Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Inawezekana; maana kama Dom-Dar ni takribani kilomita 442, hivyo jamaa kama alikuwa akitembea kwa wastani wa 145-150 kph, masaa 3 anaweza. Ila kwa barabara zetu hizi na matuta ya viazi ya kutosha sijui kama ni realistic!

Yaani Dar-Dom kama linapatikana li Autobahn letu, hata masaa 2+ kwa mtu mwenye gari yenye 260+ inawezekana.
Kuna mashimo tu na ile migogongo ambayo inaharibu show ipo hasa mlandizi chalinze.. ila matuta naona kama yamekuwa madogo unayafukia na ukijua sehemu zenye mashimo kuna mda unatembea na 160kph tu 🙂🙂.. nilipoteza mda mlandizi baada ya kuona wakuda, ila nilipo imaliza pale mwendo wangu ulikuwa 160, narudi 140 na maeneo machache kwenye ukaguzi kama sehemu tatu nikakopeza mda.. nikakuta inefika masaa manne na nusu
 
Hiyo “migogongo” ndiyo ile mibonyeo? Aisee hiyo hata maeneo kabla na baada ya Gairo ipo. Siipendi kabisa hiyo.
 
Je, kuna aliyekutana na mauzauza barabarani yeye mwenyewe siyo kwa kuhadithiwa?

Iwe kwa safri za usiku ama mchana.
Aisee..kwa umri sijawa ila ninakumbuka nikiwa mdogo kama darasa la tano hivi, tulikuwa tunasafiri na gari la kampuni, tufika kwenye daraja flani niliona watoto kama watano hivi wanavheza ule mchezo wa kitoto unaitwa Ukuti ukuti wa mnazi..( Watoto wa leo wanaonyoa viduku hawawezi kujua mchezo huu, wao wanajua kubeti)

Nilishikwa na kigugumizi, sikuweza kusema chochote gari lilipopita sikusikia kishindo cha mtu kugongwa, nilipotazama nyuma sikuona chochote..
Tulikuwa tumekaa kwenye tela ya pickup..

Hicho nilichokiona sijui ndiyo mauza uza ya barabarani, sijui nilikuwa naota... mpaka leo najiulizaga ni nini kile..

Juzi kati nikapita eneo hilo peke yangu saa nne usiku naendesha gari... nikakumbuka yale niliyowahi kuyaona. niliogopa sana lakini sikuona kitu..
 
IMG_0437.jpg

Wazee wa location..
 
Unadhani huyu alikuwa anaenda speed ngapi?View attachment 1775511
Huyo alikuwa anatembea kati ya 140-150kph. Hapo hata gari ingekuwa na airbag 10 huchomoki. Usiku labda uwe umefunga LED sports light ndio utaweza tembea hizo speed, vinginevyo ni bora utembee mwendo wa mateka 80kph au upambane na vibao vya 50 mchana.
 
LED sport ligt zinapiga umbali wa mita ngapi ? nije nizifunge hizi nione mtiti wake
 
Back
Top Bottom