Tuaminishe wewe nani alimuua Kanumba kama siyo hicho kitoto. Jaribu kufuatilia mwenendo wa hii kesi, Lulu kaonyesha namna Mahakama zetu zilivyo na Double Standard, na sidhani kama hii case itakuja tumika kama precedent huko mbele ni.
JPM alikuwa sahihi sana na huu muhimili pamoja na Wanasheria wa Serikali, unaruhusuje mtuhumiwa kubadilisha maelezo ya utetezi tofauti na yale aliyotumia jitetea hatua za awali!
Huyu mtoto alikana kuwa na Mahusiano ya Ngono na Kanumba katika hatua za mwanzo za usikilizwaji wa hii kesi
LEO HII ANAKUBALI KUWA ALIKUWA MPENZI WA KANUMBA -Tafsiri yake ni kuwa Kibatala na Msando waliosema wapo nyuma yake wamem_coach...
Lulu huyu huyu aliiambia mahakama kuwa alipomkimbia Kanumba ndani alipanda gari na kuelekea Coco Beach (Aliendeshwa na mmoja wa wenzie walio kuwa wanamsubiri nje) leo hii anasema Ali_drive mwenyewe! Bado Mahakama na Mwanasheria wa Serikali wanaona sawa tu! Maelezo ya mtu aliyeua pasipo kukusudia hayawezi kupinda kwa kiwango hiki, Lulu alifundishwa namna ya kusema Mahakamani as if yupo kutengeneza Movie
Mwanasheria wa Serikali hajaona haja ya kumuuliza Lulu wale wenzie alioenda nao kwa Kanumba walio ondoka baada ya Muda gani, na jee alipata muda wa kuonana nao tena, pia anaweza waleta Mahakamani ili mahakama Ione kama wanachochote cha kuiambia mahakama, hasa kipindi anadukuliwa na Kanumba..
Ukweli hii kesi imeidhalilisha KADA YA SHERIA VIBAYA MNO.
Lulu kaua vitu viwili kwa Mpigo, Kamuua Kanumba gwiji wa Filamu za Kibongo, na hakuishia hapo KAUA BONGO MOVIE PIA
Kihalali hata hicho kifungo cha nje sio haki kwa Lulu, yangekua ni mazingira ya sumu tungeamini kua Lulu alifanya yake lakini sio tukio kama lilivyoripotiwa kutokea. Lulu kwa umri na umbo alilokua nalo kipindi kile ni vigumu kuiaminisha jamii kua anaweza kumua Kanumba kwa kipigo.