Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Lazima ilijaa uchafu karibia kuziba

Gari nyingi ndogo full tank inatoboa Dar-Arusha. Kuepuka usumbufu unajaza tank tu
Gari yangu nikiweka full tank pale Total Mcity, taa ya mafuta inaniwakia Sanawari kabla sijafika Mianzini.

Ila mara nyingi napenda nikifika Korogwe na Moshi najazia just in case arusha kukakosa mafuta.

Kuna siku tulifika Moshi mjini tukakosa mafuta mji mzima.
 
Stability inapotea kwa ku tweak suspension parts sio horsepower na torque. Kama ni hivyo zile subaru zenye turbo zingekuwa zinaanguka maana sti zina kibati cha mpaka 280kph na haziyumbi.
Nilishawahi drive Carina Ti 1500cc to 140km/hr gari ikawa inaanza kukosa stability,Swali nililojiuliza ni Je,itakuwaje kwa mtu anayeendesha Carina Ti 2200cc ambayo i think ni Turbo charged akaenda 180km/hr sijawah pata majibu.
 
Niliikuta imejaa tope,nikaambiwa sababu ya kutumia mafuta mpk tank linaisha ambako chini kunakuwa na uchafu..au kuweka mafuta kidogo wakati tank lina mafuta kidogo Sana.So yanaenda tibua tu..
Sema mi nilishusha tank likasafishwa about 3 weeks ago. Halikuwa na residue zozote. Ila sasa imezalisha tatizo jengine baya kweli. Gauge yangu inanipa false readings. Sijui hata ishu ni nini tena maana pump iko sawa ila toka iliporudishiwa wakati wanafunga tank ikawa inasoma empty kabisa hata baada ya kuweka full tank.

Nikaenda kwa fundi kufungua tena pump na kuigeuza pengine ilifungwa upande sio ikawa inasoma ila ilikuja kuniadhiri Jangwani pale sitasahau tena nikiwa na bibie. Ikabidi nitie triangle nipande fire na kidumu. Sasa sielewi sijui tatizo litakuwa nini kupelekea wrong readings
 
Puma nina bad experience nao sana.Nishakutana na incidence za kutaka kuibiwa mafuta vituoni mwao na other issues na zikawa resolved peaceful either at the station level or HQ.Total at least naona wanajielewa sana na sijawah kukutana na major incidence kwao.
Hizi kampuni kubwa zina ofisi kabisa.

Kama ukipata shida kuna mtu au department itakusaidia kushughulikia.

Kama umepata shida na mafuta yao unalipwa na kampuni.

Ila petrol station ndogo unaweza kuta mmiliki amepeleka ng'ombe machungani. Inabidi umsubiri akusikilize shida yako.
 
Nilishawahi drive Carina Ti 1500cc to 140km/hr gari ikawa inaanza kukosa stability,Swali nililojiuliza ni Je,itakuwaje kwa mtu anayeendesha Carina Ti 2200cc ambayo i think ni Turbo charged akaenda 180km/hr sijawah pata majibu.
Gari zetu wengi hatuzingatii wheel allignment and balancing. Ndio maana unakuta zinakuwa unstable na pia kuweka ma spacer kunaharibu sana stabiliy.
Gari ambayo haijakorokochwa suspension parts na height inakuwa stable mkuu hata ikiwa Corrolla 110!
 
Total kwangu ni best. Ila mafuta yake yanaungua kwa wepesi sana. Sio rafiki kwa Safari. Labda town trips tu.
Ndio maana napendelea Lake oil nikisafiri. Nimetoboa Dar-Mbeya na wese la 130K tu..with a 1.8L engine.
Mi nina 2.5L engine.

Dar - Arusha tu taa inaniwakia sijafika mianzini.

Total wana mafuta mazuri sana.
 
Sema mi nilishusha tank likasafishwa about 3 weeks ago. Halikuwa na residue zozote. Ila sasa imezalisha tatizo jengine baya kweli. Gauge yangu inanipa false readings. Sijui hata ishu ni nini tena maana pump iko sawa ila toka iliporudishiwa wakati wanafunga tank ikawa inasoma empty kabisa hata baada ya kuweka full tank.

Nikaenda kwa fundi kufungua tena pump na kuigeuza pengine ilifungwa upande sio ikawa inasoma ila ilikuja kuniadhiri Jangwani pale sitasahau tena nikiwa na bibie. Ikabidi nitie triangle nipande fire na kidumu. Sasa sielewi sijui tatizo litakuwa nini kupelekea wrong readings
😃😃😃 noma sana, issue za vidumu
 
Hivi najiuliza hamnaga namna ya ku calibrate speed na kufunga console mpya yenye gauges ya zaidi ya 180 kph! Maybe kufunga ile inayofika hata 300KPH?
It sucks kwa kweli gari ina mashine kubwa ila iko limited to 180KPH yan kiasi kwamba usiku mkali tokea round about ya Mlimani unajikuta umeshafuta 180kph kabla hata ya flyovers za Ubungo. Kile kipande huwa najiachiaga sana.
Wale wanaofanya engine calibrate na tunings sio kwamba wanaongeza hizo kph ?
 
Back
Top Bottom