Wazee na Vijana wa Yanga acheni ujinga, nendeni mkajitafutie vipato

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Kila siku matamko na vigenge kwamba hamtaleta timu siku mechi ya derby ikipangwa. Mnafanya kazi saa ngapi?

Viongozi wenu wameshachukua hatua, wameshatoa matamko, wameshapeleka barua Bodi, TFF na huko CAS. Acheni hizo hatua na malalamiko yafanyiwe kazi na maamuzi yatatoka.

Hao wanaowachochea wapo kwenye maofisi na makampuni yao wanatafuta hela. Wewe wiki nzima unatokwa povu jua kali.

Wazee wa Yanga nendeni mkatafute vipato. Wazee wenzenu wa Yanga wenye nafasi na makampuni, hutawaona kwenye hivyo vijiwe. Hata vijana pia kina Vincenzo Jr huwezi kuwaona kwenye huo ujinga wa maandamano. Kwa nini wewe utumike?

Unaacha familia yako badala ya kwenda kusaka noti unaenda makao makuu Yanga kupiga domo. Halafu baada ya hapo unapiga simu kuomba hela. Acha kutumika
 

na wewe km mzee au kijana tafuta riziki achana na wazee na vijana wa yanga pengine wenzio wanajiweza
 
Aliewamezesha sumu ya usimba na uyanga watz amewaweza sana. Linapokuja suala la Simba na Yanga watu akili wanaziweka pemben hapo kichwa inabaki empty.
Juzi ilikuwa zamu ya yule mvuta feg, alita waandishi akatoa kauli zake, Jana ilikuwa zamu ya wazee na vijana. Tunasubiri Leo tuone itakuwa zamu ya akina nani.

Kule upande wa pili klabu ilitoa kauli moja tu kuwa hatuchez mechi na wakatoa mapendekezo yao wakatulia.
 
Mbona kama unateseka!
 
Wanasema hizi timu zimebeba maisha ya watu mjini eti,,
 
Na bado mpaka mseme
 
Simba na Yanga ni timu za Ccm zinazotumika kuwapumbaza wananchi.

Haiwezekani timu zina zaidi ya miaka 80 zikawa zinashindwa kuwa hata viwanja vyao the same Ccm
Wanatumia viwanja vya CCM miaka kwa miaka. Hizi timu kuna wakati zinakera. Halafu ukifuatilia wapiga kelele wengi kwa kisingizio cha ushabiki, wa hizi timu ni walalahoi. Akina Hersi na Mo Dewji wanaendelea kupiga pesa kwenye vitega uchumi vyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…