Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?


Nakubaliana na huu mrejesho kwa kweli. T1 ni changamoto kubwa. Pia, kuna many growing towns kama (Mikumi, Tanangozi, Mafinga) unakuta malori yanapaki barabani kwa sababu hayana mahali pa kuwekwa. Barabara yenyewe tayari nyembamba! It is very dangerous.
 
 
Kweli kabisa mkuu wale vijana ni wanauza karanga zao masaa yote!

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba zile karanga wamezichambua kwa uweledi wa hali ya juu!
Unaweza kuzitafuna hata gizani bila shida..

Hiyo ni njia yangu kuu kwenye kusaka ugali so mara kadhaa nimelala pale baada ya kukuta parking ya ruaha mbuyuni imejaa..
 
Safi sana mkuu, pia pako salama kulala pale
 
Wenye maamuzi wanapiga king'ora unakaa pembeni wao wanapita tu.

Nyie mtafuata sheria zote.
 
In my next road trip to Iringa, ntasimama kununua karanga na mimi. Niwaunge mkono vijana wetu wanaaopambana.

Ila Mahindi ya kuchoma pale baada ya kupandisha Kitonga sinunui! Yaani wote wauzaji na wanunuzi kwenye magari mpaka washike shike muhidi wote - eti wanachagua; Nilitaka kutapika kwa kuangalia tu what happened~
 
 
Mimi humu ni msindikizaji tu sijui kama Kuna siku nitamiliki gari yangu binafsi kila nikipiga hesabu naona daah sio leo wa kesho..kila la heri mnaomiliki vyombo.
Weka nia ya kumiliki usafiri wako, usikate tamaa kwenye utafutaji pia..

Hali ya kutokuwa na gari isikufanye ujione msindikizaji, zaidi iwe ni chachu kwenye mapambano yako!!!
 
Hope utazifurahia sana hizo karanga mkuu!!

Yale mahindi hata mimi nayaogopa mkuu, nikiwa na hamu na mahindi choma huwa namwambia amenye kisha achome nikiwa naona..

Hako kakituo wanakochoma mahindi baada ya kumaliza mlima, kanaitwa IKOKOTO!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…