Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ni kweli. Watu walikuwa wanaogopa sana gari za cc2500! Angalia leo Crown ndio saloon car ya kawaida!
Ila kuna watu wenye hizo crown utawaone huruma wanavyo lalamika utafikiri walipewa hizo gari 😀😀😀😀.. mtu unasikia bora nirudi kwenye ka Sentanta kangu au ka ist .. ila yote huo ni uoga. Pia watu kuwa na matumizi ya gari pasipo sababu za msingi ndio hawa wanalaumu sana. Kama gari unaitumia katila mambo ya msingi hata siku moja huwezi lalamika wese
 
Sometimes unaepusha mengi kukubali kuonewa. Usiombe upewe kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake!
kipindi cha JK kuna mshkaji ye walimkamata road akawa anabishana nao baadae akawaambia nyie badala mkapambane na majambazi mnakuja kujaa huku barabarani kutuonea tu,aisee alifikishwa kituoni nguo zake zimeshachakaa tayari akapewa na kesi nyingine serious sana.

Aliteseka sana yule mwana.
 
Hio mifano yako miwili ndio nilichosema be humble. Ukikosea tu mwanzo ujue utaandikiwa hata kama huna kosa
 
Hii unakuwa ubavuni kwa mtu, unaiminya accelerator pedal mpaka chini, mashine inarudi gia moja nyuma halafu inatoa mlio kama simba
Hii huwa tamu sana, nilienda bagamoyo majuzi kuna ka sehemu kazuri.. gari ijuta kunijua... 😃😃😃😃😃 kwa vipande vipande vile vile.. nilikuwa nasubiri gari zinajipanga.. nacheki kwa mbalii.. nakibinya hadi mwisho pwaaa nazipita gari zote.. alafu mbele nazisubiria
 
Tatizo mliwadanganya kuwa zinatumia mafuta vizuri sana! Waambieni ukweli ukiendesha Crown vile inatakiwa lazima uone tofauti na Premio ila ukiiendesha kama Passo ndio utaona mafuta yanatumika kama Premio.
Sasa kwanini ununue Crown halafu uendeshe kama IST? Afadhali ununue IST tu
 
In reality-Wakati wa JK si wakutolea mfano kabisa juu ya ufwataji wa sheria-Ndiyo kipindi ambacho hawa watu walikuwa wanazabwa vibao kituoni kwao kabisa na raia wa kawaida na hakuna kilichokuwa kinafanyika cha maana.
 
Wanaambiana crown ipo vizuri ndani, ina kimbia, mala ipo stable road.. ila hawataki sikia mafuta
 
Ukiambiwa ufuate njia husika kupeleka malalamiko yako ndo utajua hujui.

Bora umalizane nae uondoke.

Hakuna polisi wa kumshtaki polisi mwenzake.

Kitu kidogo unaweza fuatilia hata miaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…