Nimeusoma waraka ulioandikwa na wanaojiita wazee wa Kigoma nikastaajabu sana. Waraka huo batili una kichwa kisemacho _"WAZEE WA KIGOMA TUNAMUONYA SPIKA NDUGAI KWA MARA YA MWISHO"_.
Kwakweli waraka huo hauendani na maadili waliyonayo wazee wa Kigoma ndio maana sitaki kuamini kuwa umeandikwa na wazee hao. Bila shaka utakua umeandikwa na Zitto Kabwe au na baadhi ya wazee wachache wa ACT kwa maelekezo ya Zitto.
Kwanza, walioandika waraka huo wanatetea zinaa wakisema wasichana waruhusiwe kushika mimba kabla ya kuolewa kisha waendelee na masomo. Wazee wa Kigoma ninaowajua mimi hawawezi kutetea zinaa kama afanyavyo Zitto.
Pili, wazee wa Kigoma wana ufahamu mchache wa jinsi Bunge linavyoongozwa na kwamba maneno ya wabunge ndani ya bunge tukufu yanalindwa na sheria, hivyo hawawezi kutaka mmoja wa wabunge ashitakiwe kwa maneno aliyoyaongea bungeni.
Tatu, wazee wa Kigoma walikua miongoni mwa watu waliompongeza Baba wa Taifa kwa kuanzisha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima huku wakisema kuwa kumuweka mzazi darasa moja na msichana ni kuchochea uharibifu wa maadili. Hivyo basi, maneno ya kusema msichana aliyefanya uzinzi akapata mimba aende kusoma na wasichana, hayawezi kuwa maneno ya wazee wa Kigoma.
Kwahiyo, tunamuomba Zitto asiwasingizie wazee wetu ambao wana watoto wenye umri kuliko yeye. Akiandika maneno yake ya kisaliti, atumie jina lake kama alivyofanya Benki ya Dunia. Asitumie majina ya wazee wetu wa Kigoma.