukuniuliza hata privately, kwa nini nimeweka hiyo avatar.. Ukaja publicly tena in a way watu wajue nimefanya kitu kibaya?

That's a chain we were talking about being triggered.. Na huu ndo ukweli.. People attack what they don't understand.

Kwa hili lazima niwe muwazi tu, sio kupwpesha macho na kuongea kwa hulka
Sorry 🙏 hutoona again ✔️
 
Sorry 🙏 hutoona again ✔️
There's no need of being sorry, we're all trying to make one another understand. Being judgemental sometimes haisaidii.

Infact I've learned so much from you, ila Kuna muda tunafanya judgements personal which ain't good
 
Upande dhaifu daima hupenda kulisha sumu kwa watoto, wakiamini atakuwa na mshirika wa kuunganisha naye nguvu dhidi ya upande unaaonekana strong pasipo kujua damage ya hiyo sumu wanayolisha watoto.

Na bahati mbaya elimi yetu haina mtaala unaozungumzia juu ya malezi na ndoa. Ili kila upande ujue Do's na Dont's katika malezi. Hii ni kwasababu hatima ya maisha na uhai wa Taifa unategemea kwa kiasi kikubwa sana juu ya kizazi kinachoandaliwa
Kitendo cha huo upande dhaifu kutaka kuunganisha nguvu ni dalili ya tatizo la kisaikolojia ambalo lisipotatuliwa vizazi vijavyo vinarithishwa maumivu tunayoyaongelea hapa. Wazazi wapone ili madhara yasiende kizazi kinachofuata.
 
"Feeling kama mama ake amemkumbatia" , hii kauli imenitoa machozi mkuu, nimevuta picha kama mwamba namuona huyu hapa anatafuta mtu wa kumkumbatia halafu hayupo.
Wanaume nao pia wana hisia ,wanahitaji mtu wa kuwakumbatia, wanahitaji bega la kuegemea na wanahitaji mtu wa kuwaruhusu watoe machozi bila kuhisi wanadharaurika au wanapoteza uanaume wao. Lakini wengi hawapati hizo nafasi angalau kwa dakika kadhaa waonyeshe kuumizwa maana wanaogopa watadharaurika. Matokeo wanaotafuta faraja sehemu zisizofaa mfano huyo mraibu wa cocaine.
Hakika and am one among them..

Zamani nilidhani kuongelea maumivu inaonesha unyonge... Hasa hasa wakisha jua kuwa nilimfanyia hivi au vile

Ni sawa na kujivua nguo... Unaogopa wata ku bully.. Na shuleni ndo hasaaa watu tulikuwa tunakaa na maumivu hata tusielewe darasani

My school life did go to waste kabisa.. I am who I am by reparenting and educating myself.
 
Umesahau wanatafuta watoto ili kuridhisha jamii, kuwa wao sio wagumba na Tasa.
Hili ndio lengo kuu haswaa.
Ndio nimeweka hapo kama n.k. Utasikia, "umri unakwenda zaa hata mtoto mmoja", kana kwamba huyo mtoto ni wa majaribio🙆‍♂️🙆‍♂️

Uduwanzi haswa, unaridhisha watu ambao hawana impact yoyote kwenye maisha yako. Na ni hao hao ukishindwa kulea watakushangaa pia ulizaa ili iweje! Kama haitoshi na majina ya ajabu yote uitaitwa🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Ndio nimeweka hapo kama n.k. Utasikia, "umri unakwenda zaa hata mtoto mmoja", kana kwamba huyo mtoto ni wa majaribio🙆‍♂️🙆‍♂️

Uduwanzi haswa, unaridhisha watu ambao hawana impact yoyote kwenye maisha yako. Na ni hao hao ukishindwa kulea watakushangaa pia ulizaa ili iweje! Kama haitoshi na majina ya ajabu yote uitaitwa🙆‍♂️🙆‍♂️
Na ukizaa ukashindwa ku Lea wanakwambia unaona mtoto amekuwa kama wewe.

Daaahh ila wamatumbi bwana
 
Back
Top Bottom