Wazee kuna jamaa yangu kaanzisha biashara, kila wiki anataka nimuungishe, imekuwa kero!

Wazee kuna jamaa yangu kaanzisha biashara, kila wiki anataka nimuungishe, imekuwa kero!

Wakuu,

Jamani mkianzisha biashara muwe mnaangalia na wateja,

Kuna mwanangu kaanzisha biashara ya smoothies na juice. Alivyoanza biashara yake kiuana nikawa naenda kununua, nikitoka ofisini ntapitia ntanunua hata smoothies mbili nitaondoka

Sasa sijui jamaa kaona dezo, yaani kila baada ya siku tatu ananipigia anataka nimuungishe. Yaani kila Ijumaa na Jumatatu atakutafuta Whatsap anataka uagize juice akufanyie delivery

Na kuna muda anakwambia kabisa nimeshakuandalia kabisa namtuma boda akuletee, yaani hapo kantafuta yeye aniletee.

Nafanyaje wakuu maana imekuwa too much hizo smoothies ni 5,000
Wewe ni me au ke? Yaani unashindwa kukataa na kumwambia kuwa ukiwa na uhitaji utamwambia au utapitia. Hili nalo na kuomba ushauri????
 
Tatizo mnawaendekeza wenyewe.

Kwani kumwambia mtu sitaki, bajeti hainiruhusu, au sijaipenda bidhaa hivyo kuna shida gani?

Kuna unafiki fulani katika jamii hii.
Huwa namwambia bajeti hairuhusu na bado nliyonayo haijaisha. Anafosi mnunulie hata wifi au marafiki zako.
 
Huwa namwambia bajeti hairuhusu na bado nliyonayo haijaisha. Anafosi mnunulie hata wifi au marafiki zako.
Watu kama hao hujawaonesha show ya kibabe bado ndiyo tatizo.

Wabonho ndiyo maana bi mkubwa kawasema warahimu sana.

Yani pesa yako mwenyewe mtu baki anakunyenga mpaka unakuja kumsemea JF, what are you, a child?
 
Nimetoa mfano hai mkuu sijaja kumsemea kwa sababu nilishaamua sinunui tena.
 
Mimi nilichoka kumuunga huyu binti biashara yake kila usiku, nikaona nihame mkoa tu...😳View attachment 3665493
Vitu vitamu kabisa mzee wangu
f61a3b349bef3d9e49acdec35117149b.jpg
 
Hapo ndipo huwa nawavulia kofia mademu.

Hata muwe washikaji vipi au umemsaidia namna gani,ukitaka chiu yake anakuruka mita mia.😀

Yaani uso mkavu kabisa anakuambia NO,SITAKI,SIKUPI.
 
Watu kama hao hujawaonesha show ya kibabe bado ndiyo tatizo.

Wabonho ndiyo maana bi mkubwa kawasema warahimu sana.

Yani pesa yako mwenyewe mtu baki anakunyenga mpaka unakuja kumsemea JF, what are you, a child?
Kuna watu hamjui kuwa kukataa kununua una shusha brand yako
 
Ni wazi kuwa hiyo biashara bado haijasimama, analazimisha walau auze kwako.
 
Nimetoa mfano hai mkuu sijaja kumsemea kwa sababu nilishaamua sinunui tena.
Kwa hiyo hapa ni kama unaelimisha jamii kwamba kuna wanaume wamepigwa na wake zao sio?

Matatizo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu tuyatatue wenyewe, hapa tuje na yanayohitaji msaada.

Othetwise labda kama unataka kupiga umbea tu.
 
Mwambie tu kiungwana kuwa asipate shida kukutafuta siku ukihitaji utakwenda kununua.
 
Bonda raha mkuu, mie nimeuza nyumba saizi nashinda Bar 24/7...😜
Kitakacho ni maliza ni hawa viumbe hakianani😁 mkuu hivi pisi kama ile unaacha salama kabisa? Aisee huyu Mungu huyu
 
Wewe ni me au ke? Yaani unashindwa kukataa na kumwambia kuwa ukiwa na uhitaji utamwambia au utapitia. Hili nalo na kuomba ushauri????

Ni Me, njoo nikuprove!
 
Back
Top Bottom