Wazee naombeni msaada, mwili wangu unatoa sana jasho tiba ni nini?

Wazee naombeni msaada, mwili wangu unatoa sana jasho tiba ni nini?

Nikitembea tu kidogo jasho kibao hata kama kuna baridi vipi. Mfano kukiwa na baridi yani ile baridi haswa naweza nikatembea fresh tu ila nikifika tu sehem nilipokua naelekea labda dukani au sehemu yoyote nikisimama tu jasho hizoo zinaanza kutiririka tena nyingi tatizo linaweza kuwa ni nini?

Nikiendaga mikoa yenye joto kama Dar es salaam ndiyo balaa hata nikae muda mrefu vipi kwamba labda mwili utakua umezoea lakini wapi yani huko ndiyo natembeaga huku najifuta futa mpaka leso yote inaloa chapa chapa.

Mwili wangu ni wa kawaida tu wala sio mnene kabisa mpaka naona sasa hili lishakua ni tatizo. Najua humu kuna wataalam mtanisaidia namna ya kufanya. Kiukweli sijisikii vizuri na hii hali. Tatizo laweza kuwa nini wazee? Na nifanyeje kupambana na hii hali?
Pole sana.

Kutokwa jasho sana hata ktk hali ya ubaridi ni ishara kwamba kuna kitu hakiko sawa mwilini mwako.

Kuna visababishi vingi mfano shida ktk tezi ya dundumio (thyroid gland disorders).

Kwa TB kutokwa jasho pekee haitoshi kusema kwamba una TB bali kuna dalili zingine ambazo huambatana na hiyo kutokwa jasho sana hasa usiku.

Kwa hiyo fika hospital kwa daktari ujieleze na atakufanyia uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo cha tatizo lako na kutibiwa ipasavyo.
Kila lakheri.
 
Mzee vip kwa hio ulitaka utoe wese la kupikia au petroli
 
Back
Top Bottom