Wazee kuna jamaa yangu kaanzisha biashara, kila wiki anataka nimuungishe, imekuwa kero!

Mimi kuna mmoja huyo hua analeta maziwa mtindi na madumu ya lita 5 ofisini uwe umeagiza au hukuagiza atakupigia simu na usipopokea anaacha dumu hapo ofisini utajua mwenyewe. Na baada ya hapo ni simu zisizo na idadi kudai malipo.
 
stategies nzuri katika ku maintain reliable customer wako kwenye biashara kiujumla.


nilichojifunza makosa ni pale unapofungua biashara bila kujua status ya customer segment yako unayo ilenga vizuri tofauti na kujiamulia tu. na hii mara nyingi hupelekea biashara nyingi kifa kiujumla.

na fkiri ni vyema kuepusha kuleta mazoea na kujuana kwenye biashara na tujifunze kufanya bishara mbali na watu tunao Juana nao husaidia kukua kiujumla na kujitanua ndani ya muda pakiwa na uvumilivu kwenye biashara
 
Tatizo mnawaendekeza wenyewe.

Kwani kumwambia mtu sitaki, bajeti hainiruhusu, au sijaipenda bidhaa hivyo kuna shida gani?

Kuna unafiki fulani katika jamii hii.
 
Kwani huwezi kumkatalia?
 
Akija umkopeshe hiyo elfu 5 utampa?

Ongea nae tu mwambie si kila siku utahitaji, au ukihitaji utakuwa unamwambia kuliko kujiamulia mamboโ€ฆ

Kujiajiri kazi nyie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