Wazee nahisi kuna mtu amenicheza, nikipata hela hazikai

Wazee nahisi kuna mtu amenicheza, nikipata hela hazikai

Mule mule ni pombe na mademu na kampani nakuwaga nayo ile mna toka alafu mnachanga kama mob ya watu 3 hivi alafu hapo kuna wale washkaji ambao hawana mchongo wa kueleweka ila wanaotea madili mara mojamoja sana.

Sasa unakuta siku hiyo mdau kaotea kama 30,000 hivi sasa sababu mara nyingi unampa bia zako, hiyo siku akipata kama hivi za kuotea nae anajishtukia anakushtua sasa mnapga vinywaji Kwa hiyo 30,000 yake ya mchongo.

Yake ikiisha unakuta kichwa bado hakijalewa sana na ndiyo tunasema ngoja kibunda kikitoka nitamshtua mbona yeye ana hela za kuotea ila ananishtua.

Hiyo siku kibunda kimetokea unamshtua mdauu huku ushapanga bajeti ila kinachitokea hapo sasa ndiyo yaleyaleeee.

Au niwe nakunywa mwenyewe naona kampani ndiyo za kipumbavu japo tunashea matumizi.
Sasa nitoe pole kwa huyo anaeotea elf 30 alaf anaenda kulewea.

Nirudi kwako.

Maisha ya siku hizi kila mtu alipe bill yake, mfn mm kwa vinywaj navyokunyw siwez share bill na mtu nikiend ktk starehe.. tutaumizana tu.

Kama ni zile pombe za mataputapu/Gongo pamj na Serengeti.. Kilimanjaro etc ni sawa ku share bill.
 
Sijaelewa:

1. Ukiziweka bank zinatokaje?
2. Ukiziweka kwenye safe inakuwaje?
3. Au ukizikalisha zinabiringita?

Fafanua,

#When you spend your money kwenye expenses zako, acheni mawazo ya kishirikina.

Mtu unalipwa 1.5m, una IST, kazini ni 24 Km return, service, kodi, chakula, school fee, hela ikae imekuwa maji?

Mnakosa financial education na nidhamu mnakimbilia kwenye kulogwa.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Yani kabla ya mwisho wa mwezi nakuwa na mipango mingi sana tena ya maana mnoo. ila ukifika tu huo mwisho wa mwezi hela inavyopukutika sasa, hata sielewi.

Mitungi jamani mitungi jamani mitungiiiiiiiiiiiii aaaaagh.

Nakukuta tu balance niliyobaku nayo inatia huruma hapo ndo akili zinarudi hela yote ila nimetumia hivyo?

Eti wazee ni nini hiki?
Inategemea unagenerate kiasi gani versus matumizi yako. Isijekuwa unapata milioni kwa mwezi mzima halafu unaanza kulaumu chuma ulete ingali ukilamba kamshahara unapiga ulabu wa laki 2 siku ya kwanza tu ya mshahara. Make more money
 
Achana na imani za kishirikina.
Huna bajeti inayolingana na kipato chako mkuu...
Weka bajeti kabla ya kupata maokoto ya aina yoyote ile, usisahau akiba ya kukusaidia wakati wa shida ...period
 
Yani kabla ya mwisho wa mwezi nakuwa na mipango mingi sana tena ya maana mnoo. ila ukifika tu huo mwisho wa mwezi hela inavyopukutika sasa, hata sielewi.

Mitungi jamani mitungi jamani mitungiiiiiiiiiiiii aaaaagh.

Nakukuta tu balance niliyobaku nayo inatia huruma hapo ndo akili zinarudi hela yote ila nimetumia hivyo?

Eti wazee ni nini hiki?
Umeshasema mitungi Sasa nani amekuchezea
 
Back
Top Bottom