Wazee wa Kwamsisi Handeni walitaka sado tatu za mate ya binadamu!

Wazee wa Kwamsisi Handeni walitaka sado tatu za mate ya binadamu!

Mizimu ni nini na inaishi wapi?

Tambiko ni aina ya uganga wa kienyeji/ulozi na uganga wa kienyeji ni aina ya uchawi...

Hayo makololo uliyotaja ni sadaka ya kukamilisha.moja ya ibada ya kichawi iitwayo tambiko...
Watu walokufa zamani,, hata wewe ukifa unakua mzimu, in short roho haifagi kinachokufa ni mwili tu
 
Hapana siyo serikali bali ni washirikina wanajipeleka huko wakiamini watalinda nafasi zao au kupata uteuzi au kushinda chaguzi!
ni serikali, uchaguzi wa Mwaka 2015 Kijani walimtupa "Ma rope senior" kwenda naija kuleta mganga
 
Tofauti ya mkoa na tangu unaiona mpakani Mwa Tanga na kilimanjaro,same,mwanga pakame lakini pana uhai nyumba za bati tele,Tanga kwenye rutuba nyumba aibu karne hii bado wanaishi kwenye tope na nyasi,yaani hata kuchoma tofali na kutengeneza vigae vya udongo hawawezi, wanahitaji fimbo.
Hao inahitaji wapigwe mijeledi ya kutosha
 
Mbali na Shs. milioni 21 walizozidai wazee wa kijiji cha Kwamsisi pia walitaka sado tatu za mate ya binadamu ili waruhusu ujenzi wa barabara ya Afrika ya mashariki.

Baada ya kubembelezwa kwa muda mrefu na Mkuu wa wilaya ya Handeni wazee hao wameamua kuondoa madai hayo na sasa watalipwa Shs milioni moja na nusu.

Maoni: Hivi kweli serikali bado inaamini ushirikina kiasi cha kutishiwa na wazee wa Kwamsisi? Je serikali imekuwa ikilipa fedha za namna hii katika miradi yake yote inayotekeleza?
Serikali nayo inapenda kuendekeza vitu vya kipuuzi.
Hivi hawa wazee hawaoni kinyaa kutaka mate tena kwenye ndoo 😓
 
Back
Top Bottom