Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Hapana, huwezi. Inabidi uangalie udhaifu wa hoja za hukumu
Pagumu hap😵therwise wawe wameamua kumbeba
Lulu nakafahamu sana.Nilibahatika kuchovya enzi flani za perfect vision
Naomba Mungu amsaidie
 
Again ,maadam tunaishi kwenye nchi ya kusadikika hata maamuzi yake yatakuwa hivyo,kwa ushahidi gani uliotolewa mahakamani ?hakuna ripoti ya doctor?hakuna foresinc report kuhusiana na kesi hii,hakuna ripoti inayotuambia Kanumba alikufa kwa sababu zipi;na elewa ni muhimu jaji ajiridhie bila shaka kuwa mtuhumiwa aliuwa;ndio tatizo za mahakama zetu nazo kuendeshwa kimihemko.
Hayo yalikuwa ni maoni ya wazee tu, Mahakama pia ina nafasi yake ya kureason...na mahakama inaweza kukubaliana na maoni ya wazee au kuyakataa. Kama mahakama itaridhika kuwa Ushahidi wa kimazingira ulotolewa mahakamani ni myoofu (watertight) basi itamuhukumu ipasavyo na kama ikiona ushahidi huo bado unawacha shaka ya maana basi itamuachia huru.

Kikubwa zaidi tusubiri hukumu ya mahakama vyovyote itavyokuwa,lakini cha kuangalia zaidi ni reasoning za mahakama katika kumtia hatiani au kumuachia huru....nnachojua majaji ni watu makini sana,japo mapungufu kama wanadamu wengine hayakosekani.
 
Report ya uchunguzi wa mwili wa Marehemu ilisema amekufa kwasababu ya Brain Concussion.

Mtu hawezi kufa kwa kusukumwa, kupigwa, ajali etc. Kusukumwa, kupigwa, ajali etc kunaweza kusababisha mtu kuanguka, kujigonga na kupelekea mtu kuvuja damu kwa wingi, mtikisiko wa ubongo, kuvuja damu kwenye ubongo, mshtuko wa moyo na mengineyo yanayoweza kusababisha kifo. Hivyo, daktari hawezi kuthibithisha kifo kusababishwa na kuanguka, bali kifo kwa sababu mtikisiko wa ubongo etc.

That said, mahakama haiwezi kutumia sababu ya kifo kuhukumu bali kuoanisha sababu ya kifo na kisababishi cha sababu ya kifo/tuhuma za mauaji zinazomkabili mtuhumiwa. Kisababishi cha sababu ya kifo ndio hupimwa kisheria kama ilitokea kwa kukusudia au kutokukusudia kuua.

Kusema report ya Kifo cha Kanumba kuonyesha alikufa kwa concusion haina maana kuwa mtuhumiwa hakuhusika kuua kwa maana alisababisha sababu ya kifo, na ndio maana kakutwa na kesi ya kujibu ambayo sasa inasubiri hukumu.

Kwa vile sheria ni practice, basi lolote laweza kutokea kwenye hukumu, akahukumiwa vyovyote.
 
Mtu hawezi kufa kwa kusukumwa, kupigwa, ajali etc. Kusukumwa, kupigwa, ajali etc kunaweza kusababisha mtu kuanguka, kujigonga na kupelekea mtu kuvuja damu jwa wingi, mtikisiko wa ubongo, kuvujia damu kwenye ubongo, mshtuko wa moyo na mengineyo yanayoweza kusababisha kifo. Hivyo, daktari hawezi kuthibithisha kifo kusababishwa na kuanguka, bali kifo mtikisiko wa ubongo etc.

That said, mahakama haiwezi kutumia sababu ya kifo kuhukumu bali hutumia sababu ya kifo kama kuoanisha sababu ya kifo na kisababishi cha sababu ya tuhuma za mauaji zinazomkabili mtuhumiwa. Kisababishi cha sababu ya kifo ndio hupimwa kisheria kama ni lilitokea kwa kukusudia au kutokukusudia kuua.

Kusema report ya Kifo cha Kanumba kuonyesha alikufa kwa concusion haina maana kuwa mtuhumiwa hakuhusika kuua, na ndio maana kakutwa na kesi ya kujibu ambayo sasa inasubiri hukumu.

Kwa vile sheria ni practise, basi lolote laweza kutokea kwenye hukumu, akahukumiwa vyovyote.
Well said ,bila shaka utakuwa wakili msomi
 
nakubaliana nawe hukumu ipo kwa jaji sio wazee wa baraza,ila huo ushahidi wa kimazingira ni upi?elewa hakuna eye witness kwenye ile kesi kwa hiyo ripoti za doctor,foresinc zingetoa mwanga zaidi kuhusiana na kesi hii,sasa unaposema mazingira una maanisha nini?
Sasa mkuu tunaposema ushahidi wa kimazingira ndo tunamaanisha huko kukosekana kwa eye witnesses!

