Wazee wa Kataa ndoa na kitabu cha The Manipulated Manby Esther Vilar (1971) wamenifikirisha Sana

Wazee wa Kataa ndoa na kitabu cha The Manipulated Manby Esther Vilar (1971) wamenifikirisha Sana

Ndugu zangu kuna siri imejificha miongoni mwa wanawake ambao ni walimu , kuna namna hata kama kazaliwa mwaka 2000 anakua tofauti na hawa watoto wa penda pesa, vinguo vya hovyo na tamaa kedekede.

Kuna namna ukidate hata na mwanamke mwalimu awe kaajiriwa, kajiajiri au hajaajiriwa au yupo chuoni anasomea masomo ya ualimu kuna mazingira ukipita nae unaona kabisa hapa nipo na mwanamke chuma kweli kweli tena anayejitambua sana, moyo unakushuhudia kabisa hawa ndio wake wa kuoa.

Wanawake walimu wametofautiana san kimaadili na hawa wanawake wengine , wanajua wanachokifanya na mara nyingi hawafanyi kitu kwa kukurupuka, ukikaa ukatuliza akili utaona kabisa hapa amefanya hivi baada ya kufikiria sana

Ukidate / kuoa mwanamke mwalimu anajua kabisa wewe unatakiwa ufundishwe hata kama mwanaume una akili kuna namna ukiyapiga picha mahusiano yenu utaona mahusiano yenu /ndoa yenu anaipeleka kama anaongoza darasa la wanafunzi wanaohitaji kujifunza ili wa elewe na wafanikiwe kufika mbele.

Wanawake walimu kuna namna wanakua na amri/ ukali wenye masikitiko ndani yake , hata kama umefanya jambo baya kuna namna atakuelekeza kwa upole ila ndani yake utaona kunatoka tone za amri na masikitiko zinazokutaka wewe uache kufanya uo ubaya unao hangaika nao kila siku

Wanawake walimu kuna namna hawapendi purukushani mbele za jamii, kuna namna wanaishi kwenye jamii ili kuwa mfano wa kuigwa kama walimu, kuna namna hata ukiwa nae kwenye mahusiano utaona tuu anajiweka katika mazingira ya kulinda heshima yake ili iweze kusomwa vyema na jamii.

Wanawake walimu ni wanawake wanao kwenda na muda na mahesabu makali, hawezi kufanya vitu nje ya muda wala nje ya mahesabu mliyokubaliana kuyafanya, utakuja gundua mahusiano yenu anayapeleka kwa muda na mahesabu makali sana kwaajili ya kulinda future za baadae.

Wanawake walimu ni walezi wazuri na bora watoto na familia, pia ni walezi wazuri wa mume anamchukulia mwanaume kama mtoto anayehitaji kufundishwa

Wanawake walimu ndani yao ukichunguza sana utagundua ndani yao hawana ubaguzi, hawachagui wanaume wa hali ya juu sana kiuchumi, wao wanapendelea sana wanaume wa kawaida na wacha Mungu, wanapendelea wanaume wanao jiheshimu na kujitambua ila wawe ni wanaume wa kawaida sana tena wenye uchumi mdogo.

Hata ukimwambia wewe ni mpambanaji, kinyozi, bodaboda, mfanya usafi, mlinzi, kibarua viwandani, mpiga tofali ni ngumu sana kukukataa kirahisi maana anaona wewe ni kama darasa lenye wanafunzi wanaofeli hivyo wanapaswa kusaidiwa kunyanyuka kwenda juu.

Ndugu zangu, wanawake walimu ni wake bora sana , haijalishi kazaliwa mwaka 2000 ila ni wanawake bora sana kuoa na kuwaweka ndani.

* Kataa ndoa hawakatai kuishi na mwanamke wanakataa ule mkataba wa ndoa utakao watia nguvuni, wanawake walimu wanaamini hata ule mkataba wa ndoa ni makaratasi tuu kama mitihani ya wanafunzi wanayo sahihisha kila semister/ midterm*
Nimeipenda hii
 
Unasambaza ujinga tu kwa vijana , ndoa ni hitaji la asili kwa mwanadamu Kuna muda utafika utatamani tu.
Ngono ni hitaji la lazima, ndoa siyo hitaji la lazima kwa mwanadamu.
Watu waliopo katika ndoa lazima wakubali mawazo mbadala na siyo ujinga kutofautiana mitazamo.
 
Kwanza tujue huyu mwandishi wa kitabu hiki aliliolewa na kuzaa watoto au alizaa watoto na masela akaachiwa alee mwenyewe? Tujue pia anaamini na kuabudu dini gani isiyotambua umuhimu wa ndoa? Au kwao wanawake hutunza waume zao? Na je anasemaje kuhusu mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume hufanyikaje?
Dini zilianziabkwao na ndoa za kidini zianzia kwao anazijua kuliko wewe uliyeletewa. Kuhusu hayo mengine alimyazama mumewe na kuandika kitabu
 
Back
Top Bottom