Tuwe makini nyakati zote za usiku, kicheche kinaweza kukuletea majanga hata kama hakipo upande wako. Segera hiyo mida yetu ya kutawala
View attachment 3000155
Hao wenye Lori lililoharibika sio waungwana.....
Walitakiwa waweke matawi ya miti pande zote kuashiria gari zinazokuja kuna hatari wapunguze mwendo ili hata wanao overtake wawe kwenye mwendo mdogo hadi wapite eneo la hatari.
Kuna siku nilifanya safari ya hasira za mkizi, miaka kadhaa huko nyuma....
Kuna watu walinikera, mchana wa jua kali nikatoka kwenye kitongoji nilichopo kuelekea Bagamoyo. Saa nane mchana nikawa kituo cha mafuta BP pale baada ya round about.
Nikaweka full tank, nikaanza safari... niliingia Tanga mjini saa moja kasoro usiku. Nilipanga kulala, ila saa tatu usiku nikaanza safari ya kurudi Dar. Nilikunywa Redbull 2 macho yakawa kama fundi saa...
Nilikuwa nasimamishwa kwenye vizuizi vya checkpoint nashusha vioo, nasalimia wananiuliza unatoka wapi unaenda wapi najibu huyooo natambaa.... spidi inapunguzwa kwenye tuta tuu baada ya hapo ni kunyoosha goti.
Saa saba kasoro usiku niko tena kituo cha mafuta BP pale Bagamoyo kuweka mafuta maana mshale ulikuwa umelala empty.
Tanga sikuweka mafuta, niliingia kitongojini kwangu saa nane usiku. Sina hamu maana, kuna muda nilijuta kwanini niliendekeza hasira, ila kesho yake nikasikia raha kwa kuwa nilienda nikarudi salama.
Usiku mnene unatisha hasa ile barabara ya Msata Bagamoyo, kiza kinenee nikawa nawaza, nikipata pancha hapa ndo basi tena....😁.
Sikurudia na wala sitakaa nirudie tena huo mchezo.
Akili za Kasinde 🙂.