Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ni kweli. Watu walikuwa wanaogopa sana gari za cc2500! Angalia leo Crown ndio saloon car ya kawaida!
Ila kuna watu wenye hizo crown utawaone huruma wanavyo lalamika utafikiri walipewa hizo gari 😀😀😀😀.. mtu unasikia bora nirudi kwenye ka Sentanta kangu au ka ist .. ila yote huo ni uoga. Pia watu kuwa na matumizi ya gari pasipo sababu za msingi ndio hawa wanalaumu sana. Kama gari unaitumia katila mambo ya msingi hata siku moja huwezi lalamika wese
 
Sometimes unaepusha mengi kukubali kuonewa. Usiombe upewe kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake!
kipindi cha JK kuna mshkaji ye walimkamata road akawa anabishana nao baadae akawaambia nyie badala mkapambane na majambazi mnakuja kujaa huku barabarani kutuonea tu,aisee alifikishwa kituoni nguo zake zimeshachakaa tayari akapewa na kesi nyingine serious sana.

Aliteseka sana yule mwana.
 
Mzee baba unaishi bongo kweli?

Hizo unazosema ni theories tu,mimi kipindi kile cha lugola amesema( sijui ukikutwa na kosa la taa ni mbovu,side mirror mbovu,rangi imeisha hilo ni kosa 1 tu la uchakavu na sio makosa matatu) nilikamatwa kule Tegeta nikiwa na kosa la taa 1 mbovu nikakuta traffic wamemshikilia jamaa mmoja ana harrier old model yuko anabishana nao huku amewatolea simu wale maafande kwamba Lugola anasema hivi na bla bla blah kibao.

Mimi walivyonifata nikawaambia ni kweli afande taa yangu kweli ni mbovu lkn kwa sasa siko njema mfukoni lkn w/end hii salary itaingizwa nitatengeneza afande,nikaomba samahani.

Afande akaniambia jitahidi uitengeneze na sikutoa hata senti,yule jamaa aliyekua anabishana nao mambo ya Lugola akaandikiwa makosa mawili na akaambiwa mpige huyo Lugola mwambie tumekuandikia na pia na No. ya RTO hii hapa mpigie huko mbele ya safari mueleze tumekuandikia kibabe maana tunapendaga wajuaji kama nyie.

Ninajua sehemu ya ku react na mipaka yangu inaishia wapi.
Hio mifano yako miwili ndio nilichosema be humble. Ukikosea tu mwanzo ujue utaandikiwa hata kama huna kosa
 
Hii unakuwa ubavuni kwa mtu, unaiminya accelerator pedal mpaka chini, mashine inarudi gia moja nyuma halafu inatoa mlio kama simba
Hii huwa tamu sana, nilienda bagamoyo majuzi kuna ka sehemu kazuri.. gari ijuta kunijua... 😃😃😃😃😃 kwa vipande vipande vile vile.. nilikuwa nasubiri gari zinajipanga.. nacheki kwa mbalii.. nakibinya hadi mwisho pwaaa nazipita gari zote.. alafu mbele nazisubiria
 
Ila kuna watu wenye hizo crown utawaone huruma wanavyo lalamika utafikiri walipewa hizo gari 😀😀😀😀.. mtu unasikia bora nirudi kwenye ka Sentanta kangu au ka ist .. ila yote huo ni uoga. Pia watu kuwa na matumizi ya gari pasipo sababu za msingi ndio hawa wanalaumu sana. Kama gari unaitumia katila mambo ya msingi hata siku moja huwezi lalamika wese
Tatizo mliwadanganya kuwa zinatumia mafuta vizuri sana! Waambieni ukweli ukiendesha Crown vile inatakiwa lazima uone tofauti na Premio ila ukiiendesha kama Passo ndio utaona mafuta yanatumika kama Premio.
Sasa kwanini ununue Crown halafu uendeshe kama IST? Afadhali ununue IST tu
 
kipindi cha JK kuna mshkaji ye walimkamata road akawa anabishana nao baadae akawaambia nyie badala mkapambane na majambazi mnakuja kujaa huku barabarani kutuonea tu,aisee alifikishwa kituoni nguo zake zimeshachakaa tayari akapewa na kesi nyingine serious sana.

Aliteseka sana yule mwana.
In reality-Wakati wa JK si wakutolea mfano kabisa juu ya ufwataji wa sheria-Ndiyo kipindi ambacho hawa watu walikuwa wanazabwa vibao kituoni kwao kabisa na raia wa kawaida na hakuna kilichokuwa kinafanyika cha maana.
 
Tatizo mliwadanganya kuwa zinatumia mafuta vizuri sana! Waambieni ukweli ukiendesha Crown vile inatakiwa lazima uone tofauti na Premio ila ukiiendesha kama Passo ndio utaona mafuta yanatumika kama Premio.
Sasa kwanini ununue Crown halafu uendeshe kama IST? Afadhali ununue IST tu
Wanaambiana crown ipo vizuri ndani, ina kimbia, mala ipo stable road.. ila hawataki sikia mafuta
 
Kiuhalisia ni kwamba Traffic hapaswi kutafuta kosa kwenye gari-Anapaswa kujua kwa nn anakusimamishia na siyo kuibua problems kichwani kwa kuhisi.Wabongo shida yetu ni kwamba hatujui wajibu wetu na haki zetu hasa tunaposimamishwa na traffic & appropriate channels za ku escalate mambo yetu pale tunaposhindwa kuafikiana.Hon. Kangi Lugola alitufumbua sana macho wananchi juu ya haki zetu pamoja na wajibu wa traffic na ndiyo maana hawa jamaa wa wa usalama barabarani hawakumpenda hata kidogo.
Ukiambiwa ufuate njia husika kupeleka malalamiko yako ndo utajua hujui.

Bora umalizane nae uondoke.

Hakuna polisi wa kumshtaki polisi mwenzake.

Kitu kidogo unaweza fuatilia hata miaka.
 
Back
Top Bottom