Wazee wa Kigoma wasimama na Zitto na kutoa tamko dhidi ta Spika na Bunge

Ngoja niwaoneshe walivyokuwa wanahaha kutafuta location mitaani Kigoma 😅😅😅😅😅
 

Attachments

  • 3a57924cd8ce4e0bae327e928fe0af98.jpg
    122.7 KB · Views: 2
Nimeusoma waraka ulioandikwa na wanaojiita wazee wa Kigoma nikastaajabu sana. Waraka huo batili una kichwa kisemacho _"WAZEE WA KIGOMA TUNAMUONYA SPIKA NDUGAI KWA MARA YA MWISHO"_.

Kwakweli waraka huo hauendani na maadili waliyonayo wazee wa Kigoma ndio maana sitaki kuamini kuwa umeandikwa na wazee hao. Bila shaka utakua umeandikwa na Zitto Kabwe au na baadhi ya wazee wachache wa ACT kwa maelekezo ya Zitto.

Kwanza, walioandika waraka huo wanatetea zinaa wakisema wasichana waruhusiwe kushika mimba kabla ya kuolewa kisha waendelee na masomo. Wazee wa Kigoma ninaowajua mimi hawawezi kutetea zinaa kama afanyavyo Zitto.

Pili, wazee wa Kigoma wana ufahamu mchache wa jinsi Bunge linavyoongozwa na kwamba maneno ya wabunge ndani ya bunge tukufu yanalindwa na sheria, hivyo hawawezi kutaka mmoja wa wabunge ashitakiwe kwa maneno aliyoyaongea bungeni.

Tatu, wazee wa Kigoma walikua miongoni mwa watu waliompongeza Baba wa Taifa kwa kuanzisha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima huku wakisema kuwa kumuweka mzazi darasa moja na msichana ni kuchochea uharibifu wa maadili. Hivyo basi, maneno ya kusema msichana aliyefanya uzinzi akapata mimba aende kusoma na wasichana, hayawezi kuwa maneno ya wazee wa Kigoma.

Kwahiyo, tunamuomba Zitto asiwasingizie wazee wetu ambao wana watoto wenye umri kuliko yeye. Akiandika maneno yake ya kisaliti, atumie jina lake kama alivyofanya Benki ya Dunia. Asitumie majina ya wazee wetu wa Kigoma.
 
Jaribuni kumgusa Zitto muone kama atanuka au la. Maneno mengi ya nini?
Hao wazee wamesema watashtaki kwa Mungu, sasa kwa kuwa Mungu hapendelei wala kuonea mtu shida yenu ni nini?
 
Kwahiyo wewe siku zote unayajua mawazo ya wazee wa Kigoma? au unataka kusema hao wazee wa Kigoma ni kama mawe huwa hawabadiliki misimamo yao?!

Naona hata wewe umetumwa tu, sioni cha maana ulichoandika!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi tuseme waraka huo haujaandikwa na wazee wa mwisho wa reli ila umeandikwa na wazee wa lumumba
 
Wacha kuweweseka wewe lumumba, tulia dawa iwangieni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…