Kama huyo eye witness angekuwepo na akathibitisha kuwa alishuhudia tukio mwanzo mwisho,basi kusingekuwepo hiyo circumstantial evidence bali ni direct evidence...sasa hii direct evidence ndo ingekuwa funga kazi.
 
Mwenye ujuzi wa sheria kuua bila kukusudia hukum yake ni nini?
 
Kihalali hata hicho kifungo cha nje sio haki kwa Lulu, yangekua ni mazingira ya sumu tungeamini kua Lulu alifanya yake lakini sio tukio kama lilivyoripotiwa kutokea. Lulu kwa umri na umbo alilokua nalo kipindi kile ni vigumu kuiaminisha jamii kua anaweza kumua Kanumba kwa kipigo.
Uwe mwepesi wa kuelewa na kutofautisha kati ya mauaji na mauaji ya bila kukusudia, Lulu kesi ya yake ni mauaji ya bila kukusudia ambayo inawezekana hata kuachiwa huru au kufungwa
 
Nkanini ACHA UONGO WAKO, RUFAA HAIPATIKANI KWA 'DISCRETION' YA JUDGE.

RUFAA NI HAKI YA MTU, JUDGE ANAVYOITAMKA HAKI YA RUFAA NI KWAMBA ANAMKUMBUSHA MUATHIRIKA WA HUKUMU HAKI YAKE NA SYO KWAMBA JUDGE NDYO ANATOA HAKI.

JUDGE HANA UWEZO WA KUMZUIA MTU KUKATA RUFAA.

HAKUNA KOSA/HUKUMU ISYO NA RUFAA ISIPOKUWA TU KAMA HUKUMU ITAKUWA IMEFIKIA KIWANGO CHA MAHAKAMA YA JUU KABISA (KWA TZ NI COURT OF APPEAL)

HATA HVYO, MBADALA WA RUFAA NI 'REVIEW, LAKIN REVIEW SYO HAKI (MPAKA JUDGE ARIDHIE)

KUHUSU BRAIN CONCUSSION, HUTOKEA ENDAPO MTU AMEANGUKIA KISOGO AU KUPGWA KISOGON, NA SYO LAZMA UPGWE KWA NGUVU.

KWA HYO INAWEZEKANA KANUMBA ALIANGUKA MWENYEWE AKAFIKIA KISOGO AU ALIPGWA KISOGONI.
MBONA HUJAMALIZIA NA HII MKUU?

"HUWENDA PIA ALISUKUMWA NA KUANGUKIA/KUJIGONGA KISOGONI"
 
Attitude inaweza kuwa imemponza

Ni kweli kabisa, alitakiwa awe kama mtu aliyesingiziwa asisikilize maneno ya mawakili, alitakiwa aende pale amesuka twende kilioni. Ni wazo nililokuwa nalo tangu zile picha zilipoanza kumiminika mitandaoni
 
Nakumbuka miaka ya 2000 mwanzoni huko Arusha maeneo flani hivi kuna kijana aliua kwa kumchoma kisu kijana mwenzake kisa, huyo muuaji kwao kulikuwa kunauzwa maji ya bomba sasa marehemu alikuwa ni mteja wao wa maji siku ya tukio marehemu alikwaruzana na huyo kijana muuza maji, bila kutarajia muuza maji akamchoma kisu mwenzake akafa akipelekwa hospita, huyu kijana alikaa ndani miezi sita tu akachomolewa kwa kuwa alikuwa na miaka 17, na watu walishangaa sana ila ilisemekana kwa kuwa alikuwa na undugu na yule jamaa aliekuwa kwenye tume ya uchaguzi nae ni mwanasheria mkuu, wakahisi labda rushwa ila mpaka leo jamaa anadunda mtaani. Wale ndugu wa ,arehemu nao hawakuwa na la kusema ila nadhani walifanya yao maana jamaa hapo kwao kawa msumbufu haswa chizi si chizi mvutabangi wala hana akili timamu kabisa. Hii ya lulu tusubiri tu siku ya hukumu.
 
Wanasheria nisaidieni, kwa mfano familia ya kanumba ingeamua kusema kuwa wao wanamuachia Mungu au kwa sabbu yoyte ile hawana haja ya kuendelea na kesi na wanapeleka ombi la kuifuta kesi kama walifungua wao, na wasingeshiriki ktk kutoa ushahidi wwte ule je Jamhuri ktk mazingira kama hayo hiyo kesi proceedings zake zikoje.
Lulu hajashtakiwa mahakamani na familia bali ameshtakiwa na Jamhuri ila siyo yule Kiwelu.
 
Wanasheria hatu comment kwa yaliyo mahakamani subiri hukumu itoke ndo kazi yetu itaanza
 
Back
Top Bottom